in , ,

Man City wafufukia Kombe la Ligi

 

*Swansea, West Ham, Reading nje

*Arsenal, Man U, Liver, Spurs leo

 

Manchester City wameibuka na ushindi wa 4-1 kwenye michuano ya Kombe la Ligi dhidi ya vibonde Sunderland, baada ya kuwa na wakati mgumu walipofungwa na Juventus kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na West Ham kwenye Ligi Kuu ya England.

Mabingwa hawa watetezi wa Capital One Cup wanaofundishwa na Manuel Pellegrini waliingia kwa hasira kwenye mechi yao ya raundi ya tatu dhidi ya Sunderland, na kuongeza machungu na pengine shinikizo la kuachia ngazi kwa kocha Dick Advocaat.

Pengine ushindi huu utawarejesha City katika kasi waliyoanza nayo Ligi Kuu kwa kushinda mechi tano mfululizo kwa kiwango kizuri cha mabao, kabla ya kuangukia pua kwa Juve na West Ham. Sergio Aguero aliyetoka kwenye majeraha alifungua kitabu cha mabao kwa penati baada ya Patrick van Aanholt kumchezea vibaya Jesus Navas.

Ingizo jipya, Kevin de Bruyne alitikisa nyavu akimshinda kipa wa zamani wa Arsenal, Vito Mannone, kabla ya  Raheem Sterling kufunga lake. Ola Toivonen alifunga bao la kufutia machozi kabla ya Manone kujifunga.

 

MATOKEO MENGINE CAPITAL ONE CUP

Matokeo ya mechi nyingine.
Matokeo ya mechi nyingine.

Katika mechi nyingine, kocha Tim Sherwood wa Aston Villa amefarijika kwa kuweza kupata ushindi muhimu msimu huu, pale walipowafunga watani zao wa jadi jijini Birmingham, klabu ya Birmingham City

Villa walipata bao moja lililotiwa kimiani na Rudy Gestede, ambapo mshambuliaji huyo wa Benin alipiga kiki kali baada ya kupokea majalo kutoka kwa beki wao wa kushoto, Jordan Amavi, akiwa umbali wa yadi 10.

Wakicheza nyumbani, Fulham walipoteza mechi dhidi ya Stoke kwa 1-0 na kutupwa nje ya mshindano, Hull wakatumia vyema uwanja wa nyumbani kuwamaliza Swansea 1-0 wakati Leicester nao walifaidika nyumbani kwa kuwapiga West Ham 2-1.

Middleborough kadhalika walitumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kuwatandika Wolves 3-0, Preston wakatoshana nguvu nyumbani kwa 2-2 na Bournemouth kabla ya wageni kushinda kwa mikwaju 3-2 ya penati. Reading walishindwa kuchanua nyumbani baada ya kuchapwa 2-1 na Everton.

Leo Tottenham Hotspur wanawakaribisha watani zao wa jadi wa London Kaskazini, Arsenal; Manchester United wanawakaribisha Ipswich, Liverpool ni wenyeji wa Carlisle, Chelsea wakisafiri kucheza na Walsall na Norwich wanawapokea West Bromwich Albion.

Katika mechi nyingine, Sheffield Wednesday wanaposafiri hadi Newcastle, Southampton wanafunga safari kucheza na MK Dons huku Crystal Palace wakiwasubiri Charlton.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Costa kifungoni, Paulista huru

Tanzania Sports

Carneiro aondoka Chelsea