in , , ,

Liverpool watupia Tatu kuwaua Spurs

*Manchester United, Chelsea sare

*Newcastle wabahatika kwa Stoke

KWA mara ya kwanza msimu huu, Liverpool wamefanikiwa kufunga timu iliyo juu yao kwenye msimamo wa ligi.

Kocha Brendan Rodgers alijawa furaha zaidi kwa vile ushindi huo umekuja dhidi ya Tottenham Hotspurs walio matawi ya juu.

Hadi wanaingia uwanjani Jumapili hii, vijana hao wa Andre Villas-Boas hawakuwa wamefungwa katika mechi 10 mfululizo za Ligi Kuu ya England (EPL).

Pamoja na ushindi huo, Liverpool waliocheza mbele ya mashabiki wao Anfield, walionekana kupotezana kadiri mpira ulivyoanza.

Wayne Rooney of Manchester United vs Everton. ...
Wayne Rooney of Manchester United vs Everton. at Old Trafford, Manchester. (Photo credit: Wikipedia)

Ndiyo maana baada ya Luis Suarez kuwatanguliza mbele kwa bao dakika ya 21, waling’ara kidogo kabla ya kuanza kusuasua na dakika ya 45 Jan Vertonghen akasawazisha kabla ya kuongeza la pili dakika ya 53.

Kuanzia hapo, hata washabiki wa mapinduzi mekundu ya Anfield walionekana kukata tamaa, lakini Stuart Downing alitumia vyema makosa ya Kyle Walker kusogea na mpira na kuutumbukiza wavuni.

Walau baada ya kusawazisha, Liverpool walirejewa na uhai na kuanza kulisakama lango la Spurs, huku golikipa Hugo Lloris akionekana kulalamika kwa jinsi walivyoruhusu bao la pili.

Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard alitikisa nyavu za Spurs kwa mkwaju mzuri wa penati, baaada ya Benoit Assou-Ekotto kumchezea rafu Suarez alipokuwa anakwenda kufunga.

Jermain Defoe alichangia tatizo kwa timu yake, kwani alitoa pasi mbovu kuelekea eneo la hatari, huku washambuliaji wa Liverpool wakiwa hapo.

Ushindi huo umewapandisha Liverpool kutoka nafasi ya nane hadi ya sita wakiwa na pointi 45, mbele ya Everton wanaolingana nao pointi na nyuma ya Arsenal wenye pointi 47.

Spurs wamebaki nafasi ya tatu kwa pointi 54, lakini Chelsea wakishinda watakapokamilisha mzunguko huu watawazidi kwa pointi moja na kuwang’oa kwenye nafasi hiyo.

Katika mchezo mwingine, Newcastle wakicheza nyumbani St. James’ Park waliwazamisha Stoke City waliokuwa dhaifu kwa mabao 2-1.

Nyota wa Senegal, Papiss Cisse aliwapatia Newcastle pointi mbili muhimu baada ya kufunga bao dakika ya mwisho ya mchezo, baada ya kuibuka bila mabeki kutambua uwapo wake.

Goli jingine la Newcastle wanaofundishwa na Allan Pardew lilifungwa na Yohan Cabaye, lakini Stoke ndio walikuwa wa kwanza kuuona mlango wa wapinzani wao kwa penati ya Jonathan Walters.

Kwa matokeo hayo, Newcastle wamefikisha pointi 33 wakiwa nafasi ya 13 huku Stoke wakiwa nafasi ya 11 kwa pointi 33 pia.

 

ROBO FAINALI KOMBE LA FA

 

Katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA, Manchester United waliachia uongozi wa mabao mawili ya haraka ya kipindi cha kwanza, na kuishia kutoka sare na Chelsea.

Wakitamba Old Trafford, United walifunga bao la kwanza kupitia Javier Hernandez aliyemhadaa Petr Cech aliyetoka golini kwa kupiga mpira mrefu wa kichwa na kujaa nyavuni dakika ya tano.

Wayne Rooney aliyegeuka gumzo la kuhama kutoka United kwenda Bayern Munich msimu wa kiangazi, alifunga bao dakika ya 11, washabiki wakaamini wamekwenda Wembley.

Rooney aliachwa benchi na kocha Alex Ferguson kwenye mechi ya marudiano na Real Madrid, akaingizwa baada ya Man U kufungwa 2-1, na anadaiwa kulalamikia kuachwa huko.

Hata hivyo, kocha Rafa Benitez aliapanga vyema wachezaji wake kipindi cha pili, ambapo waliingia kwa nguvu.

Eden Hazard na Nascimento Ramires walirejesha matumaini Chelsea kwa kufunga mabao dakika za 59 na 68.

Juan Mata alionesha uhai mkubwa, akicheza uwanja mzima na alikosa bao la wazi dakika ya mwisho ya mchezo, baada ya kipa David De Gea kuokoa kwa ncha ya kiatu chake na kumwondolea aibu Ferguson.

Kwa matokeo hayo, mechi hiyo itarudiwa Stamford Bridge, ambapo mshindi kati yao atakabiliana na Manchester City uwanjani Wembley kwenye nusu fainali.

Droo nyingine ya nusu fainali itakuwa kati ya Wigan Athletic na mshindi wa mechi ya marudiano kati ya Millwall na Blackburn Rovers. Katika mechi ya Jumapili hii, Millwall walitoka suluhu na Blackburn.

Mechi za nusu fainali zitafanyika wikiendi ya Aprili 13 na 14.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Hayatou: Woga na udikteta

FIFA SASA YAPEWA URAIS WA TANZANIA!