in , ,

LIGI KUU BARA: VIGOGO WAANZA VIZURI

 

SIMBA YAVUNJA MWIKO MKWAKWANI

 

Mshikemshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu umeanza hapo juzi Jumamosi kwenye viwanja tofauti. Katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga Simba SC waliokuwa wageni wa African Sports iliyopanda daraja msimu huu walifanikiwa kuvunja mwiko kwa kuwafunga wenyeji wao 1-0 na kuchukua alama tatu.

Bao pekee la Simba lilifungwa na mshambuliaji wao mpya Hamis Kiiza kwa kichwa safi akimalizia krosi ya nahodha Mussa Hassan Mgosi. Kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo Wekundu hao hawakuweza kuonyesha makali ya kutosha kuwapatia bao hivyo walilazimika kusubiri mbaka kipini cha pili na kujipatia bao la ushindi kwenye dakika ya 57.

Pengine uimara wa golikipa wa wapinzani Yusuph Abdul ambaye aliwahi kuichezea Yanga pia ulichangia kuwanyima bao Simba kwenye kipindi cha kwanza. Jumla ya mshuti yaliyolenga bao kwa upade wa Simba yalikuwa manne huku mshambuliaji wao mwingine mpya Boniface Maganga akikosa nafasi ya kuipatia Simba bao la pili kwenye dakika za mwisho.

AZAM YATAMBA NYUMBANI

Azam FC kwenye mchezo wao uliopigwa nyumbani kwao kwenye dimba la Azam Complex Chamazi Dar-es-salaam walifanikiwa kuibuka na ushidndi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Prisons ya Mbeya.

Kuanzia dakika za mwanzo za mchezo Azam walionyesha ubora wa hali ya juu lakini hawakuweza kupata bao lolote mbaka kufikia dakika ya 40 ambapo Kipre Tcheche alitumia juhudi na uwezo binafsi akampangua golikipa pamoja na walinzi na kutupia mpira wavuni kwa urahisi.

Hata hivyo bao la Kipre halikuweza kuwatosha kuwapatia alama tatu pale Prisons waliposawazisha bao kupitia kwa Jeremia Juma baada ya walinzi wa Azam kufanya uzembe kwenye dakika ya 60 ya mchezo.

Ni winga anayechipukia Farid Mussa aliyewapatia Azam bao la ushindi zikiwa zimesalia dakika chache kabla ya mchezo kumalizika. Akiongea na Azam TV baada ya mchezo Farid alisema kuwa wanashukuru kupata ushindi kwenye mchezo wa kwanza na watapigana zaidi ili waendelee kushinda michezo ya mbeleni na kutwaa ubingwa.

YANGA YAKWEA KILELENI MAPEMA

Ushindi wa mabao mawili kwa sifuri ambao Yanga SC waliupata kwenye mchezo wa jana dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam umewapeleka mabingwa  hao watetezi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mapema kwenye dakika ya saba ya mchezo mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita Simon Msuva aliwapatia Yanga bao la kwanza baada ya kucheza ‘one-two’ na Amis Tabwe.

Yanga wakaendelea kuutawala mchezo huku wageni wao Coastal Union ambao pengine walikusudia kulipa kisasi cha mabao 8-0  waliyopigwa na mabingwa hawa msimu uliopita wakishindwa kufanya lolote la maana.

Makosa ya mlinzi wa Coastal Union Tumba Sued yakawapatia Yanga bao la pili dakika chache kabla ya mapumziko. Mlinzi huyo alishindwa kutumia uwezo wake  kuondosha mpira wa kona kwenye eneo la hatari hivyo mshambuliaji Donald Ngoma akajiapatia bao rahisi.

Sasa mabingwa hao wapo kileleni mwa msimamo wa Ligi wakiwazidi Azam, Kagera Sugar, Majimaji, Mtibwa Sugar, Simba SC na Toto African kwa tofauti ya mabao pekee huku timu zote hizo zikiwa na alama tatu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Leicester wawafunga Villa

Tanzania Sports

KASHFA YA MLUNGULA FIFA: