in , , ,

KWANINI KLOPP ANA NAFASI KUBWA YA KUMFUNGA PEP?

Leo kuna mechi ambayo inawakutanisha Liverpool na Manchester City
katika uwanja wa Anfield.

Mechi ya mzunguko wa kwanza Manchester City alifanikiwa kuifunga
Liverpool goli 5-0.

Leo hii wanakutana wakati ambao Liverpool anatafuta nafasi ya kubaki
kwenye nafasi nne za juu na Manchester City akitafuta nafasi ya
kujichimbia juu.

Manchester City mpaka sasa hajafungwa na katika michezo yote
aliyocheza msimu huu ni mchezo mmoja tu ambao kamaliza bila kufunga
goli (dhidi ya Crystal Palace).

Leo anaenda kwenye uwanja wa Anfield, nafasi yake ikoje? Ana nafasi ya
kupoteza mechi hii?

Manchester City ana nafasi ngumu katika uwanja wa Anfield leo hii
kutokana na sababu zifuatazo.

Liverpool wanaingia bila Philippe Countinho kwa mara ya kwanza. kuna
uwezekano mkubwa timu zote zikaingia na mfumo wa 4-3-3.

Mfumo huu utakuwa na manufaa kwa Liverpool kwa sababu kwa siku hivi
karibuni Liverpool wamekuwa wakitumia vizuri mipira ya krosi
wanazopiga na Manchester City kwa siku za hivi karibuni wamekuwa
wakishindwa kujilinda vizuri pindi mipira ya krosi inapokuja langoni
mwao.

Mfano katika mechi dhidi ya Huddersfield town, Otamendi alijifunga
kutokana na krosi iliyopigwa langoni mwao, Westham United walifunga
goli pia kutokana na krosi. Mifano hii inaonesha dhahiri Manchester
City hawajui kukaba vizuri pindi krosi zinapokuja kwao.

Ushindi mwembamba wa mechi za hivi karibuni inaonesha timu nyingi
zimeshajua kucheza na Manchester City?

Kadri muda unavyozidi kwenda kasi ya Manchester City katika viwanja
vya ugenini imeanza kupungua.

Mwezi wa kumi na mbili, wamefungwa na Shakhtar Donetsk katika michuano
ya UEFA ikiwa ndiyo mchezo pekee ambao msimu huu wamepoteza.

Wakaja kushinda ushindi mwembamba dhidi ya Newcastle United katika
uwanja wa St. James Park, pia wakaja kutoa suluhu na Crystal Palace
katika uwanja wa nyumbani wa Crystal Palace.

Hii inaonesha kasi yao inapungua pale wanapocheza katika viwanja vya ugenini.

Hali ya hewa ya uwanja wa Anfield itakuwa na nguvu kwa Liverpool?

Bila shaka Liverpool wanafaida kubwa ya kucheza katika uwanja wa
nyumbani. Uwanja ambao una mashabiki walevi wa soka wanaosimama na
wachezaji mwanzo hadi mwisho wa mchezo, hii itakuwa faida kubwa kwa
liverpool kwa sababu wachezaji wake watatiwa nguvu kubwa kutoka kwa
mashabiki.

Rekodi ya mbaya ya Manchester City pale Anfield ina nguvu kubwa kwenye
hii mechi???

Manchester City hawajawahi kushinda katika uwanja wa Anfield kwa miaka
15 mfululizo. Mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2003.

Rekodi hii inaweza ikaathiri pande zote mbili kutokana na jinsi gani
kila upande itakavyochukulia.

Mfano, kama Manchester City wataichukulia kwa hofu rekodi hii basi
watakuwa na nafasi kubwa ya kucheza kwa hofu, na unapocheza kwa hofu
unapata nafasi kubwa ya kufanya makosa mengi binafsi ambayo yanampa
nafasi adui kukuadhibu.

Ila kama wakiichukulia rekodi hii kawaida watacheza kwa utulivu zaidi,
tofaufi na kama ambavyo watakavyopania kuivunja rekodi hii kwa sababu
watajikuta wanafanya makosa mengi binafsi kutokana na kutokuwa makini.

Liverpool rekodi hii inawapa nafasi kubwa ya kuingia bila hofu hali
ambayo itawafanya wajiamini, ila wakijiamini kupitiliza kutakuwa na
madhara makubwa kwao tofauti na kama wakijiamini kiasi.

Rekodi ya Jurgen Klopp dhidi ya Pep ina nafasi gani katika mchezo wa leo?

Hakuna kocha mwenye rekodi nzuri dhidi ya Pep Guardiola kama Jurgen Klopp.

Wamekutana katika michezo 11, wote wameshinda michezo mitano na kutoka
sare mchezo mmoja kila mmoja.

Takwimu hizi zinaonesha Jurgen Klopp siyo mnyonge kwa Pep Guardiola
hali ambayo inamuongezea sababu ya yeye kushinda mechi ya leo.

Mashambulizi ya kushitukiza yana nafasi kubwa ya kuimaliza Manchester City?

Hapana shaka ndipo ilipo siri ya kuifunga Manchester City ambayo muda
mwingi hutamani kwenda mbele, hivo kuwatumia wachezaji wenye kasi kama
Saido Mane, Mohamed Salah kutakuwa na nafasi kubwa ya Liverpool kuwa
na nafasi ya kuwafunga Manchester City kupitia mashambulizi ya
kushitukiza.

Urejeo wa Mohamed Salah utakuwa na faida kubwa kwa Liverpool?

Hapana shaka,msimu huu akiwa na goli 22 kwenye mashindano yote na goli
17 kwenye ligi kuu ya England.

Ni mhimili mkubwa sana kwenye safu ya ushambuliaji ya Liverpool.Hivo
kurejea kwake kutakuwa kumeipa nguvu zaidi Liverpool.

Uwepo wa Van Djik una nafasi gani kwenye eneo la ulinzi kwa Liverpool?

Mechi ya mwisho Liverpool alifungwa goli 5-0. Liverpool ambayo ilikuwa
na matatizo ya ulinzi.

Tofauti na muda huu wanapokutana ambapo Liverpool kwenye sehemu yake
ya ulinzi kuna mabadiriko.

Gomez kwa sasa kaimarika tofauti na mwanzo ambapo timu hizi
zilivyokuwa zinakutana.

Amecheza kwa miezi 6 anaonekana kuimarika siku baada ya siku, Van Djik
ni beki bora na anakuja kuondoa makosa binafsi ambayo yalikuwa
yanafanywa kipindi cha nyuma na mabeki wa kati wa Liverpool.

Kupumzika siku tisa kwa Liverpool itakuwa na faida?

Manchester City wamecheza katikati ya wiki na kufanya mabadiliko
machache kwenye kikosi ila wachezaji wake muhimu kama Fernandhinho,
David Silva, Raheem Sterling, Sergio Aguero walianza.

Wakati huo Liverpool wakiwa Dubai, hii inawapa nafasi kubwa Liverpool
ya kutokuwa na uchovu tofauti na Manchester City

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Man U wamwendea Sanchez

Tanzania Sports

KWANINI LIVERPOOL WALIIFUNGA MANCHESTER CITY?