in

Mashabiki wa Simba SC siyo wavumilivu ?

Simba vs Yanga

Sare ambayo ilionekana kutowaridhisha mashabiki wa Simba SC kiasi cha wao kwenda kwenye gari ya timu na kuanza kuwasema kwa maneno mabaya wachezaji waliokuwa ndani ya gari ya timu.

Tuanze kujiuliza kwa swali hili kwanza, je mashabiki wa Simba SC siyo wavumilivu ? Unaweza ukajiuliza sana kwanini nauliza swali kama hili. Sababu pekee ambayo imenisababisha niulize hili swali ni mashabiki wa Simba SC.

Mashabiki wa Simba SC ndiyo wamenifanya nijiulize hili swali. Mashabiki ambao wamenikumbusha kipindi ambacho Simba SC walienda kucheza mechi Mwanza dhidi ya Mbao FC kipindi cha Patrick Aussems.

Matokeo ya mechi ile yaliwasababisha mashabiki wa Simba SC kuwaponda kwa makopo wachezaji na benchi la ufundi la Simba SC. Kwa macho yangu nilishuhudia kocha mkuu, wachezaji na baadhi ya viongozi wa Simba SC wakirushiwa chupa za maji ya kunywa.

Sababu ilikuwa moja tu, hawakuridhika na matokeo ya mechi ile dhidi ya Mbao FC. Lakini baada ya mechi hiyo Simba SC walifanya vyema mpaka wakapata nafasi ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu, Patrick Aussems huyo huyo aliwafikisha Simba SC katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Jumapili iliyopita Simba SC walikuwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam FC. Mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya magoli 2-2. Sare ambayo iliwafanya Simba SC kuvutwa nyuma kidogo kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu Tanzania.

Sare ambayo ilionekana kutowaridhisha mashabiki wa Simba SC kiasi cha wao kwenda kwenye gari ya timu na kuanza kuwasema kwa maneno mabaya wachezaji waliokuwa ndani ya gari ya timu.

Waliongea kwa hasira sana, walionekana kuchukizwa na kiwango cha wachezaji ambao waliwaita wazembe, walionekana kuchukizwa na matokeo ya mechi hiyo mpaka ikafikia wakati kuwaambia wachezaji wakatwe mishahara kutokanana na kiwango cha mechi hiyo.

Mimi siwalaumu mashabiki wa Simba SC. Mashabiki ambao wanaamini timu yao inawachezaji bora kuzidi timu yoyote kwenye ligi kuu Tanzania bara.

Mashabiki ambao wanaamini kuwa hakuna timu ambayo inaweza kuwazuia Simba SC kwenye mbio hizi za ligi kuu Tanzania bara kwa sababu ya ubora wa kikosi chao.

Mashabiki ambao wanaamini kabisa kila mechi kwao ni ushindi. Wanastahili kushinda kila mechi kwa sababu ya ubora wa kikosi chao. Hakuna kikosi kwenye ligi kuu Tanzania bara kinachoweza kupata sare mbele ya Simba Sc.

Mashabiki wa Simba Sc wanaamini kuna uwekezaji mkubwa ambao umefanyika ndani ya timu. Uwekezaji ambao wanataka usadifu matokeo ndani ya uwanja.

Uwekezaji wao mkubwa uendane na matokeo makubwa ndani ya uwanja. Kipindi ambacho timu inapata matokeo ambayo siyo ya kuridhisha mashabiki wanawakumbusha wachezaji wao thamani ya timu yao.

Tukirudi kwenye swali ambalo nimeuliza mwanzo kama mashabiki wa Simba Sc siyo wavumilivu, nitakujibu kuwa mashabiki wa Simba SC wanaiona thamani ya jezi ya Simba SC ni kubwa.

Jezi ambayo ina thamani kubwa ya ushindi ndani ya uwanja ndiyo maana wanatumia muda mwingi kuwakumbusha wachezaji wao thamani ya jezi ya timu ya Simba SC.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Azamfc

Tadeo Lwanga na Jonas Mkude waanze pamoja…

Ndayiragije

Tumlaumu kocha wa taifa stars au TFF?