in , ,

ARSENAL vs BARCELONA JIONI YA LEO…

Je unadhani nani jogoo wa mjini hapa?

Arsenal au Barcelona?

 

Majogoo wawili; mmoja wa shamba mwingine wa mjini. Yupi wa shamba na yupi wa mjini? Mtindo wa uchezaji wa timu hizi mbili unafanana; ni kile Pele alichokiita “mchezo wa kupendeza”( the beautiful game). Kocha Arsene Wenger anasifika kwa gemu la kufurahisha macho- wa mabao yanayofungwa kwa pasi nyingi nyingi na madoido. Wachezaji vijana vijana aliowakuuza yeye mwenyewe toka wakiwa wadogo kama Jack Wiltshire na Theo Walcott aliyeanza akiwa na miaka 17.

Kwa ligi ya England, Arsenal wana sifa ya mpira wa kupendeza. Lakini hawajaambulia chochote toka 2004. Ndiyo, walishinda kombe la FA mwaka jana na mwaka juzi, ila vinginevyo wanahesabika kama hawako vizuri sana. Kocha Arsene Wenger yuko na Arsenal toka 1996 lakini hajawahi kushinda ligi hii ya Ulaya (inayogombaniwa leo). Mara ya mwisho Arsenal kushinda ilikuwa 1994. Kabla ya Arsene Wenger.

Barcelona ukilinganisha si tu kwamba ina wachezaji wakubwa wakubwa, ina mtindo huo wa kupendezesha macho na hushinda mechi na kubwaga kila timu. Kipindi kilichoisha mwaka 2015 Barcelona walishinda taji tano. Tano! Copa del Rey, Liga, Champions League, nk. Sasa juu ongeza washambuliaji wake watatu wakali: Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar Da Silva.

Nimekuja hapa uwanjani kuangalia hali ikoje kabla ya mchezo
Nimekuja hapa uwanjani kuangalia hali ikoje kabla ya mchezo

Linganisha pia makocha. Arsene Wenger tunamfahamu. Hakuwa mchezaji wa kutisha kama wenzake wa Barcelona Pep Gardiola (zamani) na Luis Enrique, wa sasa. Imeelezwa akiwa mdogo, Wenger, alikuwa tu mchezaji wa wastani lakini mwenye tayari na ufundi na utambuzi wa kuongoza wenzake. Aliishia kwenda kusomea uchumi chuo kikuu cha Strasbourg, jambo linalompa sura ya Kiprofesa na weledi katika uchumi wa klabu ya Arsenal. Ndiyo maana wamemudu kujenga uwanja mkubwa maarufu wa Emirates. Arsenal matajiri.

Toka aje Uingereza 1996, Bwana Wenger amesaidia sana kubadili mpira na afya ya wachezaji. Alipoingia alifuta tabia ya wachezaji kulewa ovyo, kulala vibaya na kula bila mpangilio. Kinyume na Jose Mourinho- asiyejali sana wachezaji chipukizi- Wenger hupenda sana kukuuza na kujenga wachezaji wachanga wachanga kuwa imara kwa mfano Thiery Henry na Theo Walcott.

Kocha wa Barcelona , Luis Enrique ana historia na nyota ya ushindi. Alikuwa mchezaji mkubwa enzi zake akichezea timu za Real Madrid na Barcelona na kushinda lukuki ya vikombe miaka yote ya 1990 na kitu. Alikuwa pia mchezaji wa taifa la Spain (1992, 1998, 2002) alipofunga mabao 12 ndani ya mechi 62 za Kombe la Dunia la FIFA. Toka aingie ukocha wa Barcelona mwaka juzi ameendeleza hulka ya kushinda mechi na kujaza vikombe kila mwaka – tabia iliyokuwepo vile vile enzi za kocha Pep Gurdiola.

Leo ni leo. Tayari vyombo vya habari hapa Uingereza vimeanza kuwanukuu makocha hawa wakirushiana mishale. Kocha wa Barcelona kakaa kimya akijaribu kutojibu maswali aliyoulizwa moja kwa moja. Kwa mfano badala ya kuelezea mbinu Enrique karejea kauli ya Barcelona kuwa “lazima kushinda hata iweje” kwamba hilo “ni kawaida na ndiyo mantiki.” Mwenzake Wenger kaeleza Arsenal watafunga mabao ila tatizo litakuwa kuwazuia Barca nao wasifunge.

 

 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Chelsea wawaogesha Man City

Tanzania Sports

Wenger: Barca wanapita