in , ,

KUTAFUTA BALLON D’OR KWAANZA:

 

Ronaldo & Messi, Aguero & Toure
*Hazard, Alexis Sanchez ndani
*Wenger, Mourinho ukocha bora

Mchakato wa kupata mwanasoka bora wa dunia, maarufu kama Ballon d’Or umeanza, ambapo majina 23 yametolewa, likiwamo la anayeshikilia tuzo hiyo, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, hasimu wake, Lionel Messi wa Barcelona pamoja na wachezaji watatu wa Manchester City.

Vinara hao wa Ligi Kuu ya England wanaotaka kuwapoka Chelsea taji wametoa mshambuliaji wao kutoka Argentina, Sergio Aguero, kiungo Kevin De Bruyne wa Ubelgiji na yule wa Ivory Coast, Yaya Toure.

Sura mpya zilizoingia kwenye orodha hiyo kutokana na kufanya vyema kisoka ni Eden Hazard wa Chelsea na Alexis Sanchez wa Arsenal ambao msimu uliopita walichanua vilivyo na klabu zao. Kama ilivyotarajiwa, Ronaldo na Messi ambao wametamba kwa kugawana tuzo hiyo misimu saba iliyopita, wanaongoza msururu huu.

Mchezaji pekee wa Uingereza aliyeingia kwenye orodha hiyo ni winga wa Real Madrid na Wales, Gareth Bale. Mlinzi pekee ni Javier Mascherano wa Barcelona na kipa ni mmoja tu, Manuel Neur wa Bayern Munich ambaye msimu uliopita pia alikuwapo.

Ligi Kuu ya Hispania – La Liga imetoa wachezaji 11, Bundesliga ya Ujerumani ikiwa nao sita, wawili kutoka Italia mmoja kutoka Ufaransa, naye ni mshambuliaji wa kati wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic.

Orodha kamili ya wachezaji, nchi na timu wanazochezea na walizokuwa msimu uliopita ni: Sergio Aguero (Argentina/Manchester City), Gareth Bale (Wales/Real Madrid), Karim Benzema (Ufaransa/Real Madrid), Cristiano Ronaldo (Ureno/Real Madrid) na Kevin De Bruyne (Ubelgiji/VfL Wolfsburg/Manchester City).

Advertisement
Advertisement

Wengine ni Eden Hazard (Ubelgiji/Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Sweden/Paris Saint-Germain), Andres Iniesta (Hispania/ Barcelona), Toni Kroos (Ujerumaniy/Real Madrid), Robert Lewandowski (Poland/FC Bayern Munich) na Javier Mascherano (Argentina/ Barcelona).

Kama ilivyoelezwa awali, yumo Lionel Messi (Argentina/ Barcelona), Thomas Muller (Ujerumani/ Bayern Munich), Manuel Neuer (Ujerumani/ Bayern Munich), Neymar (Brazil/ Barcelona), Paul Pogba (Ufaransa/Juventus) na Ivan Rakitic (Croatia/ Barcelona).

Mkongwe Arjen Robben (Uholanzi/Bayern Munich) amerudi na pia wamo James Rodriguez (Colombia/Real Madrid), Alexis Sanchez (Chile/Arsenal), Luis Suarez (Uruguay/ Barcelona), Yaya Toure (Côte d’Ivoire/Manchester City) na Arturo Vidal (Chile/Juventus/ Bayern Munich).

Kwa upande wa makocha, yule wa Chelsea, Jose Mourinho na wa Arsenal, Arsene Wenger wamejumuishwa kwenye orodha ya watu 10 wanaowania  nafasi ya ukocha bora. Watachuana na yule wa Barcelona, Luis Enrique, aliyewawezesha Barca kutwaa mataji matatu msimu uliopita ikiwa ni pamoja na ubingwa wa Ulaya.

Kadhalika yumo kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola. Orodha kamili, uraia na timu wanazofundisha ni Massimiliano Allegri (Italia/Juventus), Carlo Ancelotti (Italia/Real Madrid), Laurent Blanc (Ufaransa/Paris Saint-Germain), Unai Emery (Hispania/Sevilla), Pep Guardiola (Hispania/FC Bayern Munich), Luis Enrique (Hispania/FC Barcelona), Jose Mourinho (Ureno/Chelsea), Jorge Sampaoli (Argentina/Timu ya Taifa ya Chile), Diego Simeone (Argentina/Atletico Madrid), Arsene Wenger (Ufaransa/Arsenal).

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Newcastle waona mwezi

Tanzania Sports

Pistorius atoka jela