in , , ,

*LIGI KUU YA VODACOM 2013/2014 KUANZA AGOSTI 24*

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa
2013/2014 inaanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu kwa timu zote 14 kuwa
viwanjani katika miji saba tofauti.

Hata hivyo, kabla ya ligi hiyo kuanza kutakuwa na mechi ya kufungua msimu
(Ngao ya Jamii- Community Shield) kati ya bingwa mtetezi Yanga na Makamu
bingwa Azam itakayochezwa Agosti 17 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.

Mechi za VPL za Agosti 14 mwaka huu zitakuwa kati ya Yanga na Ashanti
United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mtibwa Sugar na Azam (Uwanja wa
Manungu, Morogoro), na JKT Oljoro na Coastal Union (Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).

Nyingine ni Mgambo Shooting na JKT Ruvu (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino
Rangers na Simba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na
Kagera Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Ruvu Shooting na
Tanzania Prisons (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani).

Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Novemba 3 mwaka huu wakati wa
pili utamalizika Aprili 27 mwakani. (*Ratiba ya mzunguko wa kwanza na wa
pili imeambatanishwa- attached).*

*TAIFA STARS KWENDA KAMPALA J5*

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaondoka Mwanza keshokutwa (Julai
24 mwaka huu) kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya marudiano ya
Kombe la CHAN itakayochezwa Jumamosi (Julai 27 mwaka huu) Uwanja wa Mandela
kuanzia saa 10 kamili jioni.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini
Mwanza chini ya Kocha Kim Poulsen tangu Julai 14 mwaka huu kujiandaa kwa
mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za
CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Timu hiyo itaondoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza saa 7.25 mchana kwa ndege ya
PrecisionAir, na inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe
saa 10.15 jioni.

Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen kesho (Julai 23 mwaka huu) atakuwa na
mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya kikosi chake.
Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye hoteli ya La Kairo
jijini Mwanza.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Barcelona watamchukua nani

Mkenya ashinda Tour de France