in , ,

MZOZO WA MLUNGULA FIFA

Chuck Blazer afungiwa maisha

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limemfungia mmoja wa viongozi wake wa zamani, Chuck Blazer kujihusisha na soka katika maisha yake yote.

Blazer (70) ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Fifa na katibu mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka la Amerika na Caribbean ameadhibiwa kwa sababu ya kufanya makosa kadhaa ya utovu wa nidhamu.

Mmarekani huyu anadaiwa alikuwa akifanya kazi kwa siri na Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) kwa kuwapa siri za Fifa na masuala yanayohusiana na rushwa, na mwenyewe amekiri kuhusika na rushwa, utakatishaji wa fedha na ukwepaji kodi.

Blazer amepata kusema kwamba viongozi wa Fifa walikubaliana kimsingi kuhusiana na kuchagua Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2010. Anasema pia kwamba alikuwa mwezeshaji kwenye suala kama hili 1998. Alikuwa ofisa wa pili wa ngazi ya juu zaidi katika Concacaf kati ya 1990 na 2011 na alikuwa kwenye Kamati Kuu ya Fifa tangu 1997 na 2013.

Waraka wa makubaliano yake na maofisa wa Marekani kwa ajili ya kuwafanyia kazi kwa siri uliwekwa wazi kwa amri ya mahakama ya Marekani. Alifanya mikutano mingi na maofisa wa Fifa huku FBI wakiwa wamemwekea chombo cha kupeleka kwao mazungumzo yao moja kwa moja.

Fifa imechukua hatua dhidi ya Blazer ikiwa ni siku chache tu baada ya kumwadhibu kwa kumpiga marufuku ofisa wake mwandamizi, Harold Mayne-Nicholls kushiriki shughuli za soka kwa miaka saba.
Mayne-Nicholls (54) aliyehusika na tathmini ya maombi ya kandarasi za kuandaa fainali za michuano ya Kombe la Dunia 2018 na 2022 amewajibishwa na Kamati ya Maadili ya Fifa.

Kiongozi huyo, hata hivyo, amepanga kukata rufaa kupinga uamuzi huo na amehoji kulikoni Fifa watangaze hatua hiyo kabla ya yeye kukamilisha mchakato wa rufaa ambao kamati imesema ni haki yake.
Mayne-Nicholls amepata kuwa Rais wa Chama cha Soka cha Chile na ni mmoja wa maofisa watano waandamizi ambao Fifa ilisema mwaka jana kwamba walikuwa wakichunguzwa.

Kiongozi huyu anakiri kuzungumza na maofisa Qatar waliokuwa wakihusika na uwasilishaji wa maombi ya nchi hiyo kupewa uenyeji. Anasema mazungumzo yao yalikuwa juu ya uwezekano wa nchi hiyo kuwapa kazi jamaa zake watatu.

Kamati ya Nidhamu ya Fifa inasema kwamba inaona majadiliano hayo yanaleta shaka tosha juu ya uadilifu uliokuwapo katika mchakato wa kukagua maombi na katika tathmini ya jumla. Fifa ilikuwa imesitisha uchunguzi dhidi ya Blazer kwa sababu za afya mbaya lakini ilianza tena Desemba mwaka jana.

Fifa imesema kwamba uamuzi wa kumfungia moja kwa moja Blazer umetokana na matokeo ya uchunguzi ulioendeshwa na kitengo chake cha uchunguzi pamoja na mapendekezo ya kamati ya nidhamu. Kadhalika umechangiwa na ripoti ya mwisho juu ya uadilifu iliyotolewa na Concacaf pamoja na taarifa zilizopatikana kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Marekani.

Viongozi waandamizi wa Fifa wanahusishwa na mlungula katika michakato ya kupata nchi wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia, ikiwa ni pamoja na ile ya 2018 na 2022 iliyopangwa kufanyika nchini Urusi na Qatar katika mtiririko huo.

Tayari maofisa saba wa ngazi za juu wa Fifa wamekamatwa na wanashikiliwa nchini Uswisi, wakisubiri uamuzi wa maombi ya Marekani kuwapeleka huko kujibu mashitaka ya rushwa, wizi na utakatishaji wa fedha. Wengine saba wamenaswa nje ya Fifa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Robin van Persie kwenda Fenerbahce

SIKU YA PSPF YAFANA SABASABA