in

Kwanini Man United wamenunua mchezaji huyu?

Donny van de Beek


Donny van de Beek amecheza dakika 61 katika mechi za Ligi Kuu
England. Nyota huyo alinunuliwa kwa pauni milioni 40 lakini haonekani
kuwa mchezaji wa kupatiwa nafasi. Sasa, je ni kipi kiliwafanya
mabosi wa Man United kumsajili kiungo huyo? Usajili wake kutoka Ajax
umekuwa kama vile ni kukanyaga kaa la moto kwani kocha Ole Gunnar
Solskjaer hajamtumia ipasavyo nyota huyo.


Wachezaji wa zamani kama Gary Neville na Patrice Evra wamehoji
uamuzi wa kumweka benchi sta awao waliyomgharamia pesa nyingi, na
kuibua swali kulikuwa na ulazima gani kwa bodi ya Manchester United
kumwaga fedha za kumsajili mchezaji ambaye hawamtumii kwenye
kikosi chao.


Kiungo huyo ana miaka 23 tu. Ni kinda ambaye anao muda wa kutosha
kuonesha uwezo wake kwenye kandanda, lakini anaonekana
kuchanganywa na hali ya kukaa benchi karibu kila mechi za EPL.
Kwenye mchezo wa ufungizi wa EPL dhidi ya Crystal Palace alipewa
dakika 13 akitokea benchi.


Donny van de Beek huenda alifikiria kuwa atapata namba katika kikosi
cha kwanza mapema sana, lakini hali ilivyo kwa sasa imekuwa tofauti
na matarajio yake.


Wikiendi iliyopita Man United walimenyana na Chelsea. Mojawapo ya
maeneo ambayo yaliinyima ushindi Man United ni eneo la kiungo.
Hapakuwa na kiungo mbunifu ambaye angeweza kuleta matokeo tofauti.
Hapakuwa na hali ya kubuni mbinu za kuvunja ukuta wa Chelsea.
Man United walihitaji mchezaji ambaye angeweza kuongeza ubunifu ili
kupata mabao mbele ya Chelsea, lakini hali ilikuwa tofauti na kiungo

huyo alikuwa amekali benchi huku kocha wake Ole akiwa hana dalili za
kumpa nafasi kwenye mchezo huo.
Mashambulizi ya Man United yalikuwa yanakosa maarifa katika hatua
ya mwisho, kwa vile hapakuwa na mchezaji ambaye angeweza kuituliza
timu mbele ya lango la Chelsea na kutengeneza pasi za mabao. Hiyo ni
kazi ya van Beek lakini hakuwapo uwanjani, na kocha alimkalisha
benchi.


Picha zinamwonesha van de Beek akiwa benchi kwa huzuni. Ni
mchezaji ambaye anajaribu kuyaelewa mazingira ya yeye kukwekwa
benchi kila anapokitazama kikosi cha Man United.
Baada ya kuingia akitokea benchi kwenye mchezo dhidi ya Palace,
akapewa dakika moja tu kwenye mchezo mwingine dhidi ya Brighton.
Ndani ya kikosi cha Man United amepangwa kikosi cha kwanza kwenye
mchezo dhidi ya Luton.
Mchezo huo ulikuwa wa kuwania kombe la Carabao. Mchezo mwingine


alioanza kwenye kikosi cha kwanza ni ile dhidi ya Brighton wa kombe
la Carabao, na kisha zingine za EEPL amekuwa mchezaji wa kukalia
benchi ilhali ndiye ghali zaidi kikosini humo.
Akizungumza kabla ya mchezo wa wikiendi iliyopta kocha wa Man
Unted alisema Van De Beek atapata nafasi yake katika kikosi cha
kwanza, lakini ushindani kwenye kikosi chake ndiyo unasababisha
awekwe benchi kwa sasa.
TAKWIMU
Van De Beek amecheza dakika 78 katika mchezo dhidi ya Luton
kwenye kombe la Carabao. Amecheza dakika moja kwenye mchezo wa
EPL dhidi ya Brighton. Amecheza dakika 90 kwenye mchezo dhidi ya
Brighton wa mashindano ya Carabao.

