in , , ,

Ligi yamalizika kwa utamu

*Hull washuka, Arsenal wa pili, Spurs Europa
*Liverpool hoi, Rodgers hatarini kufukuzwa

Ligi Kuu ya England imemalizika kwa mtindo wa aina yake, baadhi ya timu zikitoka na karamu ya mabao na nyingine zikiweka rekodi mbaya.

Hull wameshuka daraja baada ya Newcastle waliokuwa wakiviziana nani ashuke kuwafunga West Ham huku Hull wenyewe wakienda suluhu na Manchester United. Hull walihitaji ushindi lakini pia wakiomba Newcastle ama wafungwe au watoshane nguvu na wapinzani wao.

Kocha Steve Bruce ameeleza kusikitishwa kwake na kushuka daraja, akisema vijana wake hawakucheza vyema. Mchezaji wa zamani wa Tottenham Hotspur aliyejiunga Hull kwa mkataba wa miaka mitatu, Michael Dawson amesema hakutarajia kitu kama hicho alipokuwa akisaini mkataba.

Arsenal walimaliza ligi kwa nguvu na kushika nafasi ya tatu hivyo kufuzu moja kwa moja kwa hatua za makundi za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL), baada ya kuwakandika West Bromwich Albion 4-1.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na Theo Walcott matatu na Jack Wilshere moja. West Brom walifunga kupitia kwa Gareth McAuley.
Walcott alichezeshwa kama mshambuliaji wa kati, nafasi ambayo amekuwa akisema anaipenda, lakini huwa hapangwi kutokana na kuwapo wengine waliobobea hapo kama Olovier Giroud.

Walcott bado hajafikia mwafaka na klabu yake juu ya kuhuisha mkataba wake akiwa amebakiza karibu mwaka mmoja tu umalizike. Arsenal hawajapata kufungwa kwenye mechi ya mwisho wa msimu tangu 2005 walipolazwa 2-1 na Birmingham.

Mahasimu wa Arsenal wa London Kaskazini, Spurs wamefanikiwa kuwavuka Liverpool na kufuzu moja kwa moja kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Europa, baada ya kuwafunga Everton 1-0 kwa bao la mshambuliaji machachari chipukizi wa England, Harry Kane.

Spurs wamewazidi Liverpool kwa pointi mbili baada ya Liver kukung’utwa mabao 6-1 kwenye mechi ya mwisho ambayo ilikuwa pia ya kumuaga nahodha wao, Steven Gerrard anayekwenda kucheza soka nchini Marekani.

Jedwari, likionyesha mgawanyo wa mapato kwa timu zote zilizo shiriki EPL 2014-2015
Jedwari, likionyesha mgawanyo wa mapato kwa timu zote zilizo shiriki EPL 2014-2015

Ushindi wa Spurs umewaweka Everton katika rekodi mbaya, wakiwa wamemaliza ligi chini ya timu 10 za juu kwa mara ya kwanza tangu 2006. Msimu huu Everton walianza ligi kwa kusuasua, tofauti na msimu uliopita ambapo vijana hao wa Roberto Martinez walikuwa wazuri. Huu ulikuwa mchezo wa tatu kupoteza miongoni mwa minne iliyopita.

Kwa upande wa Liverpool, hii ni mara ya kwanza katika miaka 52 kuruhusu mabao sita kwenye mechi moja, ambapo kocha Brendan Rodgers naye ameweka rekodi mbaya ya kukosa walau kikombe kimoja katika misimu mitatu.

Rodgers amekiri kwamba yupo katika shinikizo kubwa na atakubali kuondoka iwapo wenye klabu wataamua hivyo, japokuwa anasema pia kwamba bado ana mengi ya kuwasaidia kama atabaki Anfield.

Liver ambao msimu uliopita nusura watwae ubingwa kama si kuvurunda mechi za mwisho na kupitwa na Manchester City, wamemaliza katika nafasi ya sita hivyo watatakiwa kuanzia raundi ya tatu ya kufuzu kwa Ligi ya Europa Julai 30, ambapo wakifuzu watakuwa na mechi nyingi katika msimu ujao ambazo pia huchosha.

Southampton ndio wanaowafuata Liverpool katika nafasi ya saba ambapo Jumapili hii walikubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Man City ambao wamemaliza ligi wakiwa nafasi ya pili, baada ya kuvuliwa ubingwa na Chelsea mapema.

Swansea waliokuwa wazuri nao wamemaliza ligi vibaya kwa kufungwa 1-0 na Crystal Palace. Hata hivyo wamebaki kwenye nafasi ya nane waliyokuwa wakishikilia , wakifuatiwa na Stoke huku Palace wakikamata nafasi ya 10.

Palace wameimarishwa na kocha wao Alan Pardew aliyeajiriwa kutoka Newcastle wakati timu ikiwa katika eneo la hatari la kushuka daraja, na sasa amewawekea msingi mzuri kwa msimu ujao.

Matokeo ya mechi za mwisho wa EPL Jumapili hii yalikuwa Arsenal kuwalaza West Brom 4-1, Aston Villa kulala 1-0 kwa Burnley waliokwishashuka daraja; Chelsea kuwafunga Sunderland 3-1; Palace wakawapiga Swansea 1-0 na Everton kulala 1-0 kwaSpurs.

Kwingineko Hull na Man United walikwenda suluhu; Leicester wakawakung’uta QPR waliokwishashuka daraja mapema 5-1; Man City wakawapiga Southampton 2-0, Newcastle wakawazidi nguvu West Ham kwa 2-0 na Stoke kuwaadhibu Liverpool 6-1.

Kwa hali hii timu zilzioshuka daraja ni Hull waliomaliza wakiwa na pointi 35, Burnley wenye 33 na QPR mkiani na 30. Aston Villa ndio walibaki wakichungulia kushuka lakini wakishajihakikishia kabla kutoshuka kwani pointi zao 30 zilikuwa zinawatosha kubaki juu.

Pointi hizo ni sawa na walizokuwa nazo Sunderland ambao wameokolewa kushuka daraja na Dick Advocaat aliyeajiriwa kwa muda kwa ajili hiyo na sasa amerudi kwao Uholanzi kumuomba mkewe ruhusa ya kuendelea na klabu hiyo msimu ujao.

Newcastle walikuwa katika wakati mgumu na wangeweza pia kushuka kama si kujitahidi jana na pia kusaidiwa na matokeo ya Hull kutoshinda, wakiwa katika mkwaruzano baina ya washabiki na mmiliki Mike Ashley lakini pia kocha John Carver akiwa haelewani vya kutosha na wachezaji wake.

Timu zilizokuwa na uhakika wa kubaki EPL kwa zaidi ya wiki moja hivi ni Leicester, West Brom, West Ham na Everton lakini zikiwa hazina fursa ya kucheza michuano ya Ulaya. Jumatatu hii Norwich wanacheza na Middlesbrough kujua nani atapanda EPL kuungana na Bournemouth na Watford.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

PSG watema £88m kumtwaa Ronaldo

kaseke.

Simba, Yanga waanza usajili