in

Mambo yalivyo kwenye dili za usajili wa wachezaji

Baadhi ya wachezaji waliohama vilabu

Ni timu gani ya EPL inafanya usajili mzuri? Timu ipi inaambulia  usajili mbaya? Ni usajili upi unaoshangaza zaidi? Mchezaji gani  mpya anapanda bei ya mauzo yake? je, usajili wa bei mbaya ni  chanzo cha mchezaji kufanya vibaya? Je, ni nani anayefukuzia kila  hatua ya mchezaji kuhamia timu fulani? 

Hayo ni miongoni mwa maswali ambayo yanaulizwa na wadau wa  michezo wakitaka kufahamu undani wa usajili wa wachezaji kila  dirisha la usajili linapofunguliwa hadi kufungwa kwake.  Wanataka kufahamu kinachokuwa nyuma ya pazia. 

Baada ya usajili kadhaa kufanyika sehemu mbalimbali za miji  inakotoka klabu inayoshiriki Ligi Kuu England kufumngwa  jumatatu ya wiki iliyopita, Tanzaniasports, imefanya uchunguzi  na kupata majibu ya maswali hayo yote hapo juu kupitia  mawakala wa wachezaji ambao ambao wanasimamia dili za usajili  wa wateja wao. 

Kwa siku kadhaa, Tanzaniasports imetumia maswali 15  kuwauliza mawakala 18 kwa nyakati tofauti, na kwa masharti ya  kutotajwa majina yao walikubali kuzungumia undani wa dili za  usajili kiungwana na kubainisha kinagaubaga.  

Aidha, tumewauliza ikiwa wanapokea kitita kikubwa cha fedha  kuliko uhalisi wa kazi yao, kutokana na malalamiko yaliyotolewa  na Gary Lineker mwanzoni mwa wiki hii ambaye amedai kuwa ni  wakati sasa sheria,kanuni na taratibu za usajili wa wachezaji  zibadilike, kwani mawakala wanatakiwa kulipwa na upande  mmoja tu, badala ya sasa ambapo wanalipwa fedha na pande 

nyingi kwenye usajili mmoja. Sahau kuhusu “nioneshe fedha”. Ni  wakati wa kuwaonesha majibu. 

1.Usajili upi ni bora zaidi? 

Tanzania Sports
Sehemu ya wachezaji wapya kwenye vilabu vya EPL

“Kwa kuzingatia kuongeza hadhi ya klabu, hisia za kupenda na  utayari wa kulipa, nafikiri inachukua mapigo kadhaa; mpango wa  muda mrefu unaweza usilete faida katika timu, lakini mpango  mfupi unahitaji kuangalia matokeo yaliyopo tayari kwa sasa. Ni  mchezaji nyota, ameshajijenga tayari. Everton haisajili wachezaji  waliokataliwa na timu sita za juu, wamesajili mchezaji wa  kiwango cha juu kama yuko bora kiafya na anahamasishwa” 

Huo sio wakati ambao James Rodriguez, ambaye amekuwa  chachu ya mwanzo mzuri wa Everton katika msimu wa  2020/2021, kutajwa katika dili la usajili wa klabu hiyo yenye  makazi katika viunga vya Merseyside. 

Nyota huyo kutoka Colombia amepata asilimia 22 ya kura kutoka  kwa mawakala. “Amefanikiwa kuiboresha Everton na  amewafikisha kwenye ngazi nyingine ya juu,” anasema wakala  mmoja.  

Ingawaje nyota wa Liverpool Thiago Alcantara ameibuka na  asilimia 28 ya usajili bora zaidi, “Mchezaji mahiri kabisa  amepatikana kwa bei ndogo na dau lake lilipangiliwa vema.”  Anasema wakala mwingine, na kumekuwa na sifa kedekede  kutoka Everton kuhusiana na usajili wa Thiago. 

“Allan yupo Everton anaongeza ubora kwenye klabu hiyo. Angalia  takwimu zake akiwa Italia jinsi anavyopora mipira kutoka kwa  wapinzani wake. Ni matunda ya fedha waliyolipa kupata huduma  inayowapa wanayohitaji katika timu yao,” anasema wakala  mmoja.

”Allan kwa Everton, kuanzia vyumba vya kubadilishia nguo,  uwepo wake uwanjani, yuko upande huu au ule, lazima akuoneshe  ubora wake. Carlo Ancelotti anamfahamu kijana huyo na hakika  atapandisha thamani ya Everton kwa sasa,” anaongeza wakala  mwingine. 

Mawakala wengi wameitaja klabu ya Newcastle United imetoa  fedha ambazo zimeleta huduma mzuri kutoka kwa Callum Wilson,  mshambuliaji asiyetia shaka EPL kutoka Bournemouth kwa pauni  milioni 20. Upande mwingine dili la usajili lililotazwa ni ujio wa  Gareth Bale katika klabu ya Tottenham Hotspurs, “kwa sababu  kinachomaanisha kwa Spurs na Mourinho wametaka usajili huo  uende kwao” na Thomas Partey kujiunga Arsenal siku ya  kufungwa dirisha la usajili. Mawakala wamemwita Thaoms Partey  ni bingwa wa kubadili matokeo. 

2. Je, upi ni usajili mbovu zaidi katika dirisha hilo? 

Maneno mawili; Edinson Cavani. “Je usajili huo unaonesha  maana ya matumizi sahihi ya bajeti? Man United watafanya  mambo mengi kwa kipindi atakachokuwepo klabuni hapo? Kumleta kwenye kikosi chao inaonekana haina maana kabisa. Ni  dili bovu.” Anasema wakala mmoja. 

Baadhi ya mawakala wameita usajili wa Cavani ni wa papara, licha  ya nyota huyo raia wa Uruguay kupata asilimia 28. Wakosoaji  wanasema uamuzi wa kumsajili Cavani ni hasara. “Muda wa  kumsajili, mawakala, umri, mshahara, kila kitu. Ni kama  „tutawezaje kuuza jezi sehemu nyingine duniani? 

Usajili mwinginde uliofanyika Old Trafford ni Donny van de Beek,  ametajwa na mawakala kadhaa, ingawa maoni yao hayana cha 

kufanya dhidi ya uwezo wake, na mikakati gani waliyonayo Man  United kwenye usajili huo.  

“Sielewi Van de Beek. Ni mchezaji mzuri lakini sio aina ya wale  wanaohitajika Man United. 

Kuna pauni milioni 35 za Wolves zimetumika kulipia katika usajili  wa Fabio Silva, “kuwa mshambuliaji wa akiba” umetajwa na  wakala mmoja, wakati maswali mengine ikiwa Arsenal  watanufaika na fedha walizowekeza kwa usajili wa Thomas  Partey. 

Kwa ujumla, ingawa kuna hisia kwamba mlipuko wa ugonjwa wa  corona umechangia klabu kuwa waangalifu kwenye ,matumizi ya  makubwa ya fedha, ikiwa na maana mawakala hawakuwa na  machaguo mengi kwenye suala la kuwapeleka au kuwauza wateja  wao.  

“Hakuna usajili mbaya sana,” anasema wakala mmoja. “Klabu za  Ligi Kuu zimejaribu kuhakikisha zinanunua wachezaji  wanaohitajika kwa bei nafuu na kujizuia kusajili kwa gharama  kubwa. Ikawa sawa na kucheza kamari. Zimesajili wachezaji  wenye viwango vya juu na kuwa na thamani ya kuuzwa pia. Lakini  kama nikitaja jina, basin i Nelson Semedo.” 

Nyota huyo kutoka Ureno amenunuliwa kwa pauni milioni 27.6  kuchukua nafasi ya Matt Doherty. Kiuhalisi, uamuzi wa Wolves  kumuuza Doaherty kwenda Tottenham umeelezwa kuwa wa  hovyo, ambapo mawakala wanasema hawaelewi kwanini klabu  hiyo ilikubali kumuuza Doherty, na namna gani ataweza kuingia  katika mfumo wa Spurs, ikikumbukwa nafasi ya anayomudu ni  beki wa kushoto kuliko beki wa kulia.

Usajili wa Cavani sio pekee ulioitwa wa hovyo. “Totenham  wamemchukua Carlos Vinicius kwa mkopo wa msimu mmoja.  Mpango wao ulikuwa kumchukua Ollie Watkins na yeye alitaka  kujiunga Spurs, lakini Daniel Levy hakuridhishwa na dau  lililotakiwa kumsajili na masharti ya kucheza kikosi cha kwanza.  Daima usajili wa dakika za mwisho unaziba mapengo, sio lazima  kumpata mchezaji sahihi au klabu husika.” Anasema wakala  mmoja. 

