in

Nduda Atibua Dua ya Kifaru Jamhuri

Mtibwa

Makosa ya golikipa wa Mtibwa Sugar Said Mohamed Nduda yainyima Mtibwa Sugar kuondoka na alama tatu muhimu uwanja wa Jamhuri Morogoro dhidi ya Yanga.

Yanga imeambulia alama moja baada ya kulazimishwa sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Hii tunaweza kusema kuwa dua ya Kifaru  imedunda baada ya sare hiyo.

Kabla ya mchezo huo Msemaji wa Mtibwa Sugar  Thobias Kifaru  aliwaomba  mashabiki wa timu hiyo kuomba dua ili wapate ushindi katika mchezo huo ambao ulikuwa muhimu kupata alama tatu ili kujihakikishia kubaki ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Tanzania Sports
Dua ya Kifaru 

Mtibwa Sugar ilikuwa ya kwanza kupata goli dakika ya 28 ya mchezo baada ya beki wa Yanga Juma Makapu kufanya makosa na Haruna Chanongo kufunga goli .

Goli la kurudisha la Yanga limepatikana dakika ya 83 baada ya  Adeyun Saleh kupiga shuti nje kidogo ya eneo la hatari lililomshinda kipa Said Nduda.

Mtibwa Sugar sasa imefikisha alama 42 nafasi ya 14 ikiwa sawa na Mbao FC ikipishana kwa magoli ya kufunga na kufungwa.

Matokeo ya mechi nyingine, KMC  imepoteza goli 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons huku Mbao FC ikiichakaza  Namungo FC magoli 3-0.

Mwadui FC  imeicharaza goli 1-0 timu ya soka ya  Biashara United  wakati Singida United imeambulia kichapo cha magoli 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Azamfc

Yanga, Azam kucheza klabu Bingwa Afrika

Coastal Union

Simba kuzikosa alama tisini