in , , ,

MUHAMMAD ALI:

Usiyoyajua juu yake

Dunia imempoteza bondia mashuhuri zaidi katika historia ya mchezo huo
duniani, Muhammad Ali.

Ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 74 baada ya kusumbuliwa kwa muda
mrefu na maradhi, na inaelezwa kwamba ugonjwa uliomwondoa duniani ni
matatizo ya kupumua, lakini pia alikuwa na ugonjwa wa Parkinson.

Hakuzaliwa akiitwa Muhammad Ali, bali alikuwa na jina la Cassius Clay,
Jr; mtoto wa Cassius, lakini akaamua kubadili jina na dini yake 1964,
muda mfupi tu tangu alipotwaa mkanda wa uzani wa juu zaidi duniani.

Mkongwe na shujaa huyu aliyejulikana na wengi kwa miaka mingi,
atasahauliwa na wachache sana, akiwa amepata kutwaa mkanda huo wa
uzani wa juu mara tatu. Alibadili jina hilo baada ya kuvutiwa na
Vuguvugu la Waislamu Weusi na alipewa jina hilo na Elijah Muhammad.

Kabla ya kuwa Muhammad Ali, alipita hatua nyingine, akajiita Cassius
X, pengine kwa jinsi alivyokuwa amesisimkwa na vuguvugu lililoongozwa
na akina Malcolm X. ALipata taji lake la kwanza la uzani wa juu
Februari 26, 1964 na Machi 6 mwaka huo huo akatangaza jina lake jipya
alilopewa na Elijah Muhammad (aliyeongoza Nation of Islam tangu 1934
hadi kifo chake 1975). Hata hivyo, Malcolm X aliondoka kwenye kundi
hilo baada ya Ali kujiunga na akauawa mwaka uliofuata.

Ali alikataa kujiunga na Jeshi la Marekani Aprili 28, 1967 akijitetea
kwamba hawezi kwenda vita ya Vietnam wakati husali swala tano kila
siku kwa ajili ya amani. Anasema yeye ni Mwislamu wa madhehebu ya
Sufi, wanaoamini kwamba kuumiza mtu yeyote kwa makusudi ni kuumiza
utu, kila mtu na kuiharibu dunia.

CkFaJf8XAAAYhX5
Kutokana na kukataa huko, Ali alivuliwa mkanda wake wa uzani wa juu na
kupigwa marufuku ya kushiriki mchezo huo kwa miaka minne. Ali
alikwenda uhamishoni kwa miaka mitatu na miezi saba.

Aliporejea alikuwa ajiandae kwa pambano kali dhidi ya aliyekuwa namba
moja – Jerry Quarry. Alifanikiwa kumtwanga kwa TKO, lakini ukweli ni
kwamba alikuwa na wiki sita tu za kujiandaa, ambapo kwenye mazoezi,
rafiki yake wa zamani na bondia, Jimmy Ellis alimvunja mbavu moja,
lakini Ali akaamua kusonga mbele, akijiaminisha angemimina masumbwi
mazito mapema na kumtoa kwa KO, kabla hajaguswa mbavuni, na ikawa
hivyo.

M
Bondia huyu amekuwa na ugonjwa wa Parkinson kwa zaidi ya miongo mitatu
sasa, ambapo amekuwa akitetemeka na hili lilimfanya ajifunze mbinu
mpya za mawasiliano. Alikutwa na ugonjwa huo mwaka 1984 akiwa na umri
wa miaka 42, ikabidi ajifunze kuwasiliana kwa kutumia mikono, vidole
na pia kuonesha kwa uso na macho yake.

Kwa Waafrika, akiwa na rangi kama yao, watakumbuka sana pambano
alilocheza jijini Kinshasa, Zaire, Oktoba 29, 1974, ambalo ni maarufu
kwa jina la ‘The Rumble in the Jungle’. Pambano hilo lilianza usiku wa
saa nne, baina yake na aliyekuwa bingwa wa dunia, George Foreman.

Pambano hilo lilihudhuriwa na washabiki takriban 60,000 kwenye uwanja
uliopewa jina la ‘The 20th May Stadium’, ambapo Ali alishinda kwa KO,
akimtupa chini Foreman kabla ya kumalizika kwa raundi ya nane.
Liliitwa pambano kubwa zaidi katika karne ya 20.

Lilikuwa moja ya kazi za kwanza za promota Don King pamoja na
mfanyabiashara wa muziki, Jerry Masucci aliyewapeleka wanamuziki wake
maarufu, Fania All Stars kutumbuiza. Ali na Foreman walisaini mikataba
tofauti, wakisema wangepigana iwapo angekuwa na kitita cha dolamilioni
tano.

Dikteta wa zamani wa Zaire, hayati Mobutu Sese Seko ndiye aliomba
pambano hilo lifanyike nchini mwake, kama njia ya kujiongezea umaarufu
kisiasa, ambapo King alifanikiwa kuiita kampuni ya Panama iliyoitwa
Risnelia Investment, ya Uingereza iliyoitwa Hemdale Film Corporation,
kwa ajili ya udhamini, akatengeneza fedha nyingi; za kuwalipa
mabondia, huduma nyingine na za faida yake.

Pambano hilo lilirushwa na Closed Circuit Television kwenye kumbi za
starehe nchini Marekani lakini pia kupitia Over the Air Television
kote duniani.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na Watanzania London

Tanzania Sports

TETESI ZA USAJILI