in , ,

Martinez afikiriwa kumrithi Wenger

Kocha wa Everton, Roberto Martinez ameanza kufikiriwa na wakubwa wa Arsenal kuwa ndiye chaguo sahihi la kumrithi Arsene Wenger.

Martinez, Mhispania aliyeoa mke Mwingereza alijiunga na Everton akitoka Wigan Athletic walioshuka daraja msimu uliopita, lakini anawavutia sana wadau wa Emirates kwa tabia zake uwanjani na hata nje.

Hata jinsi alivyopokea kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Arsenal wikiendi iliyopita kwa namna ya kipekee akionesha heshima na utulivu badala ya hasira na fujo, kimemwongezea maksi miongoni mwa wakubwa wa Arsenal.

Hata hivyo, kukubalika huko kwa Martinez hakumaanishi kwamba Wenger anaondoka kesho au keshokutwa, hapana. Wenger anakaribia kuanguka saini kwa ajili ya kuendelea kuwanoa Arsenal kwa miaka mingine miwili.

Hata hivyo, wamiliki na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Arsenal wameamua kuanza kufikiria mrithi wa Wenger ili wasikutwe na mshangao wakikosa la kufanya ikitokea siku Wenger kweli anaondoka.

Kwa hiyo wamekuwa wakikuna vichwa juu ya nani angeweza kuwa chaguo lao, na jina la Martinez linashika namba moja kwa sasa, wakipendezwa na aina ya soka analowafundisha vijana wake, pasi kama zile ambazo washabiki wa Arsenal wanazipenda na wamezizoea chini ya Wenger.

Kadhalika Martinez ni muumini wa kuhamasisha kuendeleza ukuzaji vipaji kupitia timu za vijana, falsafa ambayo Arsenal wamekuwa nayo kwa muda mrefu na hata nyota wao wengi waliowakimbia walikuwa mazao yao.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Ronaldo mwanasoka tajiri zaidi

Spurs wachezea kichapo nyumbani