in

Mabadiliko ya kiutendaji yaja Yanga..

Wachezaji wa Yanga

Yanga wanatarajia kufanya mabadiliko ya timu ili iende kisasa zaidi ambapo kwa kuanza wamempata Senzo Mbatha kuishauri na kuunganisha baina ya timu hiyo na watu wa La Liga.

Kwa mujibu wa mmoja ya watu wa GSM Eng. Hersi Said ambao ni wawekezaji ameweka wazi muundo wa timu, tayari wameuandika na wamempa Senzo ili aweze kushauri namna gani mambo yaende.

Hii itasaidia kuweka sawa katika kila kitengo kilichopo ndani ya timu hiyo ambapo kwa uzoefu wake anaweza kuweka sehemu nzuri kimaendeleo.

Huko kote nazunguka tu kikubwa juu ya mgongano wa taarifa katika Idara ya Habari na Mawasiliano.

Naomba niwakumbushe kwanza tangu kitengo hiki kilipoingia madarakani ambacho kimetoa watu wawili, mmoja wapo ni Mkuu wa Kitengo cha Habari ambaye ni Hassan Bumbuli mwingine Afisa Mhamasishaji na Msemaji Antonio Nugaz.

Wazo lao ni zuri mno na kila kitu huwa kinakuwa na muanzilishi wa jambo likiwa zuri linaendelezwa.

Kabla sijasahu kitengo cha Habari huko kwa wenzetu duniani huwa kinaingiza pato kubwa ndani ya timu, ikiwemo kutumia ‘Platform’ zao Instagram, Twiter, You tube na Facebook.

Turudi kwa Yanga, je kweli hili wanalifanya? majibu yake ni kwamba wameanza kujaribu na tumeona mabadiliko wameanzisha  tovuti, ‘Application’ ambayo unaipakua na kutengeneza pesa, wameendeleza kuboresha Jarida ambalo limetoka mara moja huku wakiifanyia kazi Yanga TV.

Senzo
Senzo

Hayo ya upande wa Hassan Bumbuli ambaye ndio mkuu wa kitengo cha Habari naamini amefanya vizuri pia ila bado anatakiwa ajitahidi zaidi.

Upande wa Nugaz yeye mapato ya jezi msimu uliopita ndio zimeuzwa sana huenda kuliko timu yoyote hapa Tanzania, aliweza kuongeza mvuto wa mashabiki wa Yanga kuingia uwanjani tofuati na walivyokuwa hapo awali msimu wa Mwinyi Zahera.

Naye anatakiwa ajitahidi zaidi msimu huu ili aweze kufikia malengo zaidi ya hapo katika mabadiliko ndani ya timu hiyo.

LUGHA GONGANA BUMBULI DHIDI YA NUGAZ

Turejee katika taarifa mbali mbali za  timu hiyo pindi zinapotoka na mkanganyiko wake.

Taarifa za usajili wa wachezaji wa ndani imeonekana dhahiri kabisa Hassan Bumbuli alizijua kwa makini sana hii inawezekana kutokana ukaribu wake na uongozi, Mara zote usajili wa ndani Hassan Bumbuli hakuwa anasitasita kuzisema.

Usajili wa wachezaji wa nje imeonekana kabisa Nugaz alijua kila wakati alipokuwa anafanya mahojiano na Wasafi TV kabla hata mchezaji yoyote kufika alijua zile  ‘Attempt’ zilizofanywa na GSM na alisema wazi kuwa kuna maeneo wataenda kusajili aliyataja, Afrika Kusini, Rwanda, Burkina Faso, Misri, Angola pamoja na Kongo.

Katika sehemu hizo alizozitaja tumeona Kongo, Angola na Burkina Faso mambo yametiki.

Ushirikiano wao kikazi una maswali mengi
Watendaji wa Yanga

Lakini angalia habari za ujio wa Yacouba Sogne yeye hakuweza kutaja siku ya kumpokea ila taarifa zilipotoka na baadae yeye kuitolea ufafanuzi.

Akisema kabisa kuwa taarifa zilizotoka hazina ukweli wakati huo taarifa hizo zimetoka kwa Mwakalebela ambae ni Makamu Mwenyekiti, pamoja na Bumbuli ambaye ndio mkuu wa kitengo cha Habari.

Unajiuliza kweli wanawasiliana katika kutoa taarifa  au kuna mkanganyiko ndani yake?

Licha ya hayo hapo awali kulikuwa na mfarakano ndani ya timu juu ya utoaji wa taarifa.

Nafikiri wameweza kuzuia mtafaruku wao kutoka nje ila hakuna siri hapa duniani.

RUNGU KAPEWA SENZO

Eng. Hersi alisema kuwa ule mchoro wa timu tayari wameutoa kwa Senzo je kweli ataendelea na kitengo hiki au atakifumua na kutengeneza upya?

Kama akikifumua hawa watu wataeda katika sehemu gani? maana inavyoonekana GSM wapo karibu sana na Nugaz wakati upande wa uongozi upo karibu na Bumbuli.

Ingekuwa mimi naamini hawa wote wanaweza hivyo ni busara alifkirie hilo lakini lazima amalize hizi propaganda zinazoendelea.

Kwa Weledi wa Senzo naamini kuna kitu kitatokea na kuna mabadiliko makubwa atayafanya juu ya kitengo hiki.

Yeye ndiye atakaye amua hatma ya kitengo hiki pindi mabadiliko yatakapo kuja au wakati anatoa ripoti yake.

Maana baada ya kumaliza hii wiki ya Wananchi lolote linaweza kutokea juu ya kitengo hiki.

Juu ya ujio wa jezi, hapa viongozi wamechemka kwa kiasi kikubwa sifikirii nini kimewasibu msimu mzima wameshindwa kuzileta siku yao ya wananchi hapa kuna mapungufu. Huenda katika ngazi ya juu au hata waliopewa dili la kutengeneza.

Siku yao ya Mwananchi ingeingiza pesa nyingi sana katika jezi zao naamini ingekuwa hivyo.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Arsenal

Arsenal wameanza kama walivyomaliza msimu

Bernard Morrison

Morrison anabaki kuwa bora mbele ya “Tuisila”