in , , ,

MAAMUZI YA KAMATI YA RUFAA YA NIDHAMU

Makao makuu ya TFF

Baada ya mahojiano kati ya mrufani Dr Damas Ndumbaro na Wakili wa TFF     Nd Emmanuel Muga, pamoja na Wajumbe wa Kamati ya rufaa ya nidhamu kuwahoji wote, Mrufani na Wakili wa TFF, Kamati ya rufaa ya nidhamu ilichukua uamuzi ufuatao:- 

  1. Hoja ya kwanza cha rufaa, kwamba kamati ya nidhamu haikuwa na nguvu za kisheria kusikiliza shauri lake, Kamati ya rufaa ya nidhamu baada kusikiliza hoja za pande zote mbili, kwa uamuzi wa Wajumbe wote kwa maana ya kuwa zote nne za Wajjumbe wa kamati ya rufaa ya nidhamu, ilitupilia mbali hoja hiyo na kuona kwamba kamati ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa mkata rufaa ni afisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kwa mujibu wa Katiba ya TFF ya 2013. Uamuzi katika hoja hii uliamuliwa kwa kura 3 dhidi ya moja.
  2. Hoja ya pili inayosema kwamba kamati ilikosea kisheria kwa kutompa muda wa kuleta utetezi wake wala vielelezo vyovyote vile kwenye shauri lake.

Kamati ya rufaa ya Nidhamu kwenye Shauri hili, baada ya kufanya maamuzi kwa kupiga kura, kura za Wajumbe watatu zilitupiliwa mbali hoja yake na kura moja kati ya kura nne ilikubaliana na hoja yake kwa uamuzi huo, kamati ya rufani ya nidhamu ilitupilia mbali hoja hiyo kwa uamuzi wa wingi wa kura kwa maana ya kuwa tatu dhidi ya kura moja.

Sababu za kutupilia mbali hoja hizo ni kwamba mrufani alipata wito wa kwenda kwenye shauri, na akawakilishwa na wakili wake ( Nestory Peter Wandiba ) kwenye Shauri hilo. Shauri liliposikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 10/10.2014 shauri lilipangwa kusikilizwa tarehe 11/10/2014 Lakini siku hiyo ya pili si wakili wala Dr Ndumbaro alifika kwenye shauri hilo kwa maana hiyo basi shauri lililazimika kusilikizwa upande mmoja kwa mujibu wa kanuni za nidhamu za TFF ibara ya 94 (3).

3. Hoja ya tatu linalosema kwamba kamati ilikosea kusiliza shauri upande mmoja bila ya mtuhumiwa kuwepo, ni kukiuka haki yake ya msingi ya  kusikilizwa.

Kamati baada ya kusikiliza utetezi kutoka pande zote mbili kamati ilifanya uamuzi kwa kupiga kura, na kura tatu (wajumbe watatu) walitupilia mbali hoja hiyo, dhidi ya kura moja (mjumbe mmoja) aliyeikubali hoja hiyo. Sababu za kutupilia mbali hoja hiyo ni kutokana na ukweli kwamba mrufani alipata wito wa kuhudhuria shauri hili na akamtuma wakili wake, lakini mrufani alishindwa kuonyesha vielelezo vya kuonyesha kwamba angesafiri kwenda nje ya nchi ili kamati ya nidhamu iweze kuahirisha shauri mpaka wakati ambao angekuwa amerejea lakini hakufanya hivyo.

Hata hivyo kwa mujibu wa Ibara 144(2) (3) za kanuni ya nidhamu za TFF, mrufani  angeweza pia kuomba kamati ya nidhamu ibatilishe uamuzi iliyoutoa dhidi yake ili aweze kusikilizwa utetezi wake pia hakufanya hivyo na aliamua kukata rufaa.

4. Hoja ya nne inayosema kwamba kamati ilikosea kisheria katika uchambuzi wa ushahidi wa mlalamikaji na hatimaye kutoa uamuzi uliomtia hatiani.

 

Kamati ya rufani ya nidhamu ilisikiliza kwa umakini hoja za pande zote mbili na kujiridhisha kwamba mrufani alifanya makosa kwa kutoa taarifa isiyosahihi na kupotosha maamuzi ya TFF kinyume na kanuni ya 41 (6) ya kanuni za ligi kuu ya Tanzania toleo la 2014 (4) na pia kushawishi, kupotosha au kuzuia maamuzi/utekelezaji wa maamuzi ya TFF kinyume na kanuni ya 41(16) ya kanuni za ligi kuu za Tanzania ya (2014).

Wakati wa kufanya maamuzi, wajumbe watatu(3) kwa maana ya kura tatu zilitupilia mbali hoja hiyo, na kura moja, kwa maana ya mjumbe mmoja alikubaliana na hoja hiyo. Kwa maana hiyo, kamati ya rufaa ya nidhamu ya TFF imetupilia mbali hoja hiyo.

Kwa uamuzi huu kamati inadhibitisha uamuzi wa kamati ya nidhamu iliyosomwa tarehe 13/10/2014, uamuzi huu umefikiwa baada ya wajumbe kupiga kura na uamuzi kupitishwa kwa wingi wa kura za wajumbe watatu, dhidi ya mjumbe mmoja wa kamati hii kwa hoja ya 2,3 na 4 na wajumbe wote 4 walikubaliana kutupiliwa mbali hoja ya kwanza.

Kwa hiyo Dr Damas Ndumbaro ataendelea kutumikia adhabu yake kwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya Mpira wa Miguu (Soka) kwa kipindi cha miaka saba.

Hata hivyo mrufani Dr Damas Ndumbaro anayohaki ndani ya siku 10 kuanzia leo tarehe 10/05/2015 ya kuomba marejeo ya uamuzi huu mbele ya kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF chini ya Ibara 142 ya kanuni za nidhamu za TFF ya mwaka.

Kila upande utabeba gharama zake Hukumu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

QPR washuka daraja

Monk challenges Swansea to take sixth

Swansea wawatibulia Arsenal