in , , ,

Mourinho: Ilikuwa niwe kocha wa England

*Aibeza na kudai ni ya wazee

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho anadai alikaribia kuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya England.

Mourinho anasema alipata fursa hiyo 2007 alipoondoka Stamford Bridge na kwamba Desemba mwaka huo nusura achukue kazi hiyo.

Anasema iwapo angeanza kazi hiyo angefanya kazi kwa karibu na wachezaji wake wengi wa zamani wa Chelsea waliokuwa tayari kwenye timu hiyo.

‘The Special One’ anasema kikwazo kimoja tu kwa kazi hiyo kilikuwa mkewe ambaye alimshauri akatae ofa hiyo, naye akaridhia maoni yake.

“Akina Lampard, Terry, Joe Cole, kila mtu alikuwa ananiambia; ‘njoo, njoo, njoo’. Vijana wa Manchester United na Liverpool nao walikuwa wakiwaita wachezaji wangu hao na kuwaambia; ‘mwambieni bosi wenu aje’ … kwa kweli wengi walinitaka nifundishe Three Lions,” anasema Mourinho.

Anaongeza: “Mke wangu aliniambia kwamba nisikubali kazi hiyo kwa sababu sikuwa mtu sahihi … na kweli ulikuwa uamuzi sahihi. Tunazungumzia kitu cha miaka saba iliyopita.
“Kwa kweli nisingeweza kusubiri miaka miwili mizima bila mashindano makubwa wala mie si mtu wa kutumia miaka miwili yote kucheza na timu kama Kazakhstan na San Marino,” anasema Mourinho akimaanisha timu ya taifa haichezi mara kwa mara.

Mourinho anadai kwamba kazi ya ukocha wa timu ya taifa ni ya wazee, kwa sababu hakuna kitu kikubwa cha kufanya zaidi ya kusafiri na kutazama wachezaji wakifanya mazoezi na kucheza na kushauri kisha kupumzika muda mrefu.

Kazi hiyo sasa inafanywa na kocha mkongwe Roy Hodgson ambaye aliteuliwa bila kutarajiwa kwani aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ni Mwingereza mwingine, Harry Redknapp ambaye sasa anafundisha Queen Park Rangers (QPR) baada ya kufukuzwa Tottenham Hotspur. Kazi hiyo ilichukuliwa kwanza na Fabio Capello kisha alipojiuzulu ndipo Hodgson akaipewa.

“Kazi hii haingenifaa miaka saba iliyopita wala kwa sasa na wala sidhani kwamba itakuwa kazi mwafaka kwangu miaka saba ijayo. Labda miaka 15 kutoka sasa,” anazidi kuikandia kazi hiyo Mourinho.
Iwapo Mourinho angekuwa kocha wa England kuna uwezekano John Terry hangepokonywa unahodha baada ya kashfa ya kutoa lugha ya kibaguzi kwa Anthony Ferdinand wa QPR.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Blatter: Harufu ya ubaguzi Qatar

Wilshere: Pirlo haendi popote