Katika mchezo EPL dhidi ya Tottenham alicheza dakika 22. Mchezo
mwingine wa EPL dhidi ya Newcastle United alicheza kwa dakika 14 tu.
Katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya alicheza dakika 2 dhidi ya
PSG. Kwenye mchezo wa EPL dhidi ya Chelsea alikaa benchi pekee
hakukuwa na dakika zozote alizopewa uwanjani.
Pengine tunaweza kusema Van De Beek ameingia Ligi mpya, kocha
mpya, wachezaji wapya,maizngira mapya na mbinu mpya mbazo
zinatakiwa kuwa na muda wakutosha ili kujiimarisha.
Hata hivyo, ni namna gani kocha wa Man United anapandisha thamani
ya mholanzi huyo? Ni kwa vipi mchezaji wao ghali anakuwa wa kukaa
benchi na kuonekana kama vile hakukuwa na umuhimu wa kumsajili?
Nini maana ya matamshi ya Ole Gunnar kwa nyota huyo kwa sababu
hadi sasa Man Unityed hakuna mafanikio yoyote kwani bado imekuwa
timu inayocheza kwa kubahatisha zaidi.
VAN DE BEEK ALIKOSEA?


Kumekuwa na mjadala nchini Uholanzi, ambapo baadhi ya wanasoka
wa zamani wanaamini nyota huyo angefaa zaidi kucheza Barcelona
kuliko Man United.


Marco van Basten, nyota wa zamani wa Uholanzi amesema,
“Inawezekana Van De Beek anapitia njia ya mafunzo na kueilewa Man
United ya sasa, lakini Donny alipaswa kusubiri ofay a Barcelona si
kupokea ya Man United. Kadiri anavyokaa bila kucheza na ndivyo
nafasi ya kucheza inavyozidi kutoweka. Donny atakuwa anafikiria
mengi yanayopita kichwani mwake na kujutia uamuzi wa kwenda Old
Traford. Lazima atakuwa anafikiria ni nini kinachoendelea kwake
wakati huu. Jambo lingine, inakuwaje unatumia pauni milioni 40
kumsajili mchezaji ambaye humtumii? Kulikuwa na ulazima gani kwao

kumsajili kama mazingira yake yapo hivyo kwa sasa. Kama mchezaji
lazima Donny atakuwa anafikiria anafanya nini katika klabu hiyo.”
Kwenye mechi za Chelsea na PSG Ole aliwapanga Fred na McTominay,
huku nyota wao mwingine Paul Pogba akiwa amewekwa benchi ambapo
nafasi yake ilichukuliwa na Bruno Fernandes ambaye anaweza kucheza
nambari 10. Lakini katika nafasi ya winga ambako Van De Beek
aanamudu kucheza hakupewa nafasi, laizma atakuwa kwenye
mkanganyiko; nini kinachoendelea klabuni hapo, kw avile nafasi yake
walipangwa Juan Mata na Daniel James.


Donny aliweka jina lake katika klabu ya Ajax kama mmoja wa
wachezaji wakali watakaotikisa ulaya. Ana uwezo,maarifa ya
kuunganisha ulinzi na kiungo. Msimu uliopita alifunga mabao 10 akiwa
Ajax, lakini je anaweza kupata namba mbele ya Fernandes?


Ni lini atafaidika na matunda ya uwekezaji wake kwa Donny Van De
Beek? Imebaki miezi sita tu msimu huu kumalizika, ni wapi Donny
atakuwepo na nini kitaendelea katika maisha yake ya soka ndani ya Old
Trafford? Anapokea mshahara wa pauni 108,000 kwa wiki na ana
mkataba wa miaka mitano klabuni hapo lakini anaonekana si tegemeo
kwa msimu wa 2020-2021.


Kwa kawaida, mchezaji huweza kuchanganyikiwa pale anapoona
mambo hayaendi vizuri kwa upande wake. Hii inaweza kusababisha
kuhoji uamuzi wake wa kujiunga Man United kama ulikuwa sahihi au
mbovu. Hapo ndipo panaohitaji utulivu na umakini wa benchi la ufundi
kwani wanaweza kupoteza kiwango na ujuzi wa nyota huyo kwa
kutompanga kikosi cha kwanza. Atafubaa zaidi na kuporomoka uwezo.
Lakini kwanini walimnunua?

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Bingwa wa kikapu

Bingwa Kikapu Apatikana Bongo

Tanzania Sports

Sven wa Simba Ajiandae Kisaikolojia