in , , ,

MGOGORO WA MLUNGULA FIFA

Thabo Mbeki, Ireland ndani

Sakata la mlungula linalohusisha vigogo wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeingia katika hatua mpya, ambapo inadaiwa Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki (wa zamani) ndiye aliidhinisha malipo ya dola milioni 10 ili nchi yake ipate uenyeji wa michuano hiyo 2010.

Hayo yanajiri wakati Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) likiwa limeshaandikisha mashitaka dhidi ya watu 14 na linaendelea na upelelezi dhidi ya Rais wa Fifa, Sepp Blatter ambaye kutokana na shinikizo dhidi yake ametangaza kwamba ataachia ngazi karibuni.

Marekani inaona kwamba fedha ambazo maofisa wa Fifa walikuwa wakilipwa zilikuwa hongo ili kuwezesha mataifa au mashirikisho ya soka ya mabara au nchi kupata waliyokuwa wakitaka kutoka Fifa.

Kadhalika Fifa wanadaiwa pia kutoa fedha pale wanapoona mambo yao hayaendi vyema, na katika maelezo ya karibuni kabisa ni kwamba waliwalipa Jamhuri ya Ireland pauni milioni tano ili kuwazuia wasifungue kesi baada ya mkono wa Thiery Henry kuwakatalia bao na hivyo kushindwa kufuzu kwa fainali za 2010.

Ya Afrika Kusini yamewekwa bayana na Waziri wa Michezo, Fikile Mbalula ameeza kwamba uamuzi wa kutoa fedha hizo ulisainiwa na Rais Mbeki, ambaye baadaye aliondoka madarakani kutokana na chama chake cha ANC kupitia wafuasi wake kumzonga kwa sababu za kisiasa ili aondoke madarakani.

Afrika Kusini, hata hivyo, wanakana kwamba fedha hizo zilikuwa hongo ya kupata uenyeji huo. Madai hayo yameibuka baada ya kuwekwa hadharani barua inayoelekea kuonesha kwamba maofisa walikuwa wakiomba kupatiwa fedha hizo.

Sasa wanadai kwamba fedha hizo zilikuwa kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya michezo kwa Waafrika wanaoishi ng’ambo maeneo ya Caribbean na kwamba kuchapishwa kwa barua hiyo kwenye gazeti la Afrika Kusini la ‘Mail & Guardian’ ni uchochezi tu.

Barua hiyo iliandikwa na aliyekuwa Mkuu wa Chama cha Soka cha Afrika Kusini, Danny Jordaan, wiki tatu kabla ya awamu ya kwanza ya fedha hizo kulipwa mwaka 2007. Maofisa saba wa ngazi za juu wa Fifa na watu wengine saba wameunganishwa kwenye mashitaka ya kudai na kupokea rushwa, wizi na utakatishaji wa fedha.

Goli la Thiery Henry, lililozua utata
Goli la Thiery Henry, lililozua utata

Kuhusu Jamhuri ya Ireland, Ofisa Mtendaji Mkuu wa FA ya huko, John Delaney anasema anaamini walikuwa na kesi na ushahidi mzito dhidi ya Fifa kutokana na mpira wa mkono wa Henry aliyekuwa akiichezea Ufaransa katika mechi ya kufuzu ya 2009.

Anasema kwamba walikubaliana kisheria kuachana na kesi hiyo kwa kukosa fainali za 2010 lakini wakapozwa kwa kiasi hicho cha fedha, kitu anachoona ni haki, lakini Marekani inaona kwamba si kawaida na ni rushwa.

Kwenye mechi hiyo, Ireland walikuwa wamebakiza dakika 16 tu ili waingie kwenye changamoto ya kupigiana mikwaju ya penati ili kubaini nani angeingia kwenye fainali hizo, ndipo Henry akashika mpira wakati akishambulia, mwamuzi akakaa kimya, na Henry akampasia mpira William Gallas aliyesawazisha na kufanya mechi imalizike kwa wastani wa mabao 2-1 na Ufaransa kuvuka.

Makamu wa Rais wa Fifa wa zamani, Jack Warner, amesema katika mahojiano na kituo cha televisheni kwamba hana muda wa kuficha tena siri, bali ataanika yote anayojua juu ya rushwa katika ulimwengu wa soka leo hii.

Warner, 72, amesema anahofia usalama wake, lakini akasema anaihusisha Fifa na uchaguzi mkuu wa kwao Trinidad & Tobago uliofanyika mwaka 2010. Huyu ni mmoja wa watu 14 wanaoshitakiwa na Marekani kwa tuhuma za rushwa na utakatishaji fedha

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

STARS YAJIFUA ADDIS ABABA

PSPF YATOA ELIMU YA MFUKO KWA WAHESHIMIWA MABALOZI, WAJIUNGA NA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI