in , ,

Mbona Volleyball imekufa? anauliza JENERALI ULIMWENGU

Akiwa mkuu wa wilaya ya Hai alihakikisha timu nyingi za shule za msingi na sekondari zinashiki mashindano maarufu ya Kombe la Bonite kila mwaka.

Hivi majuzi nilishiriki mjadala mzito uliofanyika Chuo Kikuu Huria OUT Kitivo cha Sanaa  katika kusherekea  miaka ishirini tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.

Mtoa mada mkuu katika mjadala huo alikuwa Jenerali Twaha Halfani Ulimwengu.

Ndugu Ulimwengu alikuwa akizungumzia kuporomoka kwa  kasi  kwa maadili  ya Watanazania hususani viongozi wetu. Akimkaribisha Ndugu Ulimwengu mmoja wa viongozi waandamizi wa Chuo Kikuu Huria Profesa Mbwiliza hakusita kumwagia sifa kedekede  kwa  mtoa mada  na haswa misimamo yake katika utetezi wa wanyonge  katika makala zake na hata kuwa tayari kujiuzulu pale anapoona haki haitendeki.

Sio nia yangu kujadili nini alichosema mtoa mada  licha ya ukweli kukubaliana nae kwa yale aliyoyasema haswa kwa upande wa  kuoza kwa maadili. Rushwa imekithiri mno miongoni kwa jamii kiasi cha kutisha.

Sio ajabu kuona baba, mama na watoto ndani ya nyumba moja wakishiriki kwa nguvu zote katika masuala ya rushwa. Ni kweli ukiona msitu au nyika hauna nyoka  hata mmoja basi hapo kuna kasoro lakini  ukiona msitu kuna nyoka wengi  zaidi basi hapo lazima hatua madhubuti zichukuliwe  kwani madhara yake yatakuwa makubwa. Ndugu Ulimwengu aliongelea mengi ikiwa pamoja na matumizi mabaya ya madaraka  abuse of power ya viongozi wetu ikiwa pamoja na mauzo ya nyumba za serikali.

Lengo langu  ni kuzungumzia yale aliyoniuliza mara tu aliponiona katika ghafla ile. Vipi mbona volleyball inakufa? Lilikuwa ni swali nzito kwangu  na haswa ukuitilia maanani ndugu Ulimwengu alikuwa mdau mkubwa wa Volleyball nchini.

Akiwa mkuu wa wilaya ya Hai alihakikisha timu nyingi za shule msingi na sekuondari zinashiki mashindano maarufu ya Kombe la Bonite kila mwaka.

Akiwa naibu Mkurugenzi maendeleo ya michezo nchini alihakikisha timu za taifa na vilabu vinashiriki mashindano mbalimbali  ya kimataifa ikiwemo  klabu bingwa Afrika.

Kuna wakati Ndugu Ulimwengu aliamua kuongozana na timu yetu hadi Lusaka kwa treni  na kurudisha tiketi ya ndege aliopewa na serikali. Sina hakika lengo lake lilikuwa nini lakini labda alitaka nae apate shida kama sisi wakati tukienda kupigania taifa letu kimichezo mjini Lusaka.  Ni viongozi wachache wanaodiriki kufanya hivyo

Nilichoweza kumjibu Ulimwengu ni kuwa Volleyball haijafa kwani tuna mpango wa miaka mitano tukishirikiana na Shirikisho la Dunia Mpira wa Wavu  FIVB  kundeleza waalimu na waamuzi .

Pia tuna mkakati mwingine wa kuendeleza vipazi vya watoto kupitia COOL VOLLEY .

Vifaa vya mpango huo tayari  vimeshawasili na wakati wowote tutazindua rasmi mpango huo utakaolenga zaidi watoto wa shule za msingi.

Mwisho tuna mpango wa kufanya kongamano kubwa la wadau wetu wakiwemo waliowahi  kuongoza volleyball  mapema mwakani ili tupate mawazo yao  katika maendeleo ya mpira wa wavu nchini. Miongoni mwa wadau hao ni  Balozi Juma  Volter Mwapachu, Major General Rowland Leslie Makunda, Patrick Jacob Sombe na Balozi Abdul Cisco Mtiro.

Pia kutakuwepo na wafanyabiashara maarufu kama Reginald Mengi waliofanikisha maendeleo ya volleyball  kupitia kampuni yake tanzu ya BONITE BOTTLERS

Makala hii imeandikwa na Muharame Mchume

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Dar to host charity half Marathon

Fanfare as league kicks off