in , , ,

KISU ‘KILICHOIUA’ MISRI NA MOROCCO ‘KIMEIUA’ TUNISIA

Inawezekana ikawa ni moja ya timu ambayo ilikuwa haipewi nafasi ya kufanya vizuri katika michuano hii ya kombe la dunia, lakini jana England walianza vizuri safari yao baada ya kuifungaTunisia goli mbili kwa moja.

Ilikuwa sawa kwa Tunisia kukaa nyuma ya mpira muda mrefu?

Tunisia walikaa nyuma ya mpira muda mrefu na kubaki kuwa wanakabia juu kwa muda mrefu ndani ya mchezo.

Kwangu mimi sikuona sababu ya Tunisia kukaa nyuma ya mpira muda mrefu kwa sababu England ilikuwa na safu ya ulinzi ambayo ilikuwa inafanya makosa binafsi kipindi ambacho ilikuwa inatiwa presha, laiti kama Tunisia wangetia presha kubwa katika lango la timu ya taifa ya England walikuwa na uwezo wa kupata alama kwenye mchezo huu.

Kwa mantiki hii, England anatakiwa awe makini kipindi ambapo atakapokutana na timu ya kiwango cha juu kwa sababu safu yao ya ƴulinzi inafanya makosa binafsi.

Kumchezesha Walker kama beki wa kati kulikuwa na faida kwa England?

Hapana shaka kulikuwa na faida ndogo sana, ni eneo ambalo ilikuwa mara ya kwanza kwake yeye kucheza eneo lile hali ambayo ilikuwa inampa kutojiamini vizuri kama ambavyo huwa anacheza kama beki wa pembeni kulia.

Mfumo wa 3-5-2 unaonekana na faida kwa Gareth Southgate?

Tangu mwaka jana mwezi wa kumi na mbili (12) Gareth Southgate aliamua kuanza kutumia mfumo wa 3-5-2. Mfumo ambao umemfanya mpaka sasa hajafungwa katika mechi kumi (10) zilizopita, ambapo amefunga mechi nane (8) na kutoka sare mechi mbili (2).

Jordan Henderson au Eric Dier??

Katika mfumo wa 3-5-2 unahitaji mabeki wacheza mpira pamoja na viungo wacheza mpira. Gareth Southgate alianza na John Stones, Walker na Maguire kama mabeki wacheza mpira. 

Mbele yao alikuwepo Jordan Henderson. Kwa mechi ya jana Jordan Henderson alikuwa na faida sana kwa sababu alikuwa anaipeleka timu mbele na pasi zake ndefu saba alizopiga jana, pasi sita zilifika. Na kitu kikubwa ambacho alikuwa nacho na Eric Dier hana ni uwezo wa yeye kuwa kiongozi. 

England inakosa msaidizi wa Kane?

Hapana shaka huu ni ukweli uliowazi. Baada ya England kuamua kutafuta goli, alikosekana mtu wa kusaidizana na Harry Kane.

Raheem Sterling na Jesse Lingard hawana rekodi nzuri na timu ya taifa, mfano Raheem Sterling amefunga magoli mawili katika mechi thelathini na tisa na jana hakuonesha kuisaidia timu sana mpaka walipoingia Marcus Rashford na Ruben Loftus Cheek ambao waliweza kuweka presha iliyoisaidia England.

Kwanini timu za Africa zinafungwa magoli ya jioni?

Umakini hafifu kwenye dakika za mwisho ndiyo hufanya timu za Afrika kufungwa goli la jioni.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

WALICHOKOSA UJERUMANI, KILIKUWEPO KWENYE BENCHI LA BRAZIL

Tanzania Sports

HISPANIA WAMSAHAU JULEN LOPETEQUI NA KUIKUMBUKA BENDERA YAO