in , , ,

Kipa Ospina asajiliwa Arsenal

*Mourinho aubeza mshahara wa Shaw

* Ferdinand aanza Queen Park Rangers
 
Wakati Arsenal wamekamilisha usajili wa golikipa wa Timu ya Taifa ya Colombia, David Ospina, Queen Park Rangers (QPR) wameanza kupata huduma za mabeki wa kati Rio Ferdinand na Steven Caulker huku Jose Mourinho akimvaa Luke Shaw.

Arsenal wamefanikisha usajili wa kipa ambaye aliruhusu mabao machache zaidi katika hatua za makundi kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil majuzi, taarifa hiyo ikiwa imetolewa na kocha wa klabu yake ya Nice, Claude Puel.

Ospina (25) amekuwa na klabu hiyo ya Ufaransa tangu 2008 na alisaidia nchi yake kufika hatua ya robo fainali na kocha Puel alisema Arsenal watafurahi kwani Ospina ni kipa mzuri sana.
image

Pasipo kuthibitisha usajili huo, Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alijibu swali la waandishi wa habari kwa kusema aliamini kwamba kipa huyo alifanya vyema sana kwenye michuano ya Kombe la Dunia.

Wenger amepata kunukuliwa akisema kwamba kuna uwezekano wa Ospina kumpoka namba kabisa kipa namba moja wa Arsenal, Mpolishi Wojciech Szczesny. Ospina alicheza dakika zote za mechi zote za Colombia na nchi hiyo iliruhusu pia mabao machache zaidi miongoni mwa timu za Amerika Kusini wakati wa mechi za kufuzu.

Ospina ndiye alichukua mikoba ya Hugo Lloris aliposajiliwa na Tottenham Hotspur kutoka Lyon lakini kabla ya hapo alikuwa Nice.
 
 
MOURINHO ASEMA SHAW GHALI MNO
20140402-155822.jpg

 
Kocha wa Chelsea,  Jose Mourinho ameendelea kuzungumzia masuala ya wachezaji wa timu nyingine, akiwashangaa Manchester United kumsajili beki wa kushoto wa Southampton ambaye ni ghali sana.

Mourinho amedai kwamba madai ya mshahara mkubwa ya Shaw yangeweza ‘kuiua’ Chelsea. Shaw alisajiliwa kwa pauni milioni 27 na amekuwa akiwaniwa na timu nyingi, ikiwa ni pamoja na Arsenal na Liverpool.

Mreno huyo amedai Shaw kulipwa pauni 100,000 kwa wiki ni kiasi kikubwa mno, lakini Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amedai kwamba atakaa faragha na Mourinho kuzungumzia suala hilo.

“Tukimlipa kijana mwenye umri wa miaka 19 kile tulichotakiwa kumlipa, basi kumsajili Luke Shaw kungetuua. Tungeua uthabiti wetu huku tukitakiwa kuzingatia uungwana katika matumizi ya fedha, sasa ukimlipa kijana mdogo kiasi hicho basi kesho yake wengine watakuvamia kutaka nyongeza,” akasema Mourinho.

Mourinho anajenga hoja kwamba si sahihi mchezaji mpya na mwenye umri mdogo kiasi hicho kulipwa kuliko wakongwe ambao wamechezea klabu mechi hadi 200, kuiletea mataji na sifa nyingi.
 
FERDINAND, CAULKER WAANZA KAZI QPR

20140718-150851-54531954.jpg

Mabeki wapya wa kati wa Queen Park Rangers (QPR), Rio Ferdinand na Steven Caulker wameanza rasmi majukumu katika klabu hiyo iliyopanda daraja msimu huu baada ya kuwa imeshuka msimu uliopita.

Waingereza hao wawili walicheza dakika 45 kila mmoja katika mechi ya kirafiki nchini Ujerumani kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu ya England inayoanza mwezi ujao. Ferdinand alianza kufundishwa soka ya kulipwa na kocha wa sasa wa QPR, Harry Redknapp.

Katika hatua nyingine, QPR wameamua kumrejesha kipa wao, Julio Cesar (34) wa Brazil aliyekuwa ametolewa kwa mkopo katika klabu inayocheza Ligi ya Marekani ya Toronto FC. Kipa mwingine katika QPR ni Mwingereza, Robert Green.

Wakati huo huo, West Ham United wamepata pigo kubwa, baada ya mshambuliaji wao wa kutegemewa kuumia enka na hivyo atakuwa nje ya dimba kwa miezi karibu minne, ikimaanisha ataanza kucheza Novemba.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Bondia Kidunda hoi Madola

Man U kutosajili hovyo