in

Korona Inavyoendelea kuwaadhibu Wachambuzi

wachambuzi wa soka

Ligi mbalimbali duniani zimerudi ila bado mambo yamebana kwa wachambuzi kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine.

Kipindi cha nyuma tuliwahi kuangalia namna wachambuzi wa soka wanavyokufa njaa  baada ya kuingia ugonjwa wa Korona, sasa ligi zimerudi ila mambo bado  magumu ‘nganganga’.

Kwa nchi za Afrika tumezoea wakati huu wachambuzi wetu nguli wanaenda Afrika Kusini wanachambua soka kisha wanarejea.

Hii hatua kubwa sana hasa wanakitangaza Kiswahili pili wanajipatia kipato cha kujikimu kimaisha.

Lakini bado athari za Korona zinaonekana kuwatafuna kwakuwa kuna baadhi ya nchi bado hazija kaa vizuri juu ya ugonjwa huo.

Tanzania kwa uwezo wake Mungu kwa sasa hakuna mgonjwa yoyote watu wanadunda ila kwa nchi nyingine bado janga ni kubwa mno.

WALIENDA WAPI ?

Kwa wachambuzi wa Kitanzania walikuwa wanaenda Afrika Kusini kutangaza mechi, kuna kampuni ilikuwa inawachukua wanatia saini ya mikataba wanapata hela nzuri wanaenda huko wanafanya kazi vizuri kisha wanarejea.

Lakini tangu Korona na hata angalau ilivyopungua ligi zimerejea na zinaendelea bado kumekuwa pagumu kuvuka viunzi kufanya kazi zao.

Hii michongo ya Korona imekuja kuharibu kitumbua chetu kiingie mchanga.

Lakini naamini muda si mchache kila jambo litarudi sawa na tutaishi kwa mazoea kama ilivyokuwa awali.

FAIDA YA WACHAMBUZI WETU KWENDA HUKO

Faida kubwa wanayoipata kwanza kipato, pili wanaitangaza Tanzania  tatu lugha yetu ya Kiswahili inapata kusikika sehemu kubwa hivyo nayo inakuwa katika mlolongo wa kutangazwa.

Faida nyingine inatengeneza ajira kwa vijana wengi, wale wakongwe wanapoenda huko huku nyuma katika vituo vyao kuna vijana wanakuja kufanya deiwaka na kama wakifanya vizuri huenda wakafikiriwa na baadae kula shavu, hivyo wigo wa ajira unazidi kupanuka.

Najua kunabaadhi watajua nafurahia wachambuzi kukosa kwenda huko hapa sote njia moja ila leo angalau tumejiongelea wenyewe  sio kila siku story nyingine wakati na sisi tunazo stori.

MAKALA YETU YA NYUMA JUU YA UGONJWA HUO

Alosto ya kukosa kushuhudia mechi za ligi mbalimbali duniani ni kubwa kuliko kula chakula unachokipenda zaidi hasa ubwabwa, kwa wanamichezo watakuwa wanaelewa namna tulivyokuwa tunataabika kukosa ligi mbalimbali.

Kwa kawaida imezoeleka ikifika mwezi Mei hadi Juni ligi zote zinakuwa zimemalizika na tunakaa miezi miwili kisha tunarudi mzigoni katika maisha yetu ya kawaida ya michezo.

Hapa Afrika Mashariki mashabiki wengi wa Manchester United ikifuatiwa na Arsenal huku Liverpool wakiwa wamejikusanya tena Chelsea nayo ipo humo basi huwa kuna utani sana kila wiki kutokana na matokeo ya timu hizo.

Maisha ya kutaniana baina ya timu hizo yamekuwa na afya kubwa kwa wanamichezo na wengi wamekikosa kwa miezi mitatu nyuma kutokana na ugonjwa huo.

Sasa maambukizi ya virusi vinavyosabisha Korona(COVID-19) iliharibu mipango mbalimbali ya wanamichezo hasa wachambuzi wa soka katika kupiga mkwanja.

RAMANI ILIUNGUA HIVI!

Kwa Afrika kukosekana kwa kuendelea kwa ligi kubwa kumeathiri sana maisha ya wachambuzi ‘Pundit’ katika vituo mbalimbali vya Televisheni (TV).

Baadhi ya wachambuzi kutoka Tanzania na sehemu mbalimbali za Afrika walikuwa wanaenda Afrika Kusini kutangaza mechi za ligi pendwa na wengine kuchambua huwa wanapata pesa nyingi sana, ina kadiriwa wanalipwa hadi kiasi cha dola mia tano, hii yote kutokana na utajiri wa matangazo yanayotokana na michezo kitu kimoja kinachoitwa Korona kimekuja kumwaga mboga za wachambuzi na watangazaji.