3. Ni usajili upi umeshangaza zaidi? 

“Chelsea wamenishangaza zaidi usajili wao. Hatujaona usajili  sampuli ya Kai Havertz kipindi hiki. Ana miaka 21, ni mchezaji  mzuri na walikuwa tayari kulipa gharama zozote. Wameonesha  ubabe wao kwenye usajili, lakini wametengeneza presha kwa  kocha wao Frank Lampard.  

Usajili wa Partey umetajwa mara nyingi na mawakala, amepata  asilimia 25, kwa sababu ya gharama za usajili na mshahara wake,  ambapo wengi wamesema si kawaida ya Arsenal kulipa mshahara  wa namna hiyo hasa baada ya kuhisi dili lingekufa. 

“Kwa sababu wamefanikisha usajili. Partey hakuwa mchezaji wa  bei nafuu, mshahara wake ni mkubwa mno, sikufikiria kabisa  kama Arsenal wanaweza kukubali kumlipa. Hainingii akilini  kwenye dili hili kwa jinsi Arsenal walivyo.  

Akiwa amepata asilimia 19 ya kura, kurejea kwa Gareth Bale  kwenda Spurs ni jambo kubwa. “Sio kwa sababu Totenham  wamemsajili Bale, walichotoa ni halali. Lakini ukweli ni kwamba  madili mengi ya usajili hayakuwa yanaenda vizuri, hivyo inabidi  usajili kwa vile huna namna,”aanasema wakala mwingine. 

Kama kuna usajili ambao umefikirisha wengi ni wa Fabio Silva  kutoka Porto kwenda Wolves. “Huo ni usajili bora zaidi kufanywa  na Jorge Mendes katika dirisha hili la usajili, kwani alipata malipo  ya pauni milioni7 kufanikisha dili hilo,” anasema wakala mmoja. 

Wakala mwingine anasema, “Suala sio usajili wenyewe, kwa  sababu sote tunajua kuna mkono mrefu wa ushirikiano hapo.  Lakini dau lenyewe. Linavutia mno,” 

Jina la Rhian Brewster nalo limetajwa kwenye kipengere cha  usajili mbovu. Ilidhaniwa Liverpool wangemtoa kwa mkopo,  lakini ameuzwa kwa pauni milioni 23.5. “Kuna hasara kidogo  kwenye masharti ya kuuzwa Brewster kwenda Sheffield United.  Lakini hasara hiyo ipo kwa mchezaji mwenyewe pia kujiunga timu  ambayo haijapata pointi tangu kuanza msimu huu,” anasema  wakala mmoja. 

4. Timu gani imefanya usajili bora? 

“Everton. Lakini Aston Villa na Leeds United zimefanya biashara  nzuri, na Totenham wamemaliza kwa uzuri zaidi. 

Usajili wa Chelsea umeleta hisia tofauti na mawakala wamezitaja  timu tano zenye usajili mzuri. Everton wamepata asilimia 33,  Aston Villa wamepata asilimia 22. Timu zote mbili zimetajwa  kuboresha vikosi vyao kimalengo kuliko zingine. 

Villa wamenunua Ollie Watkins, Matty Cash, Emiliano Martinez,  Bertrand Traore na Ross Barkley, inaonesha wamejifunza  kutokana na kile kilichotokea msimu uliopita, ambapo  walinusurika kushuka daraja. 

Kwa upande wa Everton, wamesajili Allan,James Rodriguez,  Abdoulaye Doucoure. “Everton na Spurs zinaonekana kuwa imara 

zaidi, huenda wakaimarika zaidi kuliko walivyoanza msimu.”  Anasema wakala mmoja 

Bale, Sergio Reguilon, Vinicius na Pierre-Emile Hojbjerg ni nyota  wapya waliotua Spurs. “Spurs wameziba mapengo mengi na  wamenunua wachezaji wenye uzoefu na njaa ya mafanikio”  anasema wakala mwingine 

Chelsea imetumia fedha nyingi baada ya kutoka kwenye kifungo  cha usajili. “Kwenye ulinzi, wanaonekana wana kasoro. Lakini  kuboresha safu ya ushambuliaji wameleta nyota wapya, ambao  wanachangia ugumu kwa wengine kupata namba kikosi cha  kwanza,” 

5. Ni klabu ipi imeboronga kwenye usajili? 

Bila kupepesa macho Manchester United imetajwa kuwa klabu  iliyoharibu zaidi kwenye dirisha usajili lililopita. Man United  imepata asilimia 32, ikifuatiwa na Burnley yenye asilimia 28 na  Fulham asilimia 20, kuwa klabu zilizoboronga kwenye usajili. 

