in ,

Mambo matano niliyojifunza kwenye ushindi wa Arsenal

Jana kocha wa muda wa Manchester United, Ole Gunnar alipokea kipigo chake cha kwanza katika michuano ya ligi kuu ya England.

Arsenal waliifunga Manchester United katika uwanja wao wa nyumbani, Emirates na kuwafanya waende michezo 9 bila kufungwa katika uwanja wao wa nyumbani katika ligi kuu ya England.

Kipi ambacho nimejifunza kutoka kwenye mechi hii ?

1: Ozil siyo aina ya wachezaji wa Unai

Baada ya kuwekwa benchi muda mrefu, Mesut Ozil kwa siku za hivi karibuni amekuwa akipewa nafasi na Unai Emery.

Na jana alipewa nafasi katika mechi kubwa dhidi ya Manchester United. Lakini kuna kitu kimoja tu ambacho kinamfanya Ozil kuonekana siyo aina ya wachezaji wa Unai Emery.

Unai Emery anataka timu yake ifanye vitu viwili (Possession na Pressing). Mesut Ozil ana uwezo wa kumiliki mpira na kutoa pasi vizuri lakini kitu ambacho kinakosekana kwake ni pale timu inapotakiwa kufanya pressing.

Hiki ndicho kinamuumiza Mesut Ozil katika kikosi cha Unai Emery, anaonekana hana msaada mkubwa sana kipindi timu inapokuwa inatakiwa kufanya pressing.

2: Aubameyang na Laccazette, mmoja ni bastola mwingine ni risasi.

Kwa pamoja wanakamilisha uhatari wa safu ya ushambuliaji ya Arsenal. Baada ya Unai Emery kufungwa na Manchester United 3-1 kwenye michuano ya FA.

Aliamua kubadilisha kwa kutowachezesha wote wawili, lakini amekuja kujaribu kuwachezesha wote wawili katika mchezo wa jana na wote kwa pamoja wameonesha jinsi ambavyo timu inakuwa na nguvu wakicheza kwa pamoja.

Kuna wakati Laccazette hushuka chini kuchukua mipira katikati, anaposhuka chini hushuka na Beki mmoja wa kati ambaye husababisha uwazi eneo la nyuma.

Uwazi ambao hutumiwa na Aubameyang. Hata penalti ya Jana ilisababishwa na Laccazette na Aubameyang kuifunga.

3: Leno taratibu anajijengenea ufalme wake.

Anatokea nchi ambayo ina sifa kubwa ya kuzalisha magolikipa imara, Ujerumani. Huu ni msimu wake wa kwanza katika ligi kuu ya England akiwa na Arsenal.

Na taratibu ameanza kuwa mhimili mkubwa kwenye kikosi cha Arsenal. Jana amefanya saves ambazo zimeiweka hai klabu ya Arsenal.

4: Lukaku alijaribu kutukumbusha kuwa ni yeye.

Tangu aje Ole Gunnar moja ya wachezaji ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa na mchezo mzuri ni Lukaku.

Lakini kwa bahati mbaya jana alikuwa na mchezo mbaya. Alikosa nafasi mbili za wazi. Nafasi ambazo kama angezifunga zilikuwa zinaisaidia Manchester United kurudi mchezoni.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

PSG walikitupa kitabu walichopewa na Barcelona

Tanzania Sports

Zidane anapenda masika sana kuliko kiangazi