in , ,

KIKOSI CHA YOUNG TAIFA STARS CHATANGAZWA

Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza timu ya pili ya Taifa (Young
Taifa Stars) atakayoitumia kuangalia wachezaji ambao baadaye anaweza
kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo (Aprili 23 mwaka huu)
kabla ya kutaja kikosi hicho, Kim amesema timu hiyo ni sehemu ya Mpango wa
Maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliozinduliwa
Aprili 4 mwaka huu ukilenga kuendeleza wachezaji.

Amesema timu hiyo inajumuisha wachezaji ambao wamepita umri wa kuchezea
timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na
wakubwa ambao hawajapata fursa ya kuingia Taifa Stars, lakini atatumia
Young Taifa Stars kuangalia uwezo wao.

“Timu hii ni kiungo kati ya vijana na wakubwa. Wengi wa wachezaji watakuwa
vijana, lakini wakubwa wachache watapata fursa ya kuwemo ili kuangalia
uwezo wao hata kama uko nyuma waliwahi kuchezea Taifa Stars. Lakini timu
hii vilevile ni changamoto wa wachezaji wa Taifa Stars kuwa wapo
wanaosubiri wazembee ili wachukue nafasi zao,” amesema.

Young Taifa Stars yenye wachezaji 30 itakuwa na kambi ya siku tano jijini
Dar es Salaam kuanzia Mei 2 hadi 6 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar)
na Ali Mustapha (Yanga) ambao ni makipa. Mabeki ni Kessy Hassan (Mtibwa
Sugar), Kennan Ngoma (Barnsley FC, Uingereza), Himid Mao (Azam), Ismail
Gambo (Azam), David Mwantika (Azam), Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein
(Kagera Sugar), Waziri Salum (Azam), Samih Nuhu (Azam) na Emily Mgeta
(Simba).

Viungo ni Haruna Chanongo (Simba), Edward Christopher (Simba), Mudathiri
Yahya (Azam), William Lucian (Simba), Jonas Mkude (Simba), Hassan Dilunga
(Ruvu Shooting), Jimmy Shoji (JKT Ruvu), Abdallah Seseme (Simba), Ramadhan
Singano (Simba), Farid Mussa (Azam) na Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Jerome Lambele (Ashanti
United), Zahoro Pazi (JKT Ruvu), Twaha Hussein (Coastal Union), Abdallah
Karihe (Azam) na Juma Luizio (Mtibwa Sugar).

*AFRICAN LYON, JKT RUVU KUUMANA CHAMAZI*

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho
(Aprili 24 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya wenyeji African Lyon na JKT
Ruvu.

Mechi hiyo namba 165 itachezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam chini
ya usimamizi wa Kamishna Hamisi Kisiwa wa Dar es Salaam. Waamuzi wa mechi
hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Hashim Abdallah, Omari Kambangwa,
Abdallah Selega na Said Ndege wote wa Dar es Salaam.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Manchester United mabingwa

Fergie alivyorejesha kombe alilopoteza