in

Lini TFF wataleta utamu wa takwimu VPL?

Lakini kwenye mchezo wa soka kuna takwimu za aina mbalimbali. Hapa kwetu TFF inategemewa kuwa chanzo muhimu cha taarifa  za soka nchini

“Rekodi zimewekwa ili zivunjwe”. Huo ni msemo maarufu wa  wahenga duniani. Ni msemo ambao unatumika zaidi kwenye  michezo na burudani. Miongoni mwa rekodi zilizovunjwa ni ile ya  gwiji wa soka Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele  ya kufunga mabao 767 katika maisha yake ya soka.  

Takwimu za Pele zinaonesha mabao aliyofunga kuanzia katika maisha yake ya kandanda duniani. Kuanzia Ligi Kuu Brazil akiwa  na klabu yake ya Santos, timu ya taifa ya Brazil na kadhalika. Pele  amepachika mabao kwenye Fainali za Kombe la Dunia ambazo  alianza kucheza akiwa na umri wa miaka 17 tu. Ni umri ambao  unadhihirisha mapishi ya Kibrazil kwenye kandanda. 

Takwimu za sasa zinaonesha Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji  pekee aliyevunja rekodi ya Pele. Ronaldo amefunga mabao 770,  ikiwa ni matatu zaidi ya Pele. Takwimu hizi zinatumika kwenye  mijadala mbalimbali ili kuonesha umahiri wa wanakandanda  duniani. 

Habari ya pili baada ya ile ya kwanza ya Pele na Ronaldo  inamhusu winga mahiri Theo Walcott. Taarifa ya Walcott iliwahusu waendeshaji wa Ligi Kuu England kumzawadia tuzo  nyota huyo wa zamani wa Arsenal ambaye sasa anakipiga katika  klabu ya Southampton, Theo Walcott.  

Top 10 Most Impressive Records In Football History

Theo alizawadiwa kutokana na kutimiza mechi 300 za Ligi Kuu  England. Tunafahamu kuwa katika Ligi Kuu England kuna tuzo za  aina mbalimbali kuanzia kocha bora wa mwezi, kocha bora wa  msimu, mchezaji bora wa mwezi na msimu au tuzo za wachezaji  bora wa mechi. 

Si EPL pekee, bali La Liga, Lique 1, Serie A, Bundesliga,PSL na  nyinginezo duniani kumekuwa kukitolewa tuzo mbalimbali kwa  wana michezo.  

Tanzania ni nchi ambayo ina wanasoka mbalimbali ambao  wanatumika kwenye vilabu vya Ligi Kuu na Timu za Taifa. Ligi  Kuu tanzania bara inahusisha wageni kutoka Ivory Coast,Zamba,  DR Congo,Angola,Ghana,Togo,Burkina Fasso, Kenya, Uganda, 

Burundi, Rwanda, Zimbabwe na nchi nyinginezo. 

Kwahiyo ni Ligi ambayo inabeba nyora wan chi nyingi ambapo  taarifa zao na michango yao katika kandanda inatakiwa  kuoneshwa kokote ulimwenguni. 

Ligi Kuu Tanzania Bara pia kumekuwa na zawadi wanazopewa  wachezaji bora wa mechi, mwezi na msimu kama ilivyo kwa  makocha bora wa mwezi na msimu. TFF kama vilivyo vyama  vingine vya soka wanajaribu kuboresha na kuhamasisha mchezo  wa soka. hilo wanatakiwa kuungwa mkono. 

Lakini kwenye mchezo wa soka kuna takwimu za aina mbalimbali. Hapa kwetu TFF inategemewa kuwa chanzo muhimu cha taarifa  za soka nchini. Kuanzia historia ya wachezaji mbalimbali,  takwimu na taarifa nyinginezo.  

TFF ndio wanaolea na kusimamia mchezo wa soka kwa  kushirikiana na Bodi ya Ligi Kuu wanaweza kuwa vyanzo muhimu  vya maendeleo ya kandanda nchini. 

Iko hivi, kwenye mchezo huu inabidi TFF na Bodi ya Ligi  watuambie takwimu mbalimbali. Kwa mfano TFF na Bodi ya Ligi  Kuu walitakiwa watuambie ni mchezaji gani amecheza mechi  nyingi za Ligi Kuu Tanzania bara tangu ilipoanzishwa. 

TFF waweke hadharani (tovuti na mitandao ya kijamii) na  kutuambia kinaubaga kuwa ni mchezaji gani ambaye amefunga  mabao mengi ya Ligi Kuu Tanzaniua Bara tangu ilipoanzishwa.  

Hapo sina maana ya mchezaji aliyefunga mabao mengi kwa  msimu mmoja. Nina maana na mchezaji aliyefunga mabao mengi  katika historia ya Ligi Kuu hadi sasa. 

Bodi ya Ligi na TFF walitakiwa watuambie ni mchezaji gani  amecheza mechi nyingi za Ligi Kuu Tanzania. Matahalani  wanaweza kuiga mfano wa kutunza takwimu za wachezaji gani  wamecheza mechi 100 za Ligi Kuu Tanzania Bara.  

Tunaweza kumchukua mastaa wetu wa zamani kama Nadir Haroub na kutazama alicheza mechi ngapi za Ligi Kuu Bara.  Mrisho Ngassa alifunga mabao mangapi ya Taifa Stars au nani  alifunga mabao mengi katika kikosi cha timu ya taifa? 

Kuna wachezaji wan je, bila shaka TFF ilitakiwa kutunza takwimu  zao, nani kati yao alifunga mabao mengi kati ya wanakandada  hao. Takwimu kama hizo zinawezesha TFF kuitangaza Ligi yetu  nje ya mipaka hususani wale wanaofuatilia na kutaka kujua  mambo mengi ya mpira wetu. 

Zama zimebadilika, si kutunza nyaraka kwenye karatasi kabatini  bali pia kutumia nyenzo za kisasa kuweka takwimu na taarifa  ambazo zinawezesha wadau wa soka wa ndani na nje kuzifuatilia na kuzitumia kwa maslahi ya soka la Tanzania. 

Haya mambo ni muhimu na yanahitaji kutumia nguvu kidogo kwa  watu waliopo si lazima kutengeneza ajira mpya kwa watu.  Ninaamini TFF na Bodi ya Ligi inao watu wenye weledi ambao  wanatambua umuhimu wa kutangaza takwimu za wachezaji wetu  iwe kwa mwezi au msimu.

Inawezekana kabisa kuwatangaza na kuwazawadia wachezaji  waliotengeneza mabao, hata kwa kutambua mchango wao.  Inawezekana kabisa kuchagua bao bora la wiki ambalo litakuwa  chachu kwa wachezaji na kutangaza ligi yetu. Hizi ni takwimu  rahisi ambazo hata Shirikisho la soka Ulaya, UEFA wanatumia  kunadi vipaji vya nchi wanachama wao. Inawezekana tukiamua.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Gianni Infantino

‘African Super League’ ni pasua kichwa CAF

Barbara Gonzalez

MAFANIKIO YA UONGOZI WA BARBARA NDANI YA SIMBA