“Man United wamemkosa chaguo lao la kwanza. Jadon Sancho,  ni hasara kubwa sana kwao. Man United sio kwa sababu ya nani  amesajiliwa bali kwa sababu wachezaji waliowataka  hawajawapata. Hilo ni jambo bay asana kwa namna fulani.  Inaashiria kushindwa kwa kocha Ole Gunna Solskjaer. Klabu  kubwa inatakiwa kutikisa soko la usajili,” wamesema mawakala  mbalimbali. 

Burnley haijasajili mchezaji yeyote, ikiwa na maana watarudi  nyuma zaidi badala ya kusonga mbele,” 

Si kwamba Burnley haijasajili yeyote, isipokuwa imewachukua  wachezaji ambao wanaonekana hawana lolote, kwa mfano Dale 

Stephens amenunuliwa kutoka Brighton na Will Norris  amenunuliwa kutoka Wolves, lakini tathmini inaonesha dirisha la  usajili lililopita kocha Sean Dyche, amefeli kuwasajili wachezaji  aliowataka kama vile Harry Wilson kutoka Liverpool na  imeonesha ni udhaifu wa timu hiyo kufanya biashara nzuri. 

Fulham imesajili wachezaji kadhaa lakini macho ya mawakala  yanasema nao wameboronga. West Ham wamemuuza Grady  Diangana kwenda West Brom, lakini mipango yao ya kusajili beki  wa kati imefeli. Majaribio yao yalikuwa kuwasajili kati ya Antonio  Rudiger, Fikayo Tomori au James Tarkowski yaligonga mwamba. 

6. Je, ugonjwa wa Corona umebadili soko la usajili? 

Takwimu zinaweza kuonesha klabu zimetumia pauni bilioni moja  na kuwa hali ileile katika soko la usajili na kwamba ugonjwa wa  Corona haujabadili lolote. 

“Chelsea wametumia bajeti kubwa na wametawala soko. Lakini  corona imebadili masuala ya fedha kabisa kwa sababu klabu  zilitegemea kutoka kwa wamiliki wao kusajili wachezaji. Idadi ya  wachezaji waliosajiliwa kwa mkopo inaeleza hali halisi kuwa timu  zimekosa fedha. Timu nyingi zimetumia mbinu ya pili au tatu  kuimarisha vikosi9 vtao. Hakuna iliyokuwa tayari kuwekeza fedha  nyingi kwenye manunuzi EPL, hali ambayo imezinufaisha timu  kubwa,” 

Mawakala wanasema “Mauzo ya wachezaji yamekuwa magumu.  Timu zimehangaika kuuza hata wachezaji isiowataka kwa sababu  suala la fedha lilikuwa gumu kwa klabu nyingi. Corona imebadili  mbinu za kuingia mikataba. Mawakala hawakuwa na nguvu na  klabu zilitumia ugonjwa huo kama kisingizio cha kukwepa kulipa  dau kubwa.”

Baadhi ya mawakala wameonesha picha kubwa, kutoka juu EPL  hadi chini, ambako ugonjwa wa corona umeathiri pakubwa soko  la wachezaji. 

“Mambo yamebadilika sana, hasa klabu za daraja la kwanza, ni  balaa kubwa, na zinasua sua kwa sasa. Mara nyingi habari za top  four au top six au EPL ndio zinabamba. Lakini timu zote  zinazokuwa kundi hilo zina madeni makubwa, biashara mbovu  nab ado zinatakiwa kufanya vizuri sokoni. Kwenye ligi za chini  wanazingatia namna ya kusonga mbele kupitia hali walizonazo. 

7. Ni usajili upi umefeli sasa na huenda ukatimia Januari? 

“Kijana mmoja aliyeumizwa na usajili ni Max Aarons. Ameivutia  klabu za Barcelona,lakin Norwich waligoma kufanya biashara kwa  sababu ya dau dogo. Barcelona wakaamua kumsajili Sergino Dest,  lakini kama Aarons atakuwa wiki nane au tisa nzuri, basi timu  nyingine inaweza kubisha hodi mlangoni kwao januari. 

Rudiger, anaweza kuondoka Chelsea ifikapo Januari, dili linaweza  kubadilika ikiwa atacheza mechi nyingi kwa miezi miwili ijayo.  Tarkowski anaweza kujiunga Leicester, na haitashangaza Jadon  Sancho akijiunga Man United. 

