in , , ,

Kimenuka Hispania

*Zijue sababu za anguko lao

Baada ya Hispania kutolewa kwenye hatua za awali katika fainali za Kombe la Dunia, Kocha Mkuu Vincente Del Bosque amesema hatima yake na baadhi ya wachezaji ipo shakani.

Akizungumza baada ya kichapo cha 2-0 kutoka Chile kilichowatupa nje ya mashindani licha ya kuwa mabingwa watetezi, Del Bosque amesema wakati wa maamuzi magumu umewadia.

Hispania waliochakazwa 5-1 na Uholanzi ambao walicheza nao fainali 2010 Afrika Kusini wanatakiwa kujipanga upya kulinda heshima ya Hispania, amesema kocha huyo mkongwe aliyekataa ofa ya kuwafundisha Manchester United mwaka huu.

Amekiri wachezaji wake walikuwa legelege na hawakutia jitihada, maarifa wala ujasiri lakini akasema pamoja nao, naye anaingia kwenye mkumbo wa lawama.

Wanakuwa mabingwa watetezi wa tano kutolewa katika hatua za mwanzo. Baadhi ya sababu za kushindwa kwao ni pamoja na Del Bosque kung’ang’ania wachezaji waliopitwa na wakati katika mechi ya kwanza.

Hao ni pamoja na Xavi Hernandez, Gerard Pique, Iker Casillas wakati kuna watu kama Pedro Rodriguez, Javi Martinez, Koke, David da Gea.

Ngome ya Hispania ilikuwa inavuja tofauti kabisa na enzi za mafanikio ya 2010 na 2012 ambapo uimara wa ngome ndio uliwapaisha hadi wakatwaa ubingwa wa dunia na Ulaya.

Diego Costa naye anaonekana kuwa tatizo kwa sababu za kisaikolojia, ambapo amezaliwa na kukulia Brazil, lakini Hispania ikamng’ang’ania kwa sababu tu ameishi huko miaka sita au zaidi.
Alishindwa kutamba nyumbani alikozaliwa na kupakana. Kadhalika hawakumjenga vyema Costa kuwafaa katika mfumo wao, kwani yeye anajua mchezo wa kasi tu.

Hispania wameshindwa kwenda na mabadiliko kwa kung’ang’ania mfumo uliokuwapo kwa muda mrefu kwa kutegemea wachezaji wa Barcelona zaidi waliojengwa na Pep Guardiola.

Leo hii Guardiola hayupo, Barca wamebadili makocha mara tatu, Barca wapo hovyo na hawakuambulia kombe msimu ulioisha na sasa wameiambukiza Timu ya Taifa ya Hispania.

Kigezo cha kucheza Amerika Kusini ni kingine kinachowaangusha Hispania, kwani mataifa ya huko yamejizatiti kubakisha kombe. Mwaka mmoja uliopita hapo hapo Maracana Hispania walicharazwa 3-0 na Brazil kwenye fainali ya Kombe la Mabara.

Mataifa ya Amerika Kusini yana washangiliaji wengi sana, na mwanzo wa mwisho wa La Furia Roja ulikuwa mwaka jana, wakapokewa Brazil kwa kulambwa 5-1 na kuhitimishiwa na Chile 2-0, kocha Jorge Sampaoli akaondoka akimcheka Del Bosque. Ni wakati wa kufumua kikosi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Hispania watema ubingwa

Tembo wa Afrika…