in , , ,

Mourinho aibukia Arsenal

Kazi ni msingi wa maisha na maendeleo huletwa na kazi, alisema Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Kocha Jose Mourinho anafikiria kufanya mchakato wa kuchukua nafasi ya
Arsene Wenger klabuni Arsenal. Mreno huyo ambaye pia anapewa nafasi
kubwa ya kumrithi Lous van Gaal wa Manchester United ameonywa na
washauri wake kutojifunga Old Trafford wakati hatima ya Wenger hapo
London Kaskazini haijulikani, ikizingatiwa amebakisha msimu mmoja tu
kwenye mkataba wake.

Wenger anaonekana kuzidi kukerwa na chagizo dhidi yake, hasa kutokana
na kupoteza uongozi wa ligi, kuendelea kufungwa na sasa ndoto ya
kutwaa ubingwa kuzidi kufifia kutokana na kuachwa mbali na Leicester
na Tottenham Hotspur.

Baadhi ya washabiki wameanza kampeni ya kutaka Wenger (66) aondoke,
lakini kigingi kwao kinaonekana kuwa ni mmiliki Mmarekani, Stan
Kroenke mwenye imani kubwa na kocha huyo Mfaransa, hivyo kwamba huenda
akamwongeza mkataba hata asipotwaa taji lolote.

Washabiki na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya soka wanaona kwamba
Wenger amekuwa mhafidhina mno; hana jipya Emirates na sasa angetakiwa
mwanamageuzi atakayebadili mambo hapo na kuwapa ubingwa, na Mourinho
ndiye anayetajwa kufaa hapo.

Wachezaji wanaojiunga Arsenal wanadaiwa kutofurahishwa na mbinu za
Wenger katika kuwakabili wapinzani, lakini pia kushindwa kuwalinda
kisaikolojia wachezaji wake hao hivyo kwamba miaka nenda rudi wamekosa
ubingwa, wakapozwa na makombe mawili ya FA misimu miwili iliyopita
lakini sasa wameshatupwa nje.

Kana kwamba hiyo haitoshi, waliondoshwa kwenye michuano ya Kombe la
Ligi na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa aibu, walipotandikwa na Barcelona
kwa jumla ya mabao 5-1, ikiwa ni pamoja na kukubali kufungwa nyumbani
Emirates.

Mourinho amepata mawasiliano kutoka kwa mtu aliyesema anawawakilisha
Arsenal, akimtaka ajiandae kwa lolote hasa baada ya Arsenal kufungwa
na timu zisizo na nguvu kama wao -Manchester United na Swansea City.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea aliulizwa iwapo angependa kufanya kazi
Arsenal ikiwa Wenger atajiuzulu au kufutwa kazi, kisha akatakiwa
asijifunge na mkataba kwingine hadi Mei itakapojulikana hatima ya
Mfaransa huyo.

Mourinho (53) aliye huru tangu afukuzwe kazi na Roman Abramovich ikiwa
ni pungufu ya nusu msimu tangu awape Chelsea ubingwa wa Ulaya,
Mourinho anatajwa kuhitajika kwenye klabu mbalimbali kama AS Roma na
Internazionale za Italia pamoja na Manchester United wanaoonekana
kutofutahia mwenendo wa Van Gaal, japokuwa mkataba wake bado
haujamalizika.

Inadaiwa kwamba Mouriunho alisaini makubaliano ya awali ya kujiunga
Man U lakini mkataba kamili utafuata baadaye Mei na kwamba Man U
wanaweza kutomwajiri lakini itabidi wamlipe fidia ya pauni milioni 15.
Anadaiwa kusema kwamba Arsenal wana kikosi kizuri kinachoweza kutwaa
ubingwa na nwanahitaji nyongeza ya wachezaji wawili au watatu tu.

Katika kikosi cha sasa, wamo ambao Mourinho amepata kutwaa nao ubingwa
Chelsea na Real Madrid, Petr Cech na Mesut Ozil mtawalia. Arsenal
wanaelekea watafuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya, kitu ambacho Mourinho
angependa kufanya ili atambe Ulaya.

Kuingia kwake Arsenal kunaweza kumpa faraja na familia pia kwa sababu
watabaki kwenye nyumba yao iliyo London, badala ya kuanza kuhama tena
kwenda Manchester au ng’ambo ya nchi. Atafurahia kazi Arsenal kwa
sababu atakuwa na uamuzi wa mwisho juu ya nani asajili na mambo
mengine, tofauti na Chelsea na Real Madrid alikodhibitiwa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

SABABU ZINAZOLINDA KIBARUA CHA VAN GAAL

Tanzania Sports

Ngoma aipania Al Ahly