in , , ,

Man City out Kombe la Ligi

Manchester City wamevuliwa ubingwa wa Kombe la Ligi na kutupwa nje ya michuano hiyo ya soka ya tatu kwa ukubwa nchini England.

Katika hali ya kushangaza, walitolea na Newcastle ambao msimu huu walianza vibaya na zaidi ya hayo jana kocha Alan Pardew aliingiza uwanjani kikosi chenye wachezaji chipukizi na wasio na uzoefu na mechi kubwa.

Hata hivyo, walikuwa ni hao hao Newcastle waliomfadhaisha kocha Manuel Pellegrini kwa kuwachapa wazoefu wake 2-0, na sasa amesema lazima timu yake ifanye vizuri.

Man City walikuwa wanachukuliwa kuwa wazuri sana msimu huu baada ya kusajili wachezaji wawili wawili au zaidi wenye sifa kubwa katika kila nafasi.

Hii ni mara ta kwanza kwa Newcastle kupata ushindi Etihad kati ya mara 12 walizofika uwanjani hapo. Walipata bao la kwanza kupitia tineja Rolando Aaron kwa kupiga mpira kiufundi ukatoka kona moja hadi nyingine na kujaa kwenye kona ya mbali ya goli.

Hata kipa wao chipukizi, Rob Elliot aliwazidi maarifa wachezaji wazoefu wa Man City na wakati wakijipanga kurejesha bao hilo, nahodha Fabricio Coloccini akatumbukiza la pili kabla ya nusu ya kwanza kumalizika.

Pardew atakuwa amefarijika sana, kwani washabiki walikuwa wakilia atimuliwe, baada ya kuanza ligi vibaya. Hata hivyo, mechi mbili zilizopita walishinda na ushindi huu wa michuano ya Capital One Cup utainua zaidi ari na kujiamini kwa wachezaji wake.

Newcastle sasa watawavaa Tottenham katika hatua ya robo fainali, wakitafuta kuingia nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 1975/76 na ni mara yao ya kwanza kuingia robo fainali ya mashindano yoyote ya nyumbani chini ya bosi Pardew.

Pellegrini amesema timu yake lazima iamke na kufanya vyema, kumaliza mdororo ulioshuhudia wakitoka sare na CSKA Moscow kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufungwa 2-1 na West Ham, matokeo ambayo hayakutarajiwa kabisa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Valdes awazodoa Liverpool

Chelsea, Arsenal safi