in

Metacha Ajitathimini Yanga

Metacha

Moja ya magolikipa wazuri sasa hivi  kwa timu ya Yanga ni Metacha Mnata ana ‘Clean Sheets’ nne za ligi lakini pia tumaini la timu ya taifa ya Tanzania.

Ujio wa kocha Cedric Kaze kunaweza kubadilishia upepo wa kipa wa Yanga kama hatachukulia kwa umuhimu mkubwa.

Udhaifu wa wa Metacha katika kuchezea miguu yake yaani ukirudisha mpira utegemee mpira wa ajabu kurudi.

Kwa aina ya mchezo wa Kaze ni mpira wa chini ambao unaendana na mifumo mikubwa kama tunavyoiona katika vilabu vilivyoendelea.

Katika makipa watatu waliopo Yanga Farouk Shikalo pamoja na Ramadhani Kabwili wanauwezo mkubwa wa kucheza mpira wa chini kuliko Mnata.

Hakuna asiyejua uwezo wa Metacha kudaka na kuokoa hatari mbalimbali lakini ukija swala la kucheza mpira ndio mushkeri unaanzia hapo.

Mwenzake Shikalo anaweza kucheza chini na ndio mpinzani wake katika harakati za kugombania namba.

Kwa uwezo vijana hawa wawili hawajatofautiana sana wanazidiana vitu vichache sana kama hivyo ambavyo nimeanza kuvieleza.

Kwa sasa rekodi zinasoma kuwa Metacha ndio golikipa namba moja wa Yanga na hilo halina ubishi kwa uwezo wake wa kudaka.

Sasa anatakiwa aongezee juhudi katika kucheza mipira ya chini ya mguu wake hiyo itamsaidia sana kuweza kukubalika na kupata namba ya kudumu chini ya kocha mpya ambaye anakuja.

Walimu wote waliye na uwezo wa kufundisha kucheza mpira wa chini huwa wanapenda kuanzishia mpira nyuma kabisa kwa kipa.

Kwa Tanzania imekuwa jambo la ajabu sana kumuona kipa akicheza mpira tumezoea kuona mipira ikipaa hewani tu endapo ikifika kwa kipa.

Lakini walimu kutoka nchi mbalimbali wamekuja kubadilisha upepo na sasa vitu kama hivyo tunaviona.

Kunyoa au kusuka kunabakia kwa nyota huyo kama anahitaji kunufaika zaidi anatakiwa aimarike zaidi chini.

Hiyo itamsaidia kuwa na machaguo mengi kwa mwalimu lakini  kama ataendelea na kuwa hodari katika kudaka ila kutambaliza mipira bado mgogoro kutaweza kumuathiri na kumpoteza kabisa.

Ujio wa Kaze kunaweza kuwa faida kwa taifa kwani uhakika wa nyota Farid Mussa ataweza kupata nafasi nyota huyo anacheza mpira mithili ya kocha huyo anavyotaka.

Lakini pia huenda ikawa faida zaidi kwa kiungo Haruna Niyonzima ambaye naye mchezo wake ndio huo yaani kampa kampa tena.

Ujio wake bado unaweza kuwa na faida kwa nyota wengine kama kina Carlinhos, Feisal Salum na hata Yacouba Sogne.

Kazi yake kubwa ya kwanza kuhakikisha timu inacheza vizuri kwa kiwango ambacho kila mmoja atafurahi.

Licha ya kucheza vizuri bado anahitajika apate matokeo yaliyobora ili timu itoke katika ukame.

Kocha huyo ataweza kuchanga vizuri karata zake hadi kufikia kilele cha kuwafurahisha Wananchi?

Kaze anatakiwa ajue kuwa Yanga imekosa ubingwa kwa miaka 3 mfululizo lakini mbaya zaidi atakuwa na mmechi ngumu kabisa dhidi ya mahasimu wao Simba Novemba 7 mwaka huu, yote hayo yapo katika majukumu yake.

Kama akifanikiwa kuleta vitu vyote kwa pamoja basi ataimbwa kama ni mmoja ya watu muhimu kuwa kutokea katika timu hiyo.

Mwenyewe amesema kuwa anakuja kuifurahisha Yanga amejaribu kuangalia baadhi ya mechi ameona nini anatakiwa afanye ili kuipeleka mbele timu.

“Nimeangalia timu katika mechi tano pamoja na zile za kirafiki nimeona hivyo nakuja kuwafurahisha wana Yanga kuanzia katika mpira mzuri,”alisema.

Yanga na Simba ndio timu pendwa zaidi hapa Tanzania hivyo kila kocha akija kipimo chake kikubwa ni mchezo huo.

Baada ya hapo ndio sasa watu wanaangalia lile pira Biriyan na pira kacholi litachezeka.

Swali litabikikuwa Kaze ataimbwa na kuondoka kwa heshima kama Hans Van Pluijm au atatupiwa virago na kufukuzwakama Luc Eymael, hilo swala la kusubiri kwa kuwa mabosi wa Yanga wanaimani kubwa na kocha huyo.

KITU USICHOKIJUA

cedric kaze
Cedric kaze

Yanga walifanya mawasiliano kabisa na Kaze kabla ya kumfukuza kocha wao Zlatko , hawakuwa wajinga kumfukuza huku hawana uhakika wa kocha mpya.

Yanga wanataka kwenda katika mabadiliko wakiwa na kocha ambaye atahakikisha ataleta faraja ya mashabiki pamoja kama ilivyokuwa zamani.

Kocha huyo amepewa baraka zote na viongozi na ndio maana mkataba wa Zlatko ulikuwa wa mwaka mmoja wakitoa nafasi kwa kocha huyo amalize matatizo yake ya kifamili.

Baada ya kuwasiliana naye na kugundua kuwa amemaliza basi wameamua kumpa kazi ya kukinoa kikosi hiko.

Swali la pili je atafanikiwa kuunganisha timu , viongozi watakuwa na subra kama yalivyomapenzi yao kwake ?

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Ngumi

Hii ‘KO’ Na ‘TKO’ Inapatikana Vipi?

Roy Keane

Roy Keane atawavusha ‘Class of 92’?