in ,

Magufuli ameng’arisha sekta ya michezo

JPM

Nchi yetu imempoteza rais John Magufuli kutokana na maradhi ya moyo. Tangazo la kifo lilitolewa na Makamu Samia Suluhu mnamo Machi 17, ambapo alisema, “Tumepoteza kiongozi wetu shupavu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli, alilazwa tarehe 6 Machi mwaka huu katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo la mfumo wa umeme ambalo alikuwa nalo kwa zaidi ya miaka 10.

“Rais Magufuli amefariki kwa maradhi ya moyo katika Hospitali ya Mzena. Alilazwa Machi 6 mwaka 2021 katika Hospitali ya Jakaya Kikwete na kuruhusiwa Machi 7 na kuendelea na majukumu yake. Machi 14 alijisikia vibaya na akarudi Hospitali ya Mzena ambapo aliendelea na matibabu hadi umauti unamkuta. Nchi yetu itakuwa na maombolezo ya siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti,”

Je ni mambo gani yaliyotokea katika  michezo wakati wa utawala wa Rais Magufuli?

Kwanza, kwa mara ya kwanza Tanzania ilifanikiwa kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizofanyika nchini Misri mwaka 2019. Taifa Stars ilikuwa chini ya kocha raia wa Nigeria, Emmanuel Amunike. Kwenye fainali hizo Taifa Stas ilipangwa kundi C pamoja na Senegal, Algeria na Kenya.

Pili, Tanzania ilifanikiwa kufuzu kwa mara ya pili kushiriki fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani maarufu kama CHAN yaliyofanyika nchini Cameroon. Kikosi cha Taifa Stars kikiwa chini ya kocha Ettiene Ndayiragile kiling’ara katika uongozi wa Magufuli.

Kwenye CHAN Tanzania ilichapwa mabao 2-0 na Zambia kabla ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namibia lililofungwa na winga Farid Mussa Shah. 

Ndayiragile alichukua nafasi ya ukocha kutoka kwa Emmanuel Amunike ambaye aliiongoza Taifa Stars kufuzu na kushiriki mashindano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2019. 

Tatu, kuibuka kwa Namungo FC ya mkoani Lindi na kucheza vizuri mashindano ya Kombe la Shirikisho la CAF kwa mara kwanza na kufuzu hatua ya makundi. 

Timu hiyo kwa jina la utani wanaitwa Southern Killers na wamepangwa Kundi D ambalo linajumuisha Namungo FC, Raja Casablanca (Morocco), Nkana Rangers (Zambia) na Pyramid (Misri). 

Katika mchezo wa kwanza mjini Rabat, nchini Moroco klabu ya Namungo ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wneyeji wao Raja Casablanca. Mchezo wa pili uliofanyika jijini Dar es salaam, Namungo walikubali kipigo cha mabao 2-0. Hata hivyo mafanikio yao hadi sasa si haba na hawana cha kupoteza zaidi ya kujifunza na kupata uzoefu.

Tatu, timu ya taifa ya wanawake imekuwa na mafanikio makubwa. Mwaka 2016 walitwaa kombe la CECAFA chini ya makocha Bakari Shime na Edna Lema nchini Uganda. Mwaka 2018 walitwaa kombe hilo nchini Rwanda. Mwaka 2018 tena walitwaa ubingwa wa Afrika mashariki katika mashindano yaliyofanyika nchini Burundi. Mwaka 2019 walitwaa taji la COSAFA Chini ya miaka 20 wanawake lililofanyika nchini Afrika kusini. Mwaka 2020 timu ya taifa ya wanawake chini ya miaka 17 walitwaa taji la COSAFA kwa wanawake kwenye mashindano yaliyofayika nchini Afrika kusini

Nne, mashindano ya Ndondi yameibuka upya na kuwaibua wanamasumbwi wengi wapya. Chini ya utawala wa Magufuli ndipo mchezo wa ndondi umerejesha heshima yake kwenye sekta nzima ya michezo. Mabondia kama vile Twaha Kiduku,Dulla Mbabe Hassan Mwakinyo kwa kuwataja wachache wameibuka na kuwakilisha vizuri mchezo wa ndoa katika kipindi cha uongozi wa Magufuli. 

Tano, mafanikio makubwa ya klabu ya Simba aymejitokeza katika kipindi cha urais wa John Magufuli. Simba imekuwa ikinguruma katika soka barani Afrika, ambako sasa imekuwa kinara wa Ligi ya Mabingwa Afrika kudini A huku wakiwa na sifa ya kuichabanga bingwa mtetezi wa Ligi hiyo Al Ahly. 

Simba imeweka rekodi mbalimbali katika utawala wa John Magufuli kwa kuwa klabu ya kwanza kushinda katika mashindano nchini Nigeria, pamoja na kuzichapa timu zote zilizocheza kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Simba wanguruma Ligi ya Mabingwa Afrika

DITRAM NCHIMBI

UKISHANGAA YA DITRAM NCHIMBI UTAYAONA YA FREDDY ADDU