in

Nchimbi na Sarpong wataipa Yanga SC ubingwa ?

Sarpong

Nilikuwa naitazama Yanga ikihangaika kupata ushindi dhidi ya Kagera Sugar. Walihitaji ushindi kwa sababu mchezo uliopita walipoteza alama mbili dhidi ya Mbeya City.

Hawakutaka kupoteza alama zingine dhidi ya Kagera Sugar tena kwenye uwanja wa nyumbani, mwisho wa mchezo Yanga walipoteza alama zingine mbili.

Siyo kitu kizuri kwao hata kidogo kwa sababu wako kwenye haraka za ubingwa. Harakati ambazo wanatakiwa wawe na mwendelezo mzuri wa kukusanya alama nyingi.

Simba ambao ndiyo wapinzani wa karibu wa Yanga wako nyuma ya michezo mitatu dhidi ya Yanga mpaka sasa hivi wakiwa na alama 39, ndani ya michezo 17.

Yanga wamecheza michezo 20 mpaka sasa hivi wakiwa na alama 46. Wako mbele ya michezo mitatu dhidi ya Simba. Kama Simba watashinda michezo mitatu watakuwa na alama 38.

Alama ambazo zitawaweka Simba kileleni kwa tofauti ya alama 2 dhidi ya Yanga. Wakati jana naitazama Yanga ikipambana kutopoteza alama yoyote kitu pekee kilichokuwa kinakuja akilini kwangu ni washambuliaji wa Yanga.

Aina ya washambuliaji wa Yanga ni tofauti na aina ya washambuliaji wa Simba ambao ni wapinzani wao wakubwa kwenye mbio za ubingwa barani Afrika.

Mfano, Simba washambuliaji wake wawili Meddie Kagere na John Bocco pekee, hapo achana na Chris Mugalu. Washambuliaji hao wawili ndiyo wanaoongoza katika mbio za ufungaji bora.

Meddie Kagere amefanikiwa kufunga jumla ya magoli 9 akiwa ndiye kinara huku John Bocco akiwa amefunga magoli 8. Hii inaonesha kuwa safu ya ushambuliaji ya Simba huibeba timu hata kipindi kigumu tofauti na safu ya ushambuliaji ya Yanga.

Mshambuliaji mwenye magoli mengi katika timu ya Yanga ni Yacoub Sogne mwenye magoli 4 akiwa sambamba na Michael Sarpong mwenye magoli 4 pia.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga haifanyi jitihada kubwa kipindi ambacho timu inahitaji msaada wa magoli. Washambuliaji wake ni butu tofauti na washambuliaji wa timu pinzani ambayo ni Simba.

Safu ya ushambuliaji ni silaha kubwa katika harakati za ubingwa. Safu ya kiungo ya Yanga inajitahidi sana kufunga magoli mfano Deus Kaseke ana magoli 6 mpaka sasa hivi.

Vivyo hivyo safu ya ulinzi ya Yanga inahusika sana katika ufungaji wa magoli, mfano mpaka sasa hivi Lamine Moro ana magoli 4 akiwa amelingana na washambuliaji wa Yanga.

Swali kubwa linakuja Yanga itachukua ubingwa na safu ya ushambuliaji ya kina Ditram Nchimbi na Michael Sarpong? Safu ambayo inaonekana butu kipindi ambacho timu inahitaji ushindi ?

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
JO

Amsha amsha ya wageni kuwazindua wazawa?

SIMBA SC

Ubora wa Miraji unafichwa kwenye udhaifu wa Chikwende