in

Leeds United kubebwa tena na uchawi wa Bielsa?

Leeds United

Leo ninapenda kujibu swali la wasomaji wetu. Ninajibu swali kuhusu historia ya kocha wa Leeds United, Marcelo Bielsa baada ya siku kadhaa zilizopita kuelezea jinsi ninavyoikumbuka Leeds United. Wengi walijiuliza ni nani huyo kocha? Ana mafanikio gani katika kandanda na maswali mengine yanayofanana nayo.

Kwahiyo le makala haya yanaelezea historia ya kocha Bielsa ambaye amefanikiwa kuwarudisha kwenye Ligi Kuu England wababe hao wa Ellang Road waliopata kutikisa kwenye mchezo huo kabla ya kushuka daraja miaka 16 iliyopita.

EL LOCO

Jina lake kamili ni Marcelo Alberto Bielsa Caldera. Jina la utani anaitwa El Loco likiwa na maana ya mwehu. Katika kandanda yapo majina yanayochukuliwa kama utani lakini yanakubalika na kuzoeleka. Kwa mfano kocha wa Atletico Madrid anaitwa El Cholo. Ni jina lililizoeleka. Kwahiyo El Loco naye amezoeleka hivyo hivyo. El Loco alizaliwa tarehe 12 julai mwaka 1995 huko Rosario nchini Argentina.

BEKI WA KATI

Katika maisha yake ya soka alikuwa mchezaji wa nafasi ya beki. Aliichezea klabu ya Newell’s Old Boys (1975-1977), Instituto  de Coedoba (1978-1980. Katika kipindi chake cha uchezaji hakuwa hatari uwanjani lakini uwezo wake sio wa kupuuzwa.

TAIFA LA WABABE

Bielsa anatokea Argentina alikotokea Lionel Messi na El Cholo. Anatokea kwenye taifa lililowaleta wababe wa soka duniani kama vile Gabriel Batistuta, Juan Sebastian Veron, Ariel Ortega, Diego Maradona, Diego Simeone, Walter Samuel, Sergio Kun Aguero, na wakali wengine waliotamba vilabu mbalimbali barani Ulaya. Naye kama walivyo wababe wengine amewahi kuichezea timu ya taifa ya Argentina lakini hakufanikiwa kiufumania nyavu.

MAISHA YA UKOCHA

Bielsa alianza kuwa kocha katika timu mbalimbali nchini Argentina na Chile. Alianza maisha ya ukocha katika klabu ya Newell’s Old Boys kwa kuongoza kupata ushindi mwanzoni mwa miaka 1990. Alihamia nchini Mexico mwaka 1992, ambako alizifundisha Club Atlas na Club America. Mwaka 1997 alirejea Argentina kuwa kocha wa Velez Sarsfield.

Jina lake lilianza kunglara zaidi baada ya kuinoa timu ya taifa ya Chile ikipata matokeo bora zaidi kuliko vilabu. Kuinoa timu ya taifa ya Chile kulimpa heshima na kuanza kuafuatiliwa na vyombo vya habari ili kuzijua habari zake zaidi.

Kocha huyo amewahi kuinoa klabu ya Atletico Bilbao ya Hispania kati ya mwaka 2011 na 2013. Mafanikio aliyopata katika klabu ya Atletico Bilbao ni kufika fainali ya kombe la Ligi ya Ulaya. Mwaka 2015 aliachana na Bilbao kisha kwenda kuinoa Olympique Marseille ya Ufaransa ambako alidumu kwa mwaka mmoja.

Juni mwaka 2018 aliteuliwa kuwa kocha wa Leeds United ambapo ameiongoza kurudi tena Ligi Kuu England tangu iliposhuka daraja miaka 16 iliyopita.

Mei 2, mwaka 2014 aliajiriwa kama kocha wa Marseille ya Ufaransa.  Hata hivyo alijiuzulu ukocha klabuni hapo mnamo Agosti 8 mwaka 2015.

Mwaka 2016 Bielsa aliteuliwa kuwa kocha wa Lazio ambako alijiuzulu siku mbili baada ya kuajiriwa hali ambayo ilisababisha mnyukano wa kisheria kati ya klabu na kocha huyo.

