in , , ,

Mourinho, Wenger wakunwa na wachezaji

*Ni kipa Courtois, mshambuliaji Cambell
*Wanang’ara walikopelekwa kwa mkopo
*Vermaelen kwenda Man U yakanushwa

Makocha Jose Mourinho wa Chelsea na Arsene Wenger wa Arsenal wamevutiwa na kiwango cha wachezaji wao walio nje kwa mkopo.
Kutokana na mwenendo wao huo, makocha hao wameahidi kuwarejesha kundini kipa Thibaut Courtois (Chelsea) na Joe Campbell (Arsenal).

Courtois anachezea Atletico Madrid na aliwasaidia hadi wakatwaa ubingwa wa Hispania msimu uliomalizika majuzi na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hivi sasa Kocha Mourinho amesema ni wakati mwafaka kwa kipa huyo chipukizi kurudi Stamford Bridge. Zipo tetesi kwamba Petr Cech anatakiwa na klabu kadhaa.

“Baada tu ya michuano ya Kombe la Dunia, atarudi moja kwa moja Stamford Bridge, mwisho wa habari,” akasema Mourinho juu ya Courtois (22) anayedakia Timu ya Taifa ya Ubelgiji.

Kipa huyu hajapata kuwachezea Chelsea katika mechi za ushindani tangu walipomsajili kutoka Genk ya Ubelgiji 2011 kwani alitolewa kwa mkopo Atletico tangu wakati huo.

Hata hivyo, Courtois alipoulizwa iwapo atafurahi kurudi Chelsea, alisema anataka apewe uhakika atakuwa kipa namba moja. Alicheza dhidi ya Chelsea kwenye nusu fainali ya UCL na kuwazuia vilivyo na Atletico wakashinda.

“Mtauliza iwapo nataka kuwa kipa chaguo la kwanza kokote nitakakocheza msimu ujao. Ni kweli, nadhani kwa umri wangu na uwezo nilioonesha, nataka kuwa namba moja, kukaa benchi si kitu kizuri sana,” akaonya kipa huyo.

Kwa upande wa Campbell, kocha Wenger alisema kwamba hatamtoa tena moja kwa moja mshambuliaji huyo kwa mkopo bali watakuwa naye kwenye mazoezi na ziara za kabla ya kuanza msimu mpya.

Campbell alionesha kandanda safi Olympiakos katika ligi na UCL pia, ambapo aliwahangaisha mabeki wa Manchester United.

Kadhalika sasa anatamba na Timu ya Taifa ya Costa Rica kwenye Kombe la Dunia na ameifungia bao dhidi ya vigogo Uruguay, na Costa Rica kuibuka na ushindi kwenye mechi ya kwanza.

TETESI ZA VERMAELEN KWENDA MAN U
20140416-145957.jpg

Katika hatua nyingine, zimekuwa zikisambaa tetesi kwamba Nahodha wa Arsenal, Thomas Vermaelen anahamia Manchester United.

Ilidaiwa kwamba kimsingi amekubali kuhamia katika timu itakayofundishwa na Louis van Gaal na kwamba wakala wa Robin van Persie ndiye wakala wa Vermaelen pia na ndiye aliyewezesha hilo.

Hata hivyo, wakala huyo amekanusha kufanyika mazungumzo yoyote kwa mchezaji huyo kuhamia Old Trafford.

Man U wanatafuta mabeki wa kati kutokana na kuondoka kwa nahodha wao, Nemanja Vidic na mkongwe Rio Ferdinand.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Simba: Uchaguzi uko pale pale!

Ureno hoi kwa Ujerumani