in , , ,

MAKOCHA 32 KUSHIRIKI KOZI YA FIFA COPA COCA-COLA

Makocha 32 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani wanashiriki kozi ya
Copa Coca-Cola inayoanza kesho (Agosti 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam
chini ya Mkufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa
Miguu (FIFA).

Kozi hiyo itakayomalizika Agosti 17 mwaka huu itafunguliwa saa 3 kamili
asubuhi kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre na washiriki wote tayari
wameshawasili Dar es Salaam. Mkufunzi wa kozi hiyo ni Govinder Thondoo
kutoka Mauritius.

Washiriki wa kozi hiyo ni Ahazi Ibrahim Kasegese (Mbeya), Aloyce Mayombo
(Pwani), Andrew Zoma (Tabora), Asuri Msakamali (Simiyu), Bakari Khamis
Kilambo (Kaskazini Pemba), Chacha Sambulo (Mara), Charles Rwezaura
(Kagera), Daniel Sambala (Njombe), Dudu Haruni (Iringa) na Emmanuel
Kapurata (Rukwa).

Faki Makame Haji (Kaskazini Unguja), Fatawi Khamis Sheha (Kusini Pemba),
Hamisi Omary Mabo (Kigoma), Hussein Maulid (Morogoro), Issa Lugaza
(Kilimanjaro), James Gaspar (Shinyanga), James Wambura (Arusha), Jomo
Jackson Puccey (Lindi), Joseph Sihaba (Dodoma), Kelvin Haule (Ruvuma) na
Kessy Juma Abdallah (Tanga).

Kessy Mziray (Mwanza), Menswi Mchwampaka (Kinondoni), Mohamed Abdallah
Kweka (Singida), Nurdin Gogola (Temeke), Pius Kamande (Rukwa), Ramadhan
Abrahman Ramadhan (Mjini Magharibi), Ramadhan Salum Mnyoti (Manyara),
Raphael Ngeleja (Geita), Samuel Edgar Maokola (Ilala), Shaweji Nawanda
(Mtwara) na Vuai Abdul Haji (Kusini Unguja).

Fainali za U15 Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa zitafanyika Septemba mwaka huu
jijini Dar es Salaam.

* *

*SEMINA YA MAKAMISHNA YAANZA DAR, MWANZA*

Semina kwa ajili ya makamishna wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja
la Kwanza (FDL) pamoja na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness
test) kwa waamuzi wote wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka kuchezesha
VPL msimu wa 2013/2014 vinaanza kesho (Agosti 12 mwaka huu) katika vituo
vya Dar es Salaam na Mwanza.

Mafunzo hayo yatakayomalizika Agosti 14 mwaka huu yatakuwa chini ya
wakufunzi Leslie Liunda, Joan Minja na Riziki Majara kwa kituo cha Dar es
Salaam wakati kituo cha Mwanza kitakuwa na Alfred Rwiza na Omari Kasinde.

Kwa Dar es Salaam mafunzo yatafanyika Uwanja wa Taifa wakati Mwanza itakuwa
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Kituo cha Mwanza kitakuwa na makamishna na waamuzi kutoka mikoa ya Geita,
Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida
na Tabora.

* *

Kituo cha Dar es Salaam kitahusisha waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya
Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro,
Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.

* *

Washiriki wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo,
na si vinginevyo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Arsenal wawanyuka Manchester City

Manchester United Ngao ya Jamii