in , , ,

Mwaka 2013, haukuwa mzuri kimichezo Tanzania..

Mwaka 2013 unaomalizika muda mfupi ujao, umeshuhudia Tanzania ikipata wastani wa kawaida katika michezo ambao haunatofauti sana na miaka ya hivi karibuni kwenye michuano yote, yakirafiki na ile ya ushindani ambayo imehusisha timu yetu ya Taifa na klabu hatukuwa na kikubwa cha kujivunia.

Kulikuwa na mambo ambayo hayakutarajiwa, kama kushuhudia timu toka nyanda za juu kusini “Mbeya city council football club” ikijikita kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubingwa wa ligi ingawa, majina makubwa ya timu za Azam, Simba na Yanga yanaendelea kupewa nafasi ya kuchakuwa ubingwa huo.

Mwaka 2013 pia umeshuhudia kuibuka kwa wachezaji wengi vijana, wenye vipaji ambapo, ujuzi wao umefanya ligi iweze kuvutia na kuwa yenye ushindani mkubwa.

Mwaka 2013 haukushuhudia matukio mengi ya utovu kama vile, mashabiki kuvamia uwanja au kufanya uharibifu wa viwanja na kuharibu miundombinu, na mali za wamiliki wa viwanja.

Hali kama hii imeweza kuvutia mamlaka za soka na wachambuzi wengi kuweza kuchangia uboreshaji wa soka na kuongeza pato kwa wachezaji na mafao mengine. Kumekuwa na maboresho toka kwa wadhamini wa vilabu na hii yote ni matokeo ya mpango mkakati wa masoko kuanzia ngazi za vilabu na hata kwenye shirikisho la soka Tanzania (TFF).

Mwaka 2013 pia umeshuhudia kutofanya vizuri kwa timu zetu ngazi ya vilabu, timu za mikoa,Taifa Stars na hata kwenye mashindano ya kimataifa.

Klabu za Simba na Azam, ziliwakilisha nchi kwenye michuano ya shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kwenye ngazi ya vilabu lakini kwa masikitiko makubwa, hawakuweza kuvuka hata hatua ya makundi.

Taifa Stars haikuweza kufanya kile watanzania walichotarajia, walishindwa kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika ambazo zilifanyika nchini Afrika Kusini na michuano ya Kombe la Dunia ambayo inatarajiwa kufanyika nchini Brazil mwaka 2014.

Mwaka unaomalizika usiku wa leo,umeshuhudia mabadiliko ya uongozi pale TFF, Kamati ya Olimpiki, Chama cha Riadha Tanzania, Chama cha Netiboli Tanzania, Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) na Shirikisho la Tenis Tanzania.

Viongozi wapya ndani ya mashirikisho hayo ya kitaifa, waliahidi mabadiliko makubwa na maboresho lakini, uthibitisho wa ahadi zao katika utendaji bado ni ndoto! Kiukweli, viongozi wa TFF na BFT wamekuwa madarakani kwa muda usiozidi miezi 3, itakuwa sio uungwana kutegemea mambo makubwa toka kwao kwa muda mfupi waliokaa madarakani.

Tutashukuru endapo nguvu mpya iliyoingia madarakani itakuja na njia mahususi za kutatua matatizo, huku wakiwa na lengo la kuendeleza, kuitangaza na kuitafutia soko michezo husika ili kuongeza hamasa, watu wengi waweze kujihusisha na michezo.

Vyama vya michezo ni lazima vionyeshe uwezo mkubwa katika kuongoza michezo, wakianza na kuifanya iwe na mtazamo wa kibiashara. Itakuwa ni jambo la kusikitisha endapo tutafika mwisho wa mwaka 2014 huku viongozi wa vyama vya michezo husika wakishindwa kutamba kwenye michezo husika kwa kukosa fedha za uendeshaji.

Ushauri wetu kwao ni kuona viongozi wanakuja na mbinu mbadala zinazoweza kusaidia na kuinua ubora wa shughuri zote za michezo.

Viongozi wanaweza pia kujifunza kutoka kwenye klabu kubwa ambazo zimepitia changamoto nyingi lakini, zikaweza kujitutumua na kupata matokeo mazuri nje na ndani ya uwanja. Shukrani za dhati kabisa ziende kwa wadhamini kwa mchango wao mkubwa walioutoa, wamefanya kazi nzuri. Wote waliofanikisha, tunawashukuru pia na wote wanaoweza kusaidia wanaweza kufanya hivyo, kwa kujali uzalendo zaidi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Manchester City juu

EPL……….01-01-2014