in , ,

Madrid wababe wa Barcelona

Madrid wababe wa Barcelona

*Jose Mourinho aangukia pua kwa Wolverhampton

*Man City mabingwa Carabao, Samatta apiga bao

Wakati Real Madrid wamefanya kile ambacho hakikutarajiwa kwa kuachapa mahasimu waop – Barcelona 2-0, Jose Mourinho ameanza kuonja shubiri baada ya kupoteza mechi kwa Wolverhampton.

Kwenye Ligi Kuu ya Hispania – La Liga, wababe wa Santioago Bernabeu walifanya kweli, wakionesha dhamira ya kuchukua ubingwa msimu huu, kwani baada ya ushindi huo wamekwea kileleni, wakifikisha alama 56 baada ya mechi26, wakiwa mbele yya Barca kwa alama moja.

Ilikuwa El Clasico nzuri ambapo chipukizi Vinicius Junior alifunga baada ya mpira uliokuwa umekengeuka njia, tena baada ya Isco kushuhudia jitihada zake za kufunga bao zikishindwa kwa kuokolewa kwenye mstari wa goli.

Walicheza kwa raha zao wakiwa nyumbani na Karim Benzema alikosa bao akipiga mpira juu huku Martin Braithwaite akikaribia kuwafungia Barca muda mfupi kabla Vinicius hajawaamsha vitini washabiki wa Madrid. Mariano aliyeingia kipindi cha pili alihakikisha ushindi kwa kupachika bao, ikiwa ni mechi yake ya kwanza msimu huu chini ya kocha Zinedine Zidane.

Real walimaliza wa tatu msimu uliopita, wakiwa alama 19 nyuma ya Barcelona, lakini sasa wanajenga mazingira ya ushindani hasa wakati ambapo watani wao wa jijini Madrid – Atletico Madrid, wakiwa na hali ngumu.

Walikuwa wametoka kufungwa na Manchester City 2-1 kwenye mechi ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) hatua ya 16 bora na watarudiana Etihad, England baadaye mwezi huu. Ni mara ya kwanza kuwafunga Barca katika mechi nane sasa za lifi. Kocha wa Barca, Quique Setien aliwasili akijiamini, kwani alikuwa ameshinda mechi nne mfululizo kabla, lakini akaumbuliwa.

Nchini England, Tottenham Hotspur walipigwa nyumani mabao 3-2 na Wolves, Mourinho akisema kwamba hawezi kukumbuka mara ya mwisho wachezaji wake walipocheza vyema. Wamefungwa wakiwa hawana mshambuliaji mzoefu wa asili, baada ya nahodha wao Harry Kane kuumia.

Katikia mechi nyingine ya EPL, Manchester United walikwenda sare ya 1-1 na Everton, baada ya utata wa Kocha Msaidizi wa Video (VAR) kuwanyima Everton bao ambalo lingekuwa la ushindi. Kocha wa Everton, Carlo Ancelotti alitolewa nje na mwamuzi.

Kwingineko, Manchester City walitwaa ubingwa wa Kombe la Ligi – Carabao, baada ya kuwafunga Aston Villa 2-1. Walitangulia kufunga kupitia kwa Sergio Aguero na Rodri, ikiwa ni msimu wa tatu mfululizo wanachukua kombe hilo dogo.

Mtanzania Mbwana Samatta aling’ara na alitundika kambani bao zuri la kichwa baada ya hayo mawili ya Man City ambao kiujumla walicheza vyema. Anakuwa Mtanzania wa kwanza kufunga kwenye fanali za aina hiyo.

Kadhalika, anakuwa mchezaji wa tano tu kutoka Afrika kufunga kwenye fainali ya Kombe la Ligi baada ya Didier Drogba , Joseph-Desire Job, Obafemi Martins na Yaya Toure, akiing’arisha zaidi nyota yake baada ya kuwa Mtanzania wa kwanza kusajiliwa na kucheza kwenye EPL.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Watford wamewazuia ‘Liver’ kuifikia rekodi ya Arsenal

Tanzania Sports

Chama ndiye Mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Simba