in

Kwanini PSG na Bayern Munich hazipo European Super League?

MICHUANO ya European Super League imetangaza rasmi kuanzishwa. Mwenyekiti wa klabu 12 ambazo zimekubaliana kuanzisha mashindano hayo Florentino Perez alizitaja timu husika lakini katika orodha yake hakuna timu za Ufaransa na Ujerumani, ambako kuna PSG na Bayern Munich. 

Timu hizo mbili hazikuwa miongoni mwa wanachama 12 waliotia sahihi ya kukubalia kuanzisha mashindano ya klabu kubwa barani Ulaya na zitashiriki-na inatajwa zipo zingine 3 ambazo hazijawekwa wazi.

Tanzaniasports inachambua sababu za msingi za kwanini timu za nchi hizo mbili  yaani Bundesliga na Ligue 1 hazijajitokeza kuwa miongoni mwa timu zilizoanzisha wala kutamani kushiriki mashindano hayo.

Tanzania Sports
VILABU VINAVYOTAJWA KUASISI LIGI MPYA

Tukianzia suala la PSG, ambako timu hiyo imejitokeza katika pande tatu za siasa (kutokana na umiliki wan chi), uchumi (kutokana na uwekezaji wa kampuni ya umma) na kimichezo (kutokana na uhusiano kati ya Qatar na mashirikisho ya UEFA na FIFA).

PSG inamilikiwa na kampuni ya Qatar Sports Investment na rais wake ni Nasser A Khelaifi ambapo pande zote mbili zina uhusiano thabiti na mashirikisho ya soka ya UEFA na FIFA. Kampuni yao nyingine ya BeiN Sporyts inamiliki haki za Televisheni za kurusha matangazo ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Aidha, nchi ya Qatar itakuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022. Mashirikisho yua soka UEFA na FIFA zimekataa mpango wa kuanzishwa mashindano ya European Super League. Rais wa PSG Al Khelaifi amechukua uamuzi wa kulinda uhusiano mzuri na rais wa UEFA, Aleksander Ceferin,

Zipo tetesi kuwa Al khelaifi huenda anajiandaa kuchukua nafasi ya urais wa urais wa Umoja wa klabu za soka za Ulaya (ECA) baada ya Andrea Agnelli kuondoka na kuhamia Super League.

Kwa upande mwingine, SPG inafahamu kuwa kujitoa kw eye Ligi ya Mabingwa Ulaya na kujiunga European Super League itakuwa chanzo cha kupoteza mapato yanayotokana na nyota wao hivyo kuwawia vigumu wakatiwa kuingia mikataba nao. Mikataba ya Neymar na Kylian Mbappe inamalizika mwaka 2022 na huenda ikawa vigumu kuwasainisha mipya.

Tanzania Sports
UEFA

Vyombo vya habari vya Ufaransa vimetaja uamuzi wa kuanzisha Super League umetengeneza pengo kubwa kati ya klabu za Ufaransa na Ujerumani hivyo kuibua vita vya matajiri wa klabu.

Nchini Ujerumani, hali imekuwa tofauti kwani klabu zao daima zimekuwa na uhusiano wa karibu na mashabiki wao na kwa sababu hiyo nyingi zinaona hakuna hoja ya msingi kujiunga na Super League.

Mkurugenzi mtendaji wa Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke amethibitisha kuwa klabu yake na Bayern Munich zimekataa ofay a kujiunga na European Super League. Badala yake Dortmund na Bayern Munich zinakubaliana kuwa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yaimarishwe.

Timu zingine ambazo hazijakubali mpango ni za Ureno; Porto, Benfica, Sporting Lisbon zenye sifa lukuki katika mashindano ya Ulaya. Nchini Hispania klabu kama vile Sevilla haijakubali mpango wa kujiunga Super League hali ambayo inatajwa kuwa ni mgawanyiko mkubwa.

Fahamu undani wa European Super League

Mosi. Jumla ya tomu 20 zinatakiwa kushiriki mashindano hayo. Timu 12 ndio waanzilishi wa mashindano hayo na klabu zingine tatu hazijatajwa zinaelezwa kuwa miongoni mwa wanachama wa Super League.

Pili, kwa mujibu wa utaratibu wa mashindano hayo, inatakiwa timu tano ziwe zinafuzu kila mwaka. Timu 20 zitapangwa katika makundi mawili yenye timu 10.

Tatu,mechi za mashindano ya Super League zitakuwa za nyumbani na ugenini kwa timu zote za zitakazounda makundi hayo. Mfano timu za kundi A kumi zitacheza mechi za nyumbani na ugenini, hali kadhalika timu za kundi B.

Nne,timu tatu katika msimamo wa kundi kutoka makundi hayo mawili zitakuwa zimefuzu kwa hatua ya robo fainali. Huku zile zitakazoshika nafasi ya nne na tano zitapambana na zile zitazotolewa kwenye robo fainali na nusu fainali.

Tano, mchezo wa fainali utapngwa kuchezwa kwenye uwanja wa ugenini mwezi Mei.

Sita, timu wanachama wa Super League ni wa kudumu hivyo hawatakuwa na hofu ya kushindwa kufuzu mashindano hayo kama ilivyo kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Saba, kila klabu mwanachama anatarajiwa kuvuna kitita cha pauni milioni 400 kama njia ya kujiongezea kipato kwa uendeshaji na faida za mashindano kwa timu. Kiasi hicho ni kikubwa mara nne zaidi ya kile kinachotolewa kwa mshindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

Nane, timu za Super League zitapokea fedha za haki za televisheni moja kwa moja kuliko ilivyo kwa UEFA ambako bodi huzigawanya na kukabidhi kwa timu na kushirikisha zingine ndogo. 

Tisa, ligi nyingi ztaonekana hazina maana tena, vyama vya soka havitakuwa na mamlaka tena, wachezaji watapunguziwa mishahara au viwnago vya mishahara vinaweza kushuka kwa kasi, thamani za klabu ndogo zitazidi kuporomoka kwa sababu hazitakuwa na mvuto kibiashara kuliko zile zilizoanzisha Super League.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

70 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Mnyukano wa European Super League na UEFA

Tanzania Sports

Utamu mwingi wa Yanga unakosa makocha