in , ,

MAMBO MATANO YALIYOOKOA KAZI YA MOURINHO

Jana ile sura ya Sir Alex Ferguson ilionekana kwenye timu ya Jose Mourinho. Manchester United walikuwa nyuma ya magoli 5 kipindi cha kwanza, lakini kipindi cha pili waliingia na kushinda mechi kwa magoli 3-2.

Ipi ilikuwa silaha kubwa ya Manchester United katika mechi ya jana?

1: Kwa mara ya kwanza Jose Mourinho aliamua kuchezesha wachezaji watano kwa pamoja wenye asili ya kushambulia (Anthony Martial, Alexis Sanchez, Romelu Lukaku, Paul Pogba na Juan Mata).

Hii iliifanya timu iwe juu muda mrefu na kizuri zaidi aliwafanya wachezaji hawa huko mbele wawe huru zaidi. Tumezoea kuona mbinu za Jose Mourinho akiifanya timu yake iwe ngumu na iwe inajilinda kwa asilimia kubwa, lakini jana wachezaji walikuwa huru na hii iliwasaidia sana kutengeneza uwazi ambao uliwasaidia kupata nafasi za kufunga.

2: Mabadiliko ya kutoka Eric Bailly na kuingia Juan Mata yalikuwa na faida ipi kwa Manchester United?

Manchester United kabla hajaingia Juan Mata, walikuwa wanakosa ubunifu katika eneo la mbele. Hawakuwa na mtu ambaye anaweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga. Hivo baada ya Eric Baily kutoka na kuingia Juan Mata, kuliongezeka ubunifu katika eneo la mbele la Manchester United.

3: Pogba wa jana ndiye Paul Pogba anayeliliwa kila siku arudi?.

Bila shaka ndiyo huyo na alikuwa na msaada mkubwa sana katika mechi ya jana. Kwanini ?. Pamoja na kwamba alitoa pasi ya mwisho ya goli lakini alikuwa na msaada mkubwa kuifanya timu iwe juu muda mrefu wa mchezo na hii ilichangiwa kwa kiasi kikubwa kwa yeye kucheza huru eneo la juu. Kitu ambacho amekuwa akililia muda mrefu na jana alipata nafasi hiyo na kuibeba timu yake.

4: Anthony Martial.
Jana ilikuwa siku nzuri kwake ingawa kipindi cha kwanza hakuanza vizuri sana, kipindi cha pili kilikuwa kizuri kwake na alifanikiwa kufunga goli moja kati ya magoli matatu. Kasi yake ilikuwa muhimu sana katika eneo la juu la Manchester United.

5: Alexis Sanchez alikuwa anasubiriwa kwa muda mrefu arudi, amekuwa na mwanzo usio mzuri katika ligi. Tangu aje Manchester United mwezi January mwaka jana huku kukiwa na mategemeo makubwa kuwa atafanya vizuri lakini jana ndiyo alifunga goli 4 tangu ajiunge na Manchester United. Alipoingia kuchukua nafasi ya Marcus Rashford, alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuongeza kasi katika eneo la mbele, kasi ambayo ilikuwa inasaidia kutengeneza uwazi katika eneo la nyuma la Newcastle United.

MWISHO:

Natamani kujua kipi ambacho Jose Mourinho alienda kuongea na wachezaji wake katika vyumba vya kubadilishia nguo. Ile hali ya kupigana kwa nguvu ndiyo tamaduni ya Manchester United kwa muda mrefu. Na ndiyo iloyookoa pia kibarua cha Jose Mourinho. Kama Jose Mourinho atafanikiwa Kuitunza hiyo hali ya kupigana atakuwa na nafasi kubwa sana ya kumaliza msimu huu akiwa na Manchester United.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

LIONEL MESSI, HADITHI ISIYO KUFA

Tanzania Sports

Hata tukimuondoa Aussems, Simba SC anayefuata atamlaumu tu Masoud Djuma