in

Mikel Arteta bado anadaiwa na Arsene Wenger

Mikel Arteta bado anadaiwa na Arsene Wenger

Natamani sana niisimulie Arsenal ya mwanzoni wa miaka ya 2000. Ile Arsenal ya mzee Arsene Wenger. Mzee ambaye alitumia mikono yake kujenga timu imara ambayo imeandikwa kwenye kitabu cha dhahabu kinachobeba kumbukumbu za mpira wa miguu.

Kipindi kile ndicho kilikuwa kipindi ambacho Sylvain Wiltord aliweza kufunga goli pekee kwenye uwanja wa Old Trafford, goli ambalo lilimwezesha Arsene Wenger kutangaza ubingwa wa ligi kuu ya England mbele ya Sir Alex Ferguson. 

Tanzania Sports
Moja kati ya kipindi kigumu kwa Arsenal

Arsene Wenger aliweza kuwavua ubingwa Manchester United kwenye uwanja wao ambao wanajivunia, tena kwa kuwafunga na kutangazwa rasmi kama mabingwa wa ligi kuu ya England mbele ya mashabiki wao  hii ilikuwa msimu as mwaka 2001/ 2002.

Arsene Wenger alizidisha ubabe wake, msimu wa mwaka 2003/2004 alifanikiwa kutangaza ubingwa wa ligi kuu ya England katika uwanja wa White Hart lane . Uwanja wa maadui wao wakubwa Tottenham Hotspurs. Ikawa ni mara ya kwanza kwa Arsenal kutangaza ubingwa wa ligi kuu ya England kwenye uwanja wa Tottenham Hotspurs tangu mwaka 1971.

Arsenal walihitaji alama moja tu kutangaza ubingwa, na Arsenal walitangulia kufunga magoli mawili kupitia kwa Patrick Viera na Robert Pires. Magoli ambayo yalisawazishwa na Jamie Redknap pamoja na Robbie Keane lakini mwisho wa siku Arsenal akatangazwa bingwa kwenye uwanja wa mahasimu wao.

Kuchukua ubingwa Old Trafford na White Hart lane yalikuwa matukio makubwa sana kwenye historia ya mzee Arsene Wenger. Matukio ambayo yalikuja kupambwa na neno “Invincible”. Kwenye msimu ambao Arsenal wanachukua ubingwa kwenye uwanja wa Tottenham Hotspurs ndiyo walifanikiwa kushinda ubingwa wa ligi kuu ya England bila kufungwa. 

Wakakabidhiwa kikombe cha dhahabu. Mikono yao ikawa imebaki na deni moja tu kubwa, deni la kuhakikisha mikono yao inashika kikombe cha ligi ya mabingwa barani Ulaya. Mwaka 2006 walifanikiwa kufika fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Kwa bahati mbaya hawakufanikiwa kubeba kombe hili mbele ya FC Barcelona baada ya kufungwa magoli 2-1. Kilikuwa kipindi kigumu cha maisha ya Arsene Wenger pale Arsenal, na inawezekana mechi hii ni moja ya mechi ambayo hawezi kuisahau katika maisha yake ya soka pale Arsenal.

Arsene Wenger kaondoka Arsenal huku moyo wake ukiwa na huzuni kwa kushindwa kubeba kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya. Inawezekana hiki kitu kinamuuma sana, hawezi kurudisha siku nyuma tena ili arekebishe makosa yake ya nyuma.

Muda huu yupo sebuleni mbele yake kuna luninga, luninga ambayo inamuonesha Mikel Arteta, mmoja wa manahodha wa Arsene Wenger kipindi ambacho anaifundisha Arsenal. Huyu ni mwanae, zao lake kabisa, na leo hii anamshuhudia akikaa kwenye kiti kile kile ambacho Arsene Wenger alikuwa anakitumia kukalia.

Kitu pekee ambacho Mikel Arteta anatakiwa kukifahamu ni deni kubwa ambalo analo kwa Arsene Wenger. Mikel Arteta anatakiwa kufahamu kuwa kipindi ambacho alikuwa mchezaji alishindwa kumsaidia Arsene Wenger kubeba ubingwa wa ligi ya mabingwa barani ulaya. 

Miguu ya Arteta hakuitumikishwa ipasavyo ili kumbeba Arsene Wenger, leo hii akili ya Mikel Arteta inahitajika zaidi kuliko vitu vingine ili kutimiza kitu ambacho Arsene Wenger alishindwa kukifanya.  Najua msimu huu hatuwezi kumdai chochote Mikel Arteta,  tutaanza kumdai baada ya miaka mitatu, muda ambao tutamuuliza ni lini atalipa deni kwa Arsene Wenger?

Kichwani kwa Mikel Arteta kuna swali ambalo linazunguka, ni lini atalipa deni hili ? Wakati akiwa mchezaji,  yeye na wachezaji wenzake walishindwa kumpigania kwa kiwango kikubwa Arsene Wenger ili achukue ubingwa, msamaha pekee ambao Mikel Arteta anatakiwa kuutimiza ni yeye kubeba ligi ya mabingwa barani ulaya na kulipeleka kombe hili sebuleni kwa Arsene Wenger.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tofauti kati ya Uingereza na England

Ligi Kuu England ni ipi hasa?

Soka imeegemea kwenye sifa tu

Wenger: Klabu imara zitaboreka