“Tetesi kuhusu Sancho zitarejea kwa kasi. Taarifa za ndani  zinasema anataka uhamisho mkubwa. Sina uhakika kama Man  United watafanikiwa kumsajili. Jadon Sancho kuhama Dortmund  ni suala linalowezekana lakini huenda likatimia zaidi dirisha  kubwa la usajili ujao. Ila huenda asjiunge Man United. 

Fikayo Tomori na Billy Gilmour wanaweza kuhama Chelsea  januari mwakani. Brandon Williams hataki kuwa beki wa kushoto  chaguo la tatu Man United, kiakili amejiandaa kuhama lakini sio  kujiunga timu kama Leeds au Southampton. 

8. Usajili gani unaangaliwa kwa kiasi kikubwa kuleta matunda? 

Hili lilikuwa swali gumu kwa mawakala kujibu. “Hakuna usajili  uliowekwa kwenye matazamio. Lakini hakuna aliyetegemea  Thomas Partey angeenda Arsenal, hilo linaweza kuwa kubwa  kwao” 

Ross Barkley umekuwa usajili maarufu Aston Villa akiwa na  asilimia 16 ya kura. Baadhi ya mawakala wameeleza kuwa usajili  huo wa mkopo wa msimu mmoja ni kurudi nyuma kwa sababu  haukutegemewa kuvutia wengi. 

“Zipo dalili usajili wake unaweza kuleta matunda, hasa baada ya  kucheza nafasi ya kiungo huru. Ross anatakiwa kuthibitisha  thamani yake.” 

“EBerechi Eze pale Crystal Palace atashangaza watu, na Gabriel  wa Arsenal atathibitisha kuwa na thamani iliyolipwa kwake”  anasema wakala mwingine 

Eze, pamoja na Timothy Castagna wa Leicester ni wachezaji  pekee waliotajw amara mbili zaidi ya Barkley. Majina mengine ni  mshambuliaji Raphinha aliyejiunga Leeds akitokea Rennes na  Ryan Fraser aliyehamia Newcastle kutoka Bournemouth. 

“Nafikiri Ryan Fraser kujiunga bure Newcastle ni usajili bomba.  Iwapo atakuwa fiti, atakuwa miongoni mwa wachezaji bora 10.  Klabu nyingi zilitaka kumsajili. Inaonekana alitaka kujiunga na  timu za Top six lakini ndoto yake haijafanikiwa.” 

9. kama ingewezekana kubatilisha usajili mmoja, ni upi ungezuia?

Kitu cha kwanza, hakuna anayefurahishwa na muundo wa sasa  ulivyo.  

“Iwe ndefu hadi machi au fupi ni muhimu kuwa na dirisha moja la  usajili. Ukizingatia kile kiichotokea sasa wakati wa corona, kuna  timu daraja la kwanza zinahitaji pauni 50,000 kulipia deni lakini  zinakosa. Nafikiri ilibidi kufanya mabadiliko. Pengine sio mwezi 

machi bali februari, hasa pale mchezaji anapoambiwa hayuko  kwenye mipango ya kocha. Mchezaji hana nafasi na anaishia  jukwaani, na hawezi kuhama hadi dirisha kubwa au dogo. Je  kwanini huyo asiondoke mapema mfanbo Novemba kama sio  sehemu ya mipango ya kocha?”  

Baadhi ya mawakala wamedai kuwa dirisha la usajili ni kama  biashara yenye vikwazo. Wengine wanaamini muundo wa sasa ni  mrefu mno huku timu zikiwa hazijafanya usajili wa maana.  

“watu wengi walichanganywa na siku ya kufungwa usajili Oktoba  5. Ni upuuzi huwezi kutoka EPL kwenda EFL sasa, wala kutoka  EFL kwenda EPL.” 

“soko sasa litatazama muundo wa usajili kwa jicho tofauti.  Hatujui lini mambo yatakuwa sawa baada ya ugonjwa. Timu  zinahitaji muda kutengamaa. Tatizo ni mfumo wa usajili  unachangia presha kubwa.” 

10. Ni kocha yupi atakuwa wa kwanza kupoteza kazi yake? 

“Wapo wawili, lakini mmoja amefanikiwa kwenda mbali kwa sasa.  Solskjaer anakabiliwa na presha kubvwa kwa sababu dirisha la  usajili halikwenda vizuri kwa upande wake. Lampard yuko  kwenye presha kubwa pale Chelsea. Kuna kijana mmoja hana kazi  kwa sasa, na huenda akachukua ya moja. Ni Mauricio Pochettino.

