in

Makocha wanaowindwa Manchester United 

Kuthibitishwa habari za kufukuzwa Ole Gunnar Solskjaer ni tangazo la kwamba nafasi ya kazi  ipo Old Traford. Na sasa Manchester United wapo katika msako wa kocha mpya ambaye  atakiongoza kikosi hicho katika mafanikio zaidi. Tangu aondoke gwiji wao Sir Alex Ferguson  hakuna kocha aliyeleta mafanikio klabuni hapo, na wengi wao wanaishi kufukuzwa. Hata hivyo  sifa ya Man United ni kuwavumilia zaidi makocha wake.  

Kwa namna ambavyo Ole alivyoboronga ilitarajiwa angefukuzwa mapema sana, lakini badala  yake akaongezewa mkataba wa kubaki klabuni hapo. Muda aliopewa na kile kilichotokea ni vitu  viwili tofauti, ambavyo vinawafanya mashabiki wawe na hasira na kuona waziwazi kocha wao  huyo hakuwa na umahiri kuinoa klabu hiyo. Kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Watford  kilihitimisha kibarua cha kocha Ole Gunnar Solskjaer ambapo s asa wapo makocha watano  wanaowindwa na mabosi wa Man United ili wakubali ofa za kuinoa timu hiyo.  

ZINEDINE ZIDANE 

Tanzania Sports
Mauricio Pochettino na ZZ

Ni raia wa Ufaransa. Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid hana kibarua tanu Mei mwaka huu  alipojiuzulu nafasi ya ukocha kwa mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi ya Mbaingwa Ulaya na La  Liga. Zidane anahusishwa na Man United kwa sababu anazo sifa kubwa ambazo zinahitajika Old  Traford. Mafanikio yake akiwa Real Madrid ndiyo yanawavutia mabosi wa Man United. 

Ametwaa mataji mawili ya La Liga, mawili Supercopa de Espana, mawili ya UEFA Super cup na  mawili ya klabu bingwa dunia. na zaidi anametaa mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.  Kwahiyo ni kocha mwenye uzoefu wa mashindano mbalimbali barani ulaya kuanzia ligi za ndani  hadi kimataifa. Taarifa zaidi zinasema uwezekano wa kumpa Zidane ni mdogo kwa sababu hana  mpango huo kwa sasa na familia yake inatajwa kuweka ngumu kuishi England. 

BRENDAN RODGERS 

Huyu ni raia wa Ireland kaskazini ambaye kwa sasa anaifundisha Leicester City, na amewahi  kuzinoa timu za Swansea City,Liverpool na Celtic. Anapendwa na mashabiki na wachezaji wengi  kutokana na kazi yake, na ameiongoza Leicester kutwaa mataji mawili ya Ngao ya Hisani na FA.  Pia alikiongoza kikosi hicho msimu uliopita kumaliza Ligi ikiwa nafasi ya tano ambayo  iliwawezesha kushiriki michuano ya Europa League. Uwezekano wa kumpata kocha huyo ni  mkubwa ikiwa mabosi wa Man United watalipa gharama za kuvunja mkataba wake na Leicester.  

MICHAEL CARRICK 

Nyota huyu wa zamani naye ni miongoni mwa wanaotajw akuchukua nafasi ya ukocha Man  United. Kwa sasa anapewa jukumu la kukiongoza kikosi hicho kwa muda hadi pale atakapotangazwa kocha mkuu. Kiungo huyo atakuwa na kibarua cha kuongoza Man United  katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Villareal. Kama Carrick atapata matokeo  mazuri huenda akafikiriwa kuchukua mkataba wa kudumu wa kuinoa Manchester United. Kwakuwa anaifahamu kalbu hiyo na akiwa kocha msaidizi inampa nafasi ya kurithi mikoba ya  Ole Gunnar.

ERIK TEN HAG 

Kocha huyo wa Ajax Amsterdam naye amekuwa miongoni mwa wanaohusishwa na kibarua cha  kuinoa Man United. Hag amekuwa kocha wa Ajaz tangu mwaka 2017, akisifika kufundisha soka  la burudani na ushindi ambalo limempa mataji mawili ya Ligi Kuu Uholanzi, pamoja na  kukiongoza kikosi hicho hadi nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita. Kumshawishi  kocha huyu si suala dogo kwa sababu presha za Ajax na Man United zinatofautiana. Akiwa  ametulia Ajax na kutengeneza falsafa yake iliyohitaji muda hadi kuleta mafanikio, haifahamiki  kama mabosi wa Man United watamvulia hadi kuunda falsafa yake Olkd Traford na changamoto  ya kufanya kazi na wachezaji wakubwa. 

LAURENT BLANC 

Mfaransa huyu amewahi kuwa kuichezea Man United mwaka 2003. Alikuwa beki mahiri wakati  akicheza soka. amewahi kumkochi Edinson Cavani alipokuwa kocha wa PSG ambako walitwaa  mataji matatu ya Ligi Kuu Ufaransa. Kwa sasa anafanya kazi kama kocha wa Al Rayyan nchini  Qatar. Blanc amewahi kuiongoza klabu ya Bordeaux kutwaa taji la Ligi Kuu Ufaransa mwaka  2009 na alikuwa kocha wa timu ya taifa baada ya fainali za Kombe la dunia mwaka 2010. 

MAURICIO POCHETTINO 

Ni miongoni mwa makocha wanaotawa kuwa tayari kuchukua kibarua cha Man United.  Pochettino kwa sasa ni kocha wa PSG, lakini anahusishwa na kibarua hicho kwa sababu familia  yake yote iko jijini London, wakati yeye akiwa Paris. Ana uwezo wa kuwaongoza wachezaji  wakubwa kwa sasa ambako yuko na Lionel Messi, Neymar,Kylian Mbappe na wengineo ndani ya  PSG hivyo huenda kawa mtu sahihi kupokea jahazi la Man United.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Brendan Rodgers

Brendan Rodgers ni wakati wake sasa  

Tanzania Sports

Fahamu mambo muhimu Kombe la Dunia 2022