in

Morrison amejimaliza mwenyewe..

Benard Morrison

Nyota wa Yanga Benard Morrison alipofanyiwa ‘sub’ alitoka katoka nje kabisa ya uwanja kama alivyowahi kufanya Balotelli.

Morrison  huyo aligoma kuongea kwa kingereza au Kiswahili ambazo ndio lugha zinazotumika sana Tanzania, bali alitumia lugha yao kutoka Ghana wakati anaondoka nje kabisa ya uwanja.

Kitendo cha utovu wa nidhamu cha Morrison kinaweza kuharibu morali ya wachezaji wa Yanga kama hawaja itafutia dawa yake mapema.

Kwa namna hii anayofanya inaweza ikamharibia hata huko anapotaka kwenda kwani hakuna timu inayopenda mchezaji asiyekuwa na nidhamu.

Kama ataenda Simba au klabu nyingine yoyote sidhani kama watafurahishwa na hiki anacho kifanya hivi sasa na itaweza ikampotezea soko lake.

Haya mambo yalifanyika miaka mingi nyuma wakati watani wa jadi walipokuwa wanachukuliana wachezaji sio kipindi hiki chenye teknolojia.

Katika mchezo huu wa nusu fainali Yanga na Simba kocha wa Yanga alicheza vibaya karata zake.

Papy Tshishimbi, Benard Morrison na Haruna Niyonzima hawakucheza katika kiwango bora kabisa.

Morrison alikuwa mzigo kabisa kwani hakuonesha kama anahitaji kucheza,  hakuhitaji kabisa kujituma hii imepelekea atolewa naye akaona isiwe tabu.

Ila inaonekana alikuwa na dhamira yake ameipanga kabisa baada ya mchezo ule wasiwasi wangu hakuzoa simu za wachezaji wenzake maana sifa zake tulishaambiwa.

Mchezaji huyu anaonekana mkorofi tangu alipotoka, licha ya kipaji alichokuwa nacho.

Ndio maana nikajiuliza kwa kipaji chake na uwezo alionao kwanini aje kucheza ligi ya Tanzania? baada ya vituko vingi ambavyo nimeviona nikagundua kuwa nidhamu yake mbovu na haiwezi kumpelekea popote.

Pia naishangaa Yanga kama iliweza kufukuza wachezaji wote mwaka 1977 wanashindwaje kumlipua Morrison? kama anataka kuondoka waangalie katika mkataba wake hizo hela walizompa wakasajili mchezaji mwingine aje acheze mpira.

Ila Yanga wakiendelea kumlea hivi hivi basi italeta mpasuko ndani ya timu hiyo na watakosa msingi imara kwa mambo yao yanayoendelea.

Tumewahi kuona aina hii kwa nyota wa zamani wa Manchester City ya England  ‘Super’ Mario Balotelli naye aliwahi kutoka kabisa na kuelekea Italia kuangalia AC Milan dhidi ya Inter Milan baada ya kutolewa ‘Sub’.

Lakini matokeo yake tunayaona licha ya kipaji alicho nacho Balotellli bado anazidi kutokomea kusikojulikana.

Naye Morrison inawezekana kabisa kwa tabia yake hii akamaliza soka mapema sana na biashara ikaisha haraka mno.

Yaani jamaa alitoka nje kabisa na alionekana kutafuta gari nje aondoke zake Yanga kunani hapo kwenu, mbona  soka linachezewa hivi.

Kuondoka kwake kule inawezekana akaondoka mazima maana haeleweki kabisa.

Maswali sasa najiuliza je Yanga watafanya nini baada ya tukio hili ? watavunja mkataba au watampa nafasi nyingine ajisafishe na aendelee kuwavuruga wenzake.

Tusubiri muda utaongea wenyewe na kama hatua zitachukuliwa tutaziona.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

73 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply
  1. Hao Yanga ni mazuzu kulea uozo. Na nitadharau sana soka la bongo kama watamchukua Simba. Ni kajinga sana hako ka ngedere.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Bianca Williams

Mwanariadha alalamikia polisi kwa ubaguzi wa rangi

Jhai Dhillon

Kulikoni Waasia wachache EPL?