in , ,

Mambo muhimu kwenye mechi ya YANGA na SIMBA

1: Hapana shaka ule wimbo wa “U-underdog” wa Simba kwenye mechi za ligi ya mabingwa barani Afrika unahamia kwa Yanga Leo. Hii inaweza silaha kwa Yanga kumuua Simba anayejiamini zaidi.

2: Mechi ya Al Alhy imewafanya Simba wajiamini sana, na ikawafanya Yanga waonekane waoga sana. Ila kuna kitu ambacho unatakiwa kukifahamu, mechi kama hizi huwa haziangalii kiwango chako kikoje kwa sasa.

3: Andrew Vincent ndiye anayebeba udhaifu mkubwa wa Yanga, aina yake ya uchezaji wa kushuka mpaka chini katikati huwafanya Yanga wawe na uwazi eneo lao la nyuma. Uwazi ambao ukitumiwa vizuri inaweza ikawa na madhara makubwa kwa Yanga.

4: Simba bado ina madhaifu katika safu yao ya ulinzi na ndiyo sehemu ambayo Yanga wanatakiwa kuitumia vizuri kwa ajili ya kuwaadhibu Simba.

5: Hapana shaka kwa sasa hakuna safu imara ya ushambuliaji kama ya Simba inayoundwa na Meddie Kagere, John Bocco na Emmanuel Okwi na hapa ndipo mtihani wa kwanza wa Yanga unapoanzia.

6: Huwezi kuizuia Simba kumiliki mpira na Yanga hawatakiwi kuingia kwenye mchezo huu kwa ajili ya kushindana na Simba jinsi ya kumiliki mpira, cha muhimu ni wao kufikiria namna ambavyo wajalinda bila madhara.

7: Ni aina gani ya mbinu ambayo Yanga wanatakiwa kuitumia wakati wanajilinda kwa kukaa nyuma ya mpira?, bila shaka ni mashambulizi ya kushitukiza. Kitu hiki kitaisaidia sana Yanga kwa sababu Simba watakuwa wanaacha uwazi nyuma kutokana na kupanda sana mbele.

8: Ramadhani Kabwili ndiye anayetegemewa kuilinda leo hii Yanga. Ni mechi kubwa kwake lakini ndiyo mechi ambayo anatakiwa kufikiria namna ambavyo anaweza kuwasahaurisha mashabiki wa Yanga kuhusu Beno Kakolanya.

9: Uwezekano wa Makambo na Amis Tambwe kucheza kwa pamoja kutawapa nafasi kubwa ya Yanga kushinda hii mechi kwa sababu hawa ni wafungaji mahiri, pili hawa wana nafasi kubwa ya kuifanya timu Iwe na njia mbadala mfano kutumia mipira ya juu.

10: Mabeki wa Simba wa pembeni mara nyingi huwa wanapanda juu na kufanya kuwe na uwazi eneo la nyuma. Kitu hiki kinaweza kuwa na madhara kwa Simba kama wakishindwa kukiangalia vizuri kama Yanga wakiamua kutumia uwazi wa pembeni kuwaadhibu Simba.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Tanzia kwa kipa hodari Gordon Banks

Tanzania Sports

Paul Godfrey katusahaulisha Juma Abdul