in , ,

Kim Poulsen ametaja wachezaji 22 watakaoingia kambini

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 22 watakaoingia kambini Januari 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Morocco itakayochezwa Machi mwaka huu.

 

Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma saa 11.30 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza Januari 7 mwaka huu.

 

Wachezaji walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam. Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).

 

Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).

 

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

 

Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).

 

CAF YAMTUMA LIUNDA KUKAGUA VIWANJA ETHIOPIA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua ofisa wake Leslie Liunda wa Tanzania kwenda Ethiopia kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa utoaji leseni kwa klabu zitakazoziwezesha kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho hilo.

 

Ofisa huyo atawasili nchini Ethiopia kesho (Januari 2 mwaka huu) ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 6 mwakani na baadaye kupeleka ripoti yake CAF.

 

Utekelezaji wa kazi yake hiyo nchini Ethiopia utahusisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ethiopia (EFF), Wizara ya Michezo ya nchi hiyo, viongozi wa klabu na mameneja wa viwanja husika.

 

Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Matukio Makubwa ya Michezo 2012

Mancini ajipa matumaini