in , ,

Mayweather avuliwa ubingwa WBO

Bondia wa Marekani, Floyd Mayweather amevuliwa mkanda wake wa ubingwa wa Shirikisho la Ngumi Duniani (WBO).

Mayweather (38)alitwaa taji hilo baada ya kumpiga bondia wa Ufilipino, Manny Pacquiao Mei mwaka huu. Amevuliwa taji kutokana na kushindwa kulipa ada ya pambano hilo – pauni 128,000 iliyotakiwa ilipwe kabla au ilipofika Julai 3.

Mayweather hutamba binafsi kwamba ni mtu mwenye kiasi kikubwa cha fedha asizojua afanye nazo nini, ikizingatiwa ndiye anaongoza miongoni mwa wanamichezo wote duniani kwa utajiri.

Baada ya kumshinda Pacquiao kwenye pambano lililokuwa na utata, Mayweather aliahidi kuachia mikanda yake yote ili kutoa fursa kwa mabondia wachanga kuipigania.

Taarifa ya WBO imesema kwamba baada ya Mayweather kwenda kinyume na matakwa ya ulipaji ada, kamati haikuwa na jingine la kufanya zaidi ya kubatilisha ubingwa wake.

Baada ya pambano hilo, Pacquiao alidai kwamba alikosa udhindi kwa sababu alikuwa anaumwa bega, na muda mfupi baadaye alifanyiwa upasuaji.

Utata mwingine wa pambano hilo ni madai kwamba alama za kona ya Pacquiao zilitolewa kwa Mayweather kimakosa na majaji, na kama ndivyo ingemaanisha mshindi ni Mfilipino yule.

Mayweather bado anashikilia mikanda ya Chama cha Ngumi Duniani (WBA) na wa Baraza la Ngumi Duniani (WBC) kwa uzani wa Welterweight. Hata hivyo, bondia huyo ana hadi Julai 20 kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa WBO.

Mayweather anatarajia kucheza pambano moja kabla ya kuachia ngazi, na imepangwa lifanyike Septemba 12 japokuwa mpinzani wake bado hajatajwa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

MZOZO WA MLUNGULA WACHEMKA:

Sterling aonesha jeuri