in , , ,

Kutoka TFF Leo……….


*SIMBA YALIMWA FAINI KWA KUENDEKEZA VITENDO VYA KISHIRIKINA

Wang’amuzi vipaji 28 wanakutana Lushoto mkoani Tanga kwa siku saba katika mpango maalumu wa maboresho ya Taifa Stars ambapo watatoka na orodha ya mwisho ya wachezaji waliopatikana katika mechi za maboresho hayo zilizochezwa nchi nzima.

Katika kikao hicho, wang’amuzi hao watapitia majina ya wachezaji walioteuliwa ikiwemo kuwaangalia tena kwenye video kwa vile mechi zote zilirekodiwa. Wachezaji watakaoteuliwa katika mpango huo baadaye wataingia kambini mkoani Mbeya.

Wang’amuzi vipaji ambao wanaoondoka Machi 9 mwaka huu kwenda Lushoto ni Abdul Mingange, Boniface Pawasa, Charles Mkwassa, Dan Korosso, Dk. Mshindo Msolla, Edward Hiza, Elly Mzozo, Hafidh Badru, Hamimu Mawazo, John Simkoko, Jonas Tiboroha, Juma Mgunda na Juma Mwambusi.

Kanali mstaafu Idd Kipingu, Kenny Mwaisabula, Madaraka Bendera, Madaraka Selemani, Mbarouk Nyenga, Mohamed Ally, Mussa Kissoky, Nicholas Mihayo, Peter Mhina, Salum Mayanga, Salvatory Edward, Sebastian Nkoma, Sekilojo Chambua, Selemani Jabir na Shabani Ramadhan.

Wengine ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Kidao Wilfred, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana, Ayoub Nyenzi, Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi na Mshauri wa Rais (Ufundi), Pelegrinius Rutayuga.

MUJUNI KUICHEZESHA AFC LEOPARDS CC

Mwamuzi Israel Mujuni ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu (CAF) kuchezesha mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho (CC) Afrika kati ya wenyeji AFC Leopards ys Kenya na SuperSport United ya Afrika Kusini.

Mujuni katika mechi hiyo itakayochezwa kesho (Machi 8 mwaka huu) jijini Nairobi, Kenya atasaidiwa na Samuel Mpenzu, Josepht Bulali wakati mwamuzi wa mezani atakuwa Ramadhan Ibada.

Kamishna wa mechi hiyo ni Amir Hassan kutoka Mogadishu, Somalia. SuperSport United ilishinda mechi ya kwanza iliyochezwa wiki mbili zilizopita mabao 2-0.

SIMBA YALIMWA FAINI KWA KUENDEKEZA VITENDO VYA KUSHIRIKINA
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga faini ya jumla ya sh. milioni moja klabu ya Simba kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo vitendo vinavyoashiria ushirikina uwanjani.

Simba ilifanya vitendo hivyo katika mechi yake dhidi ya Mbeya City ambapo imepigwa faini ya sh. 500,000. Pia imepigwa faini nyingine ya sh. 500,000 kwa makocha wake Loga, Selemani Matola na Idd Pazi kuingia uwanjani na kumzonga mwamuzi kwenye mechi hiyo.

Naye mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushangilia bao alilofunga kwenye mechi hiyo kwa kuonesha ishara ya matusi kwa kidole.

Mbeya City imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa washabiki wake kuingia uwanjani kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa mjini Bukoba. Klabu za Yanga na Coastal Union zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa washabiki wao kurusha chupa za maji uwanjani wakati timu hizo zilipopambana jijini Tanga.

Kiungo wa Mtibwa Sugar, Shabani Nditi amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumpiga mchezaji wa Simba, wakati Salvatory Ntebe pia wa Mtibwa Sugar amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtukana refa kwenye mechi dhidi ya Mbeya City.

Pia mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Musa Mgosi amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kosa la kupiga uwanjani kwenye mechi dhidi ya Ashanti United ambapo vilevile atakosa mechi tatu za ligi. Coastal Union imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa washabiki wake kumrushia chupa za maji kipa wa Mbeya City.

Nayo JKT Ruvu imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi dhidi ya Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Vilevile wamiliki wa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wameandikiwa barua ya kufanya marekebisho ya vyumba vya wachezaji, kwa vile havina hewa ya kutosha.

Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) klabu zilizopigwa faini kutokana na makosa mbalimbali ni Friends Rangers (sh. 200,000), Lipuli (sh. 200,000), Majimaji (sh. 400,000), Polisi Morogoro (sh. 400,000) na Transit Camp (sh. 200,000).

Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro, John Tamba atapelekwa kwenye Kamati ya Maadili kutokana na vitendo visivyo vya kimaadili katika mechi dhidi ya Burkina Faso.

Kiongozi wa Lipuli, Hamis Kiemba na wachezaji Boniface Sawaka, George Enock na Green Paul watapelekwa katika Kamati ya Nidhamu kutokana na utovu wa nidhamu waliofanya kwenye mechi dhidi ya Kimondo.

Naye mchezaji Sangalau Nyamoka wa JKT Kanembwa aliyelalamikiwa uhalali wake na Polisi Tabora suala lake linapelekwa Kamati ya Nidhamu.

COASTAL, ASHANTI KUUMANA MKWAKWANI VPL

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Machi 8 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo Coastal Union itaumana na Ashanti United kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Ruvu Shooting itaikaribisha Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwania wakati Mbeya City itacheza na Rhino Rangers kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za Jumapili (Machi 9 mwaka huu) ni Tanzania Prisons na Simba kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, na JKT Ruvu na Mtibwa Sugar zitacheza Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

FDL KUTIMUA VUMBI WIKIENDI

Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea wikiendi hii kwa timu za makundi yote matatu kushuka kwenye viwanja tofauti nchini ambapo kesho (Machi 8 mwaka huu) Tessema itacheza na Transit Camp kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Kundi B ni Burkina Faso vs Kurugenzi (Jamhuri, Morogoro) wakati C Polisi Tabora vs Mwadui (Ali Hassan Mwinyi), Stand United vs Pamba (Kambarage), Polisi Mara vs Kanembwa JKT (Karume) na Polisi Dodoma vs Toto Africans (Jamhuri, Morogoro).

Mechi za Jumapili ni kundi A, African Lyon vs Polisi Dar (Karume), Villa Squad vs Friends Rangers (Mabatini, Pwani) na Ndanda vs Green Warriors (Nangwanda Sijaona, Mtwara). Kundi B ni Polisi Morogoro vs Majimaji (Jamhuri, Morogoro) na Mlale JKT vs Lipuli (Majimaji, Songea).

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Messi atapika uwanjani

Moyes ashukuru mashabiki kumvumilia