Mashindano ya COSAFA yalimalizika wiki iliyopita, timu ya taifa ya
Tanzania ilifanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye mashindano hayo.

Nafasi hii ya tatu ndiyo mafanikio makubwa ambayo Tanzania ndiyo
imewahi kufikia katika mashindano haya.

Siyo jambo la kubeza hata kidogo, kuna kila haja ya kumpongeza kocha
Mayanga, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wote wa timu ya taifa.

Mafanikio waliyopata siyo haba hata kidogo, lakini siyo mafanikio
ambayo yanatakiwa yatulevye sisi hata kidogo.

Kwanini tunatakiwa tusilewe na mafanikio haya ?

Ukiangalia timu ambazo zilikuwepo katika mashindano haya ya COSAFA ni
timu ambazo nyingi zilileta vikosi vya ziada na siyo vikosi kamili
mfano timu ya taifa ya Afrika Kusini, Zimbambwe, Zambia.

Hii inaonesha ushindani ulikuwa siyo mkubwa sana ukilinganisha na kama
wangeleta vikosi vya kwanza vya timu zao za taifa.

Hii haitupi nafasi ya kujivunia kuwa tulienda kushindana na washindani
haswa jambo ambalo halitakiwi litupe nafasi ya sisi kulewa na
mafanikio haya na kusahau vita iliyopo mbele yetu na kuridhika na
COSAFA.

Kilicho mbele yetu ni mechi za kufuzu CHAN na mechi za kufuzu AFCON.
Hii ndiyo vita kubwa tuliyonayo mbeleni.

Vita ambayo kila mpinzani huleta kila aina ya silaha anayoiamini kwa
ajili ya kushinda vita, ndipo hapa utofauti kati ya COSAFA na hizi
mechi unapoanzia.

Ushindani kwenye hizi mechi za kufuzu CHAN na AFCON ni mkubwa sana
kuliko ushindani wa COSAFA. Kitu ambacho hatutakiwi kabisa kukaa na
kujisifu kuhusu COSAFA.

Kitu cha muhimu ambacho tunatakiwa tukipate kutokana na mafanikio ya
COSAFA ni ile tabia ya ushindi tuliyoipata kwenye mashindano hayo
tuiishi ndani yetu twende nayo na kwenye mechi hizi zinazotukabili.

Ushindi wa COSAFA utumike kama nguzo kubwa ya sisi kutujengea hali ya
kujiamini kuwa tunaweza kwa kiasi kikubwa kushinda mechi.

Huu siyo muda wa kufurahia matokeo ya COSAFA, ila ni muda wa kuyatumia
matokeo ya COSAFA katika njia chanya ili yaweze kutusaidia kwa kiasi
kikubwa katika mechi zinatotukabili.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

LUKAKU HATOSHI, NI LAZIMA POGBA AREJESHE MAKALI YAKE

Tanzania Sports

MCHEZO WA KIRAFIKI KATI YA GOR MAHIA NA EVERTON