Lampard na Ole Gunnar wame[ata asilimia 32 ya makocha ambao  wanaweza kufukuzwa wakati wowote. mwingine ni Scott Parker wa Fulham amepata asilimia 40. Sean Dyche naye amepata  asilimia 12. Wengine ni Slaven Bilic, Chris Wilder na Graham  Potter. 

11. nani atanyakua taji la EPL? 

“Wiki iliyopita ilikuwa na maajabu, lakini bado naamini Liverpool  watachukua ubingwa. Wanafahamu namna ya kurekebisha  mambo, wana wachezaji mahiri, kocha mwenye uwezo wa  kupindua matokeo Juregn Klopp. Manchester City, Man United,  Chelsea zina matatizo yao, lakini Everton haiwezi kushindana na  Liverpool” wamesema mawakala hao. 

Mawakala wengi wameonesha kushangazwa na ki[pigo cha mabao  7-2 ilicho[pata Liverpool kutoka kwaAston Villa. Lakini Liverpool  wamepata asilimia 68 ya timu yenye uwezo wa kunyakua  ubingwa. 

12. Timu zipi zitamaliza nafasi nne za juu? 

Kuna timu 7 zinazopigania kumaliza nafasi nne za juu. Everton imepata asilimia 16 na inatajwa kuwa na maendeleo mazuri na  huenda ikaonesha maajabu. 

Manchester City na Liverpool zinaongoza. Chelsea (72%), Spurs  (67%). Manchester United, wamepata asilimia ndogo kuliko  Everton. 

13. Nani atashuka daraja?

Fulham, West Bwom,Leeds United, Burnley, Sheffield United,  Brighton ni miongoni mwa timu zinazotajwa hunda zikashuka  daraja msimu huu na kwedna kushiriki EFL. 

14. Je, mawakala wanalipwa fedha nyingi kuliko kazi halis? 

“Namna tunavyolipwa fedha zetu imepotoshwa kwenye vyombo  vya habari. Mashabiki hawaelewi nini tunachofanya. Tunafanya  kazi ya kuwasaidia wachezaji na kusapoti familia zao. Tunafanya  kila kitu kwaajili yao, sio suala la kuingia mkataba tu. Tupo  kwaajili ya wachezaji kusaidia namna ya kuingia mikataba, nasi  tunalipwa. Mengi yanayosemwa ni kupotosha msingi wa  wachezaji kuwa na wakala wake. Wachezaji wanahitaji wakala.  Ingawa tunakubali kuwa wapo mawakala wabaya wanaharibu kazi  zetu,” wameeleza baadhi ya mawakala.  

“Kama unafikiria kiasi cha fedha anacholipwa Mino Raiola,  inabidi usahau. Watu wanapoongelea gharama za nyumba  England, hawazungumzia asilimia 0.01 ya nyumba kama Mayfair  ambazo zinauzwa pauni milioni 20. Wanaongelea nyumba za bei  nafuu, na kuna kazi wakala anakuwa ameifanya kuhakikisha  mchezaji wake anafanikisha kila kitu bila mizengwe.  

15. Je, ni sahihi mawakala kulipwa na pande nyingi? 

Gary Lineker aliandika Twitter akishauri ni wakati wa FIFA  kuwazuia mawakala kulipwa fedha na pande nyingi kwenye dili la  usajili. Nyota huyo wa zamani wa England anasema mawakala  wanapaswa kulipwa na wachezaji wao ambao ndio wateja husika  kwenye dili. 

“Kuna matatizo mengi. Kama una timu ya daraja la kwanza  inamtaka mchezaji wako ambaye hataki kulipwa mshahara chini  ya pauni 2500, lakini unatumia wiki kadhaa kumshawishi 

mchezaji kuwa ni fursa sahihi, hiyo ni kazi ngumu sana, kisha  unatakiwa kuzungumza na uongozi wa timu pamoja na pande  zingine. Kuna wakati wakala analipwa kwa niaba ya klabu na  mchezaji, haina maana kuwa anapokea fedha hizo kama za kwake,  bali wapo wahusika wanaotakiwa kupewa.” 

“Uwakilishi pacha umefutwa na FA, ukaidhinishwa na HMRC na  inawanufaisha wachezaji kwa kiai fulani kuhusu masuala ya kodi.  Inaokoa fedha za klabu pia.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Arsène Wenger

Wenger: Nasoma yanayonisaidia kuwaelewa binadamu

Tanzania Sports

Usajili Wa Kaze Watakata Yanga