in

Maswali magumu kuahirishwa mechi Simba vs Yanga

Simba vs Yanga

Pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara lililopangwa kufanyika Mei 8 mwaka huu na kuzikutanisha timu kubwa nchini Tanzania Simba na Yanga halikufanyika. Mchezo huo ulikuwa ni sehremu ya mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania ulishikana kufanyika kutokana na mgogoro wa muda ulioibuka kati ya Shirikisho la Soka TFF na klabu ya Yanga.

Kiutaratibu ratiba za mechi za Ligi Kuu zinapangwa na Bodi ya Ligi. Mei 8 ilijulikana miezi mitatu iliyopita kuwa ni siku ambayo mashabiki watashuhudia vinara wa soka nchini Simba na Yanga wakimenyana kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Kwanini sababu ya kubadilishwa muda wa mchezo hazikutajwa bayana?

Taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka TFF saa chache kabla ya kuanza mchezo huo haielezi sababu za msingi za kubadilisha muda wa mchezo badala yake imedai kuwa ilipokea maelekezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Michezo na Wasanii kusogeza mbele muda wa mchezo kutoka saa 11 jioni hadi saa moja usiku.  

Mchezo huo ulikuwa umepangwa miezi mitatu iliyopita ikiwa na maana ulijulikana kwa mamlaka za serikali,wadau wa michezo na wengineo. Hata hivyo hadi sasa mambo yamebaki yanaelea hewani hakuna sababu nzito iliyotajwa na TFF au serikali kutolea maelezo yoyote.

Je, fedha za viingilio zilizolipwa na mashabiki zinakwenda wapi?

Mashabiki wa timu zote mbili walikuwa wameshaingia uwanjani mapema kusubiri muda wa mchezo yaani saa 11 jioni, lakini tangazo la ghafla kutoka TFF kuwa mchezo ungechezwa saa moja usiku lilikasirisha mashabiki wa Yanga na hivyo kuungana na timu yao kutoka nje ya uwanja wa Benjamin Mkapa kupinga kubadilishwa muda wa mchezo kienyeji na kinyume cha Kanuni ya 15(10) ya Ligi Kuu inayohusu utaratibu wa kubadili muda mwa mchezo.

Kanuni hiyo inajieleza, “Mabadiliko yoyote ya muda wa kuanza mchezo  yatajulishwa ipasavyo  angalau saa 24 kabla ya muda wa awali. Baadaye TFF ililazimika kutangaza kuahirisha mchezo huo.”.  Hata hivyo swali linalotamba kwa sasa ni namna gani fedha za mashabiki zitarudishwa na wai zitakwedna ikiwa hazijarudishwa?  

Kwa sababu mabomu ya machozi yalitumika kuwatimua washabiki na ndani ya uwanja walifukuzwa kwa kuzimiwa taa. Huu ni ukosefu wa heshima na usumbufu mkubwa unaotoka kwenye taifa ambalo linaonekana kuongozwa na watu wasio na adabu kwa mashabiki wa soka. Mbali na viingilio nani atafidia muda waliotumia mashabiki kuanzia saa tatu asubuhi ambao aliingia uwanjani hapo kusubiri pambano.

Je, hatua gani zitachukuliwa dhidi ya waliohusika kutia hasara kwa kusababisha mgogoro?

Tanzania Sports
Baadhi ya maoni mitandaoni

Hili ni swali ambalo litapatiwa majibu ndani ya sikua chache zijazo. Tanzaniasports inafahamu kuwa TFF na Bodi ya Ligi pamoja na viongozi wa timu za Yanga na Simba watakuwa na kikao Mei 10 na kutolea tamko juu ya kadhia nzima. Vyovyote iwavyo ni lazima watu wawajibike katika suala kama hili kwa watu wote waliohusika na kusababisha vurugu hivyo kulilazimsiha jeshi la polisi kutumia nguvu kuwafukuza mashabiki waliokuwa wakidai hela zao.

Ni Mamlaka gani ya serikali inaweza kuingilia masuala ya soka kokote duniani?

Jibu ni mamlaka ya hali ya hewa na vyombo vya dola yaani ulinzi na usalama. Kwa majukumu ya vyombo hivyo, idara ya Hali ya Hewa inaweza kutoa tahadhari juu ya kutokea mvua kali,barafu na sababu zingine ambazo zinafana nazo kuwa chanzo cha kuahirishwa mchezo. Kwa upande wao vyombo vya ulinzi na usalama vinaweza kuliagiza shirikisho la soka TFF kuahirisha mchezo kutokana na sababu za usalama, mfano tishio la kigaidi,milipuko na mabomu na kadhalika.

Tanzania Sports
Baadhi ya maoni ya mitandaoni

Tanzaniasports limezungumza na mtaalamu mmoja nchini Tanzania ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake, alisema, “Kuna shida kubwa ya dunia ambapo kitaalamu tunasema kuchukua vihatarishi na kufanya mambo mengi nje ya utaratibu. Hapa pana shida kubwa mno ndio chanzo kikuu, hii ndiyo tunaweza kufanya Risk and Compliance analysis. Hivyo ningeshauri TFF iwe sababu ya kuanzisha kitengo cha hiki cha Risk and Compliance Unit. Hebu fikiria pangezuka vurumai kubwa kati ya timu zote na vyombo usalama, nani angewajibika kwa muktadha huo? Pia katika kufanya risk and compliance evaluation kuna suala la kulipa fidia kwa timu husika na mashabiki, je watawezaje kupima hali hii?  Ni wazi waliohusika na suala hili ambalo limeleta aibu katika taifa hawapaswi kuendelea kuwepo katika nafasi walizonazo kiuongozi, nadhani wanaweza kusaidiwa kama ambavyo amewahi kusema Rais Samia Suluhu kwa aliyekuwa waziri wa Tamisemi, Seleman Jaffo.”

Je Yanga wanapaswa kupongezwa?

Kimsingi uongozi wa klabu ya Yanga unapaswa kupongezwa kwa kuchukua uamuzi mgumu na makini kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazoongoza Ligi Kuu Tanzania msimu wa 2020/2021. Yanga waliamua kusimamia kanuni. Hilo lina maana kuwa TFF na wadau wake wakuu wametumiwa ujumbe wa umuhimu wa kuzingatia kanuni,sheria na busara hasa wakati mgumu kama huu.

Pili, TFF na wadu wakuu wanatakiwa kuona maumivu wanayopata klabu zinazobadilishiwa muda katika dakika za majeruhi kupitia gharama za timu,viingilio vya mashabiki na wapenzi wa mpira.

Hivyo ni wakati wa TFF na Bodi ya Ligi Kuu kuona umuhimu wa kuwaheshimu mashabiki na vilabu vinavyocheza Ligi Kuu kwa sababu huko nyuma kanuni zimepindishwa mara nyingi, ikiwemo pambano la Yanga na Azam ambalo TFF ilitoa taarifa nje ya utaratibu wa saa 24 kwa mujibu wa kanuni, lakini vilabu viliamua kutii hilo.

Tatu, TFF wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kusimamia kanuni za kuendesha mpira wetu Tanzania ikiwemo kutunga sheria inayoangalia mazingira kama ya Mei 8 na kusababisha pambano liyeyuke pamoja na kuacha kuendesha mpira wa miguu kwa mazoea.

Nini umuhimu wa muda  wa mchezo kwa timu?

Kwa mujibu wa kocha wa zamani wa Yanga ambaye amepata kulalamikia tabia yakuahirisha mechi za Ligi Kuu holela, Mwinyi Zahera alipata kusema, “Unapojua muda wa mchezo ndio unapanga mpango wa siku ya mechi, kwamba wachezaji wale chakula saa ngapi, wapumzike saa ngapi, na kuondoka kwenda uwanjani saa ngapi. Na hata mazoezi yako kabla ya mchezo husika unapaswa kujua unayafanya kujiandaa kucheza saa ngapi. Hivyo si suala la kubadili muda wa mchezo kuna matokeo makubwa sana kwenye viwango vya timu katika mchezo husika.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Teddy Mapunda

Nazikumbuka amsha amsha za Teddy Mapunda Taifa Stars

Mbappe

Nini kitatokea kwa Kylian Mbappe?