in

Fainali ya UEFA bila washambuliaji

Manchester City vs Chelsea Champions League final

MFUNGAJI bora wa Manchester City katika Ligi Kuu England msimu huu ni Ilkay Gündogan akiwa ametupia wavuni jumla ya mabao 13. Jorginho ni kinara wa mabao kwa upande wa Chelsea akiwa ametumbukiza wavuni mabao saba, akifuatiwa na Tammy Abraham, Mason Mount na Timo Werner ambao kila mmoja amepachika mabao 6. Naam, timu hizo zinatarajiwa kukutana katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa mwishoni mwa wiki hii.

Hizo ni miongoni mwa timu ambazo zimekuwa zikifanya matanuzi makubwa katika manunuzi ya wachezaji, zikiwa zinalenga kusajili washambuliaji wenye majina makubwa, na kuhakikisha wanacheza kitimu. Bila kujali kama wanapatia au wanakosea, lakini kwa kuwa umri wa Lionel Messi umekuwa mkubwa (ambaye amebaki kuwa mshambuliaji mahiri na mwenye thamani kubwa sokoni kutokana na kipaji binafsi lakini yeye ni zao la kucheza kitimu)- na Cristiano Ronaldo amekuwa mshindani wa karibu kariba ya Messi. Hata hivyo fainali ya UEFA inakosa mshambuliaji hatari ambaye anaweza kufunga mabao kila wakati na kuyaleta mambo kuwa mazuri kwa klabu hizo.

Tanzania Sports
Wachezaji wa Chelsea

Kwa miaka kadhaa sasa timu hizo zilishindwa kutamba katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na kujikita katika utawala wa Ligi ya ndani EPL. Hilo ndilo ni jambo ambalo limeipa timu hizo kucheza kwa kasi na kutawala mchezo lakini zinakosa mshambuliaji hatari pale mbele. Man City msimu wamejitahidi kupachika mabao kiasi, na Chelsea wanaonekana kutengeneza nafasi ya kuwa na mshambuliaji hatari kutokana na mbinu zao tofauti na washindani wao ambao hawana mtu wa aina hiyo.

Timu zote zina uwezo wa kutawala mchezo kadiri zinavyohitaji-, kwa msingi huo Thomas Tuchel amemwacha mbali mshindani wake Pep Guardiola kama mwalimu mahiri wa soka la kisasa la Kijerumani. Makocha wote wawili wapo makini kutengeneza viungo wakali katika vikosi vyao. Pia wote wawili wanaelekea kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa wiki hii bila mshambuliaji asilia.

Upo uwezekano  Kevin De Bruyne au Bernardo Silva wakaongoza safu ya ushambuliaji kwa upande wa Man City na Kai Havertz akawa ndio mshambuliaji kwa Chelsea.

Kinachoonekana hapo ni kuiga mfumo ulioletwa na AS Roma wakati ilipokuwa ikitumia mbinu za kumpanga Francesco Totti kama mshambuliaji wao, na Barcelona wanavyomtumia Lionel Messi na Manchester United walivyofanya kwa Cristinao Ronaldo (kabla hajawa mshambuliaji zaidi kwa miaka ya karibuni), wote hao wamekuwa nguzo ya safu ya ushambuliaji kwa nyakati tofauti.

Man City na Chelsea zote zinatumia viungo wao kama washambuliaji hivyo kucheza bila mshambuliaji kamili kutokana na sababu mbalimbali. Kuumia mara kwa mara kwa Sergio Aguero na kuporomoka kiwango cha Gabriel Jesus ilimaanisha Guardiola hakuwa na mchezaji wa kumtegemea katika safu ya ushambuliaji. Ndio maana alilazimika kuwatumia Ferran Torres ambaye hana uzoefu na akiwa amesajiliwa kwa nafasi ya winga, ni ujumbe rahisi kuwa Guardiola hakuwa na chaguo lingine.

Tanzania Sports
Aguero

Kwa upande wake Thomas Tuchel anaonekana hamzingatii Tammy Abraham kama mshambuliaji muhimu katika kikosi chake. Olivier Giroud ndiye mshambuliaji wa asili katika kikosi cha Chelsea, hata hivyo Tuchel hamtumii kwenye kikosi chake na daima amekuwa akiwekwa benchi kwa sababu anafikiria kuwa na mshambuliaji wa namna nyingine.

Akiwa kocha wa Mainz, aliwatumia Andre Schürrle na Shinji Okazaki kama washambuliaji, na alipokuwa Borussia Dortmund alimtumia zaidi Pierre-Emerick Aubameyang, wote walikuwa washambuliaji, lakini hakuna aliyeleta ufanisi uliotakiwa na kocha huyo kwa sababu walikuwa wakicheza kwa kurudi chini au kwenda pembeni zaidi.

Akiwa kocha wa Paris Saint-Germain, alikuwa na nyota wawili Neymar na Kylian Mbappe, alikuwa na uchaguzi mzuri wa kuamua namna ya kupanga safu yake ya ushambuliaji lakini ilikuwa dhaifu.

Timo Werner na Kai Havertz wamepangwa kucheza safu ya ushambuliaji, na pengine Werner ni mshambuliaji kamili hivyo huwezi kumchezesha kama Kai Havertz au Gundogun kwa Man City lakini anakosa ufanisi wa kupachika mabao.

Tanzania Sports
Pep Guardiola

Kama bahati yake ya kufunga mabao itarudi, basi Tuchel hana namna nyingine zaidi ya kumpanga Werner kwenye safu ya ushambuliaji, kwa sababu yeye anacheza kwa mtindo kama wa Aubameyang kwa kasi,wepesi na anapenda kushambulia akitokea pembeni kushoto kuingia eneo la hatari.

Havertz ni winga na kiungo wala si mshambuliaji, kwahiyo anapopangwa safu ya ushambuliaji anakuwa mshambuliaji feki au asiye wa asili. Kinachompa nafasi ni uwezo wake wa kuunganisha safu ya ushambuliaji na kiungo pamoja na nguvu za mwili.

Swali linalobaki sasa ni kwamba nani kati ya Gaurdiola na Tuchel atatumia mbinu ya mshambuliaji asiye wa asili, kwa kuzingatia namna wlaivyopanga timu zao kwa miezi kadhaa iliyopita. Pia uamuzi wa kutumia mshambuliaji asiye wa asili katika safu hiyo ni ishara kuwa makocha hao wanaweza kukabiliana na mazingira tofauti ya wapinzani waliopo mbele yao.

Kwamba, inawezekana wanabuni kitu hicho kwa njia isiyofaa, lakini wanategemea na hali halisi walizo nazo katila vikosi vyao. Mfano, Gaurdiola atachukua uamuzi gani pale anapohitaji mchezaji mwenye uwezo wa kucheza kiungo mshambuliaji mwenye jukumu la kuongoza safu ya ushambuliaji?  Kigezo anachotumia ni kumpanga mchezaji mwenye uwezo wa kumiliki mpira eneo la hatari pamoja na kutanua mbinu za mchezo husika. Anatakiwa kuwa tayari kupokea mabadiliko ya namna ya kushambuliaji kutoka kwa timu yake,kurudi chini kusaidia wengine na kuchangamsha timu kusaka mpira waliopoteza.

Tanzania Sports
Thomas Tuchel

Hivyo basi ni sababu tosha ya Guardiola kutumia mshambuliaji asiye wa asili akilenga ubora wa nafasi ya mbinu kuawala mchezo kuliko kutegemea mshambuliaji wa asili-kushambulia ba kufunga mabao. Pia kwake analenga kupiga pasi nyingi na kufungua nafasi kuanzia nyuma kwa golikipa wake kwenda kwa mabeki wenye jukumu la kupigania mipira ya juu hadi safu ya ushambuliaji kupiga mashuti.

Kabla ya kupata majeraha, Aguero alimudu kucheza kwa mbinu za Guardiola, lakini kwenye mchezo dhidi ya Real Madrid msimu uliopita, Gabriel Jesus alipangwa kikosini akicheza upande wa kushoto pamoja na Phil Foden aliyekuwa na jukumu la kuongoza safu ya ushambuliaji akitokea eneo la kiungo.

Mchango wa Gabriel Jesus ulileta mabao mawili katika mchezo huo, kisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alionekana kuwa tayari mchezaji wa mbinu za Guardiola kwenye safu ya ushambuliaji. Hata hivyo ukame umetawala kwa nyota huyo, mabao yameadimika na kiwango chake kimeonekana kushuka kwa msimu huu.

Harry Kane, amehusishwa kujiunga na Man City ambapo wiki mbili zilizopita alitanga mpango wake wa kuhama Tottenham Hotspurs, anaweza kuongoza safu ya ushambuliaji huku akirudi chini kusaidia viungo wake na kutekeleza majukumu ya mshambuliaji kiongozi, huenda akamudu mfumo wa Guardiola.

Je, ni nini anachotaka Tuchel kwenye timu yake? licha ya muda mfupi aliokaa na timu hiyo, lakini mfumo wa 3-4-2-1 amaotumia unahitaji kuwa mshambuliaji kiongozi kutegeneza nafasi kwa wachezaji wanaokimbia kuelekea lango la adui wakitokea nyuma, ambako Werner anacheza kwa amani.

Je, mabadiliko ya kimfumo hadi kumtumia mshambuliaji asiye wa asili yanalenga kitu gani? Ifahamike kuwa mchezaji wa aina hiyo hachezi kwa sababu ya nafasi hiyo kuwepo bali ni kwa aajili ya kuopachika mabao akitokea pembeni na chini, limekuwa jambo la kawaida kwa timu mbalimbali na kucheza kitimu zaidi kuliko kuwa na mshambuliaji mwenye jina kubwa ambaye anatakiwa kuchezeshwa yeye.

Mbali ya majukumu ya kufunga wanatarajiwa kuunganisha timu. Kama mambo yakienda vizuri wanaweza kupachika mabao 25 kwa msimu mmoja, hilo linakuwa matunda ya mipango, kamambavyo Man City wamekuwa wakifanya msimu mzima huku kwenye safu ya ulinzi wakiwa na Ruben Dias ambaye si kwamba anatimiza matakwa ya mfumo wa Guardiola pekee kwa nafasi hiyo, lakini anaweza kuwa mlinzi kwa asili yaani nje ya mbinu za Gaurdiola anazotumia kuchezesha mfumo wake.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Loftus Road Stadium

EPL washabiki kurudi

Unai Emery

FAINALI EUROPA