in , , ,

Mourinho awapiga mkwara Man United

*Chelsea, Spurs watamba ligi ya Europa

*Liverpool kilio ugenini, Newcastle sare

 

Wakati Manchester United wanachekelea sare dhidi ya Real Madrid nchini Hispania, Jose Mourinho anasema Old Trafford ni mahali pazuri pa kufunga mabao.

United walipata sare ya bao 1-1 katikati ya wiki, baada ya Cristiano Ronaldo kusawazisha bao lililoshangiliwa sana la Danny Wellbeck, yote yakiwa ya kichwa.

Mourinho anayetarajiwa kurejea kufundisha soka England msimu ujao kutokana na Bernabeu kumchoka, anasema Man U hawana cha kufurahia, maana magoli ni nje nje, na wanarudiana Machi 5.

Mourinho alikuwa akidhaniwa angemrithi Alex Ferguson Old Trafford, lakini amekanusha, akisema anatarajia Fergie aendelee na kazi miaka mingi.

Chelsea ndiyo klabu isiyokuwa na kocha wa kudumu hadi sasa, alipata kufundisha hapo na pia Manchester City wanaelekea kuachwa mbali na United, hivyo huenda wakaamua kubadili kocha.

Katika mechi nyingine iliyofuatiliwa sana Uingereza, ambayo ilichezwa Uskochi, mabingwa wa huko, Celtic hawakuamini waliponyukwa mabao 3-0 na Juventus.

Celtic walishaanza kujiamini tangu walipowafunga Barcelona kwenye mechi za kufuzu, na sasa wanahitaji muujiza kwenda kulipa kisasi hicho na zaidi nyumbani kwao Torino, Italia.

Katika mechi nyingine, Zlatan Ibrahimovic wa Paris Saint-Germain alitolewa kwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya, wakati timu yake ikiishinda Valencia ya Hispania kwa mabao 2-1.

Hii ni kadi ya tatu kwa raia huyo wa Sweden katika mashindano ya Kombe la Mabingwa Ulaya, akiwa na timu tatu tofauti, japokuwa safari hii haikuonekana kama faulo ilikuwa kubwa.

Mechi zidi za raundi hiyo ya 16 bora zinaendelea katikati ya wiki kwa Arsenal kuwakaribisha Bayern Munich kutoka Ujerumani na Malaga wa Hispania kwenda Ureno kuwavaa Porto.

AC Milan wa Italia watawakaribisha Barcelona kutoka Hispania wakati Wajerumani wengine, Schalke wanaalikwa Urusi kukipiga na Galatasaray. Katika mechi za Ligi ya Europa inayoshirikisha timu 32 kwa mtoano, Chelsea walijifuta machozi kwa kuwachapa Sparta Prague bao 1-0 nchini Czech.

Hata hivyo, mechi hiyo haikuwa na msisimko, na Cheslea walilazimika kusubiri hadi dakika nane kabla ya mpira kumalizika, Oscar aliyeingia dakika hiyo hiyo akafunga bao muhimu la ugenini.

Mechi ya marudiano itafanyika Stamford Bridge, lakini hakuna uhakika wa ushindi, kwa sababu uwiano unaonesha kwamba Chelsea wamepoteza au kutoa sare mechi nyingi zaidi kuliko kushinda nyumbani.

Jijini London, msisimko ulikuwa mkubwa kwa washabiki wa Tottenham Hotspurs, kutokana na magoli mawili mazuri ya mpira wa adhabu yaliyofungwa na Gareth Bale dhidi ya Lyon wa Ufaransa.

Spurs walishakata tamaa ya ushindi kutokana na goli la mwishoni mwa kipindi cha kwanza kusawazishwa na kiki kali ya aina yake ya Samuel Umtiti.

Hata hivyo, alikuwa Bale tena, aliyepata nafasi ya kupiga mpira wa moja kwa moja wa adhabu ndogo, akautenga kama alivyofanya mwanzo, na adui hawakuambulia hata kuugusa.

Kwingineko kaskazini mashariki mwa nchi, Newcastle walishindwa kutumia faida ya kuwa nyumbani kwa kwenda suluhu na Metalist Kharkiv kutoka Ukraine.

Vijana hao wa Alan Pardew walionekana kutokuwa na bahati, kwani walikuwa na kosa kosa nyingi na mabao yao mawili yalikataliwa kwa madai ya wafungaji kuotea.

Watakuwa na kazi ya kuwazamisha wapinzani wao hao nyumbani kwao Kharkiv ili waingie awamu ya 16 bora.

Liverpool nao waliangukia pua baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 ugenini kutoka kwa Zenit St Petersburg.

Brendan Rodgers atasikitishwa na vijana wake walivyotumia hovyo nafasi walizopata, akiwamo mpachika mabao wao, Luis Suarez aliyekosa hata akiwa tadi tano na goli akapiga nje.

Hata hivyo, Rodgers alidai kwamba wana kila sababu ya kushinda kwenye marudiano Anfield, mtaji wao ukiwa ni washabiki.

Katika mechi nyingine Viktoria Plzen waliwafunga Napoli 3-0.

Anzhi Makhachkala waliwafunga Hannover 3-1;

Levante wakawafunga Olympiacos 3-0 huku Dynamo Kiev wakienda sare ya 1-1 na Bordeaux.

Ajax waliwatungua Steaua Bucharest 2-0; Fenerbahce wakaenda suluhu na BATE Borisov  wakati Lazio walienda sare ya 3-3 na Borussia Monchengladbach.

Mabingwa watetezi, Atletico Madrid waliachwa hoi kwa kipondo cha mabao 2-0 kutoka kwa klabu ya Kirusi ya Rubin Kazan.

Dnipro walipoteza mechi nyumbani mikononi mwa Basle kwa kufungwa mabao 2-0 wakati Inter Milan waliwadhibiti Cluj kwa kuwakandamiza mabao 2-0.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Malinzi aongea juu ya kuenguliwa katika orodha ya wagombea wa TFF

WATU WA SOKA KWENDA MAHAKAMANI HAKUEPUKIKI TANZANIA