Kwa Tanzania iliathiri kabla mambo kwenda sawa na ugonjwa kuisha kwa mifano halisi inaonekana karibuni vituo vyote vina vipindi vya michezo na kuna baadhi ya wachambuzi hualikwa katikavituo hivyo japo malipo yao sio mazuri sana lakini yalikuwa yanasogeza maisha yao kwa wahusika.

Ilivyokuja Korona ilifanya kila  kituo kuogopa kupokea wageni kwa kujihami kwa kuenea maambuzi ya virusi, hiyo ni athari moja wapo ya ugonjwa huo.

Mfano huu unafanana kabisa na nchi nyingi za Kiafrika mara nyingi zinafana kwa kila matukio yao, inatokana na mfumo wa michezo barani humo.

Kuna wale wa kupiga pesa kupitia tiketi za uwanjani nao wamekosa ulaji huu kutokana na janga hili, hii inategemea sana na dua pamoja na sala kuomba ugonjwa huu uishe  hapa Bongo zilifanyika nazilifanikiwa.

Huko duniani vituo kama Sky Sports, BBC Sports na vituo vingine navyo vilisimamisha shughuli hii kwa kupisha ugonjwa wa Korona.

Wachamvuzi wengi walikuwa wanafanyia uchambuzi wao nyumbani wanaunganishwa na Internate wnaongea ambapo ni kitu cha tofauti kabisa.

Kwa wale waliokuwa wanafanya kazi viwanjani nako hakuliki sasa maana hakuna kinachoendelea hii kwa nchi zaUlaya bado inaendelea.

Kwa wale wa vibandau umiza nao walikosa hela kwani watazamaji walikuwa wanajazana kuangalia ligi mbalimbali duniani ila kabla ya hapa Tanzania kuruhusu walikuwa hawaingii.

Moja ya wamiliki wa Kibandaumiza maarufu sana hapa Kinondoni Moscow Dar es Salaam, Uwesu Ngwabi ameichukulia Korona kama changamoto nyingine ila alikiri kukosa fedha nyingi sana kupitia kuonesha ligi mbalimbali.

Amesema kuwa kila wiki alikuwa na uhakika wa kuingiza laki mbili na hamsini kwa kuonesha mechi mbalimbali, tangu uingie ugonjwa huo hajapata kabisa kiasi hiko kwa wiki.

“Huu ugonjwa noma sana, umeniharibia kuongeza kipato changu, kwa miezi hii miwili nimekosa laki mbili na nusu kila wiki kuonesha ligi mbalimbali,”alisema.

Aliweka bayana kuwa ligi kuu Uingereza maarufu kama ‘EPL’ ndio sehemu kubwa inayomuingizia kipato huku mechi za ligi kuu Tanzania bara inapocheza Yanga au Simba watu wanajaa sana na ndio sehemu ya kupiga pesa.

“Ligi kuu Uingereza inanipa fedha nyingi sana hasa washabiki wengi wanapenda timu za huko kuliko ligi nyingine, kwa hapa nyumbani Yanga na Simba inapocheza na timu yoyote nako natengeneza mpunga mwingi(fedha) sana,”aliongeza.

Mchambuzi wa michezo anayekuja kwa kasi nchini Tanzania, Yahya Njenge yeye aliitizama Korona katika sekta hiyo kwa jicho la pili.

Amekubali kuwa wachambuzi wengi wanategemea michezo kuweza kualikwa na kutengeneza kipato hivyo kiuchumi imeathiri sana,” Alisema Njenge.

Pia amesema vipindi vyenyewe vya michezo vilipooza sana kwa kuwa hakuna matukio ya maana ya kuyachambua hivyo vipindi vingi vinakosa ladha vinakuwa katika mlengo wa kuangalia historia za wachezaji wa zamani au takwimu zilizopita.

“Vipindi vyenyewe vilipooza sana kwakuwa hakuna maudhui na matukio yaliyo bora ya kuchambua, kwa aina hiyo pia inawaboa wasikilizaji wetu, vipindi vingi vimepooza sana,”aliongeza.

Hata hivyo Burundi ilikuwa nchi ya kwanza kurudisha ligi ikafuatiwa na Tanzania, sasa duniani kote ligi imerudi changamoto watazamaji kuingia uwanjani.

Janga hili kama ilivyo majanga mengine yaliyowahi kupita, mfano Surua,Pepopunda na Ukwimi na kwa uwezo wa Mugu litapita maisha mengine yataendelea.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Watkins

Samatta,Watkins, majibu mwisho wa msimu..

Alex Telles

Manchester United taabani