Mwezi Mei mwaka 2017 aliteuliwa kuwa kocha wa Lille ya Ufaransa, akiwa klabuni hapo aliwapa nafasi chipukizi kama Nicolas Pepe, Thiago Mendes,Thiago Maia, Kevin Malcutt, Fode Ballo-Toure, Luiz Araujo na Edgar. Novemba 2017 alifukuzwa kazi ya ukocha Lille baada ya mechi  13 za Ligi Kuu Ufaransa.

TIMU YA TAIFA

Bielsa alikabidhiwa jukumu la kuinoa timu ya taifa ya Argentina mwaka 1998 katika kipindi ambacho alikuwa kocha wa klabu ya Espanyol. Alipokea kijiti kutoka kwa Daniel Passarella. Mwaka 1999 aliongoza Argentina kutinga fainali ya mashindnao ya Copa America.

Hata hivyo katika mchezo wa fainali Argentina ilifungwa mabao 3-0 na Colombia. Ni katika mchezo huo mshambuliaji Martin Palermo alishindwa kufunga penati tatu walizopata.

Mwaka 2002 aliongoza Argentina katika fainali za Kombe la Dunia, hata hivyo hakufua dafu baada ya kutolewa  katika hatua za awali. Mwaka 2004 alitwaa medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki baada ya nchi hiyo kushindwa kwa miaka 52. Baada ya mashindano hayo alijiuzulu na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Pekerman.

FAINI YA MPELELEZI

Miongoni mwa mambo ya kukumbukwa ya kocha huyu ni mtindo wake wa kuwatuma wapelelezi kwa timu pinzani kuona namna wanavyojiandaana mchezo dhidi ya timu yake.

Tukio la kukumbukwa ni maandalizi ya timu ya Derby Country iliyokuwa ikifundishwa na Frank Lampard kabla ya khamia Chelsea. Bielsa alikiri kumtuma mpelelezi wake kuichungulia Derby ilivyokuwa inajiandaa kwa mchezo dhidi ya Leeds United.

Mnamo Februari 18 Leed United walilimwa faini ya pauni 200,000 kwa kosa la Bielsa kutuma mpelelezi kwa timu pinzani ambapo walikiuka kanuni namba 3 kifungu cha 4.

Tukio jingine ni uwezo wake wa kuwafundisha waandishi wa habari namna ya timuyake inavyocheza uwanjani. Januari 16 mwaka 2019 aliitisha mkutano na vyombo vya habari ambako aliwasilisha namna ya makocha wanavyofanya kazi.

GWIJI WA MBINU

Bielsa anasfika kwa timu zake kutawala mchezo. Daima anatumia mfumo wa 3-3-3-1; mabeki watatu, viungo watatu (mmoja kiungo wa ulinzi na wawili wanacheza pembeni), viungo washambuliaji watatu (mmoja namba 10 na wawili mawinga) na mshambuliaji mmoja.

Mfumo wa 3-3-3-1 unafanya kazi ya kushambulia na kujilinda kwa wakai mmoja. Pia unasaidia kujilinda kwa mabeki 7, kisha kushambulia kw akutumia wachezaji 6 au 7. Ni mfumo ambao mashambulizi yanatokea kila upande, ambapo aliutumia alipokuwa Olympique Marseille.

Msimu wa 2018-2019 akiwa Leeds United alianza kutumia mfumo wa 4-1-4-1. Alipokabiliana na timu inayotumia mfumo wa washambuliaji wawili yeye alibadili na kutumia 3-3-3-1. Mbinu zake zimekuwa zikiwavutia makocha wengine ambao wamekiri kuiga mtindo wa Bielsa. Mfano Gerardo Matino, Pochettino, Diego Simeone, Matias Almeyda, Eduardo Berizzo, Mauricio Pellegrino, Santiago Solari na Marcelo Gallardo ambao wametokea Argentina pia.

Kwa mujibu wa nahodha wa zamani wa Argentina, Roberto Ayala, amewahi kuaviambia vyombo vya habari kuwa Bielsa anatumia mifumo 29 tofauti katika mechi mbalimbali. Kwenye kazi hiyo amewahi kutwaa taji la Ligi Kuu Argentina pekee. Lakini ni mwalimu ambaye anasifika kwa ufundi wa kufundisha kandanda.  

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Ndemla

Simba siyo sehemu sahihi kwa Ndemla

Wachezaji wetu

Nini chanzo wachezaji wetu kurudi kutoka